Nini chanzo cha ongezeko la ajali za barabarani? Je, kipi kifanyike ili kupunguza ajari hizi?

Bornhero

Member
Nov 7, 2021
14
18
Hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko la ajari za barabarani ambazo zimesababisha vifo vya watu wengi je, unahisi ni sababu zipi ambazo zimepelekea ongezeko la ajari hizi? Na ni nini mwarobaini wa tatizo hili?
Karibuni kwa maoni na ushauri.
 
Dah rafiki yangu kafariki jana Tanzanite brigde dah
 
Ajali nyingi zinatoksna na uzembe,ujinga unao sababishwa na madereva kwa kutokuwa makini wawapo barabarani

Pili, miundombinu yetu ni mibovu

Ova
 
Madereva wengi hawana uzoefu masafa
Watakaosababisha ajali ya kifo wafunguliwe mashtaka na walipe faini kubwa

Lazima kuwe na ukaguzi wa magari mara moja kwa mwaka na mwenye Gari anapewa cheti cha ubora kwa mwaka lakini pia anaweza kugaguliwa mda wowote

Garage za kuangalia magari ziwepo kwa Amri ya serikali na hakuna rushwa
Gari ukiambiwa badili tairi ni lazima ubadili la sivyo Hakuna cheti hii itawafanya wenye garage wawabane wenye magari kubadili kila kitu kibovu na kunakuwa na mtandao unaounganisha traffic department na garages ambazo zitatoa taarifa kuwa hiyo gari imefeli haitakiwi kuwa barabarani

Hapo mwenye garage hawezi kukubali kutoa cheti fake ikijua gari mbovu maana dereva akishikwa imekula kwake

Pia sign post barabarani lazima ziwe nyingi kuwatahadharisha madereva
 
Hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko la ajari za barabarani ambazo zimesababisha vifo vya watu wengi je, unahisi ni sababu zipi ambazo zimepelekea ongezeko la ajari hizi? Na ni nini mwarobaini wa tatizo hili?
Karibuni kwa maoni na ushauri.
Ajari za balabalani.
 
Hii kwa bongo ngumu sna sabab ya rushwa ilioyokithiri. Kama barabarani tu trafick wanashindwa kuzuia gari bovu lisiendelee na safari itakuwa sembuse wamiliki wa garage ambao wanataka kazi?.
 
Juzi nimeweka uzi humu wa njia kuu Highways zote ziongezewe lanes ili gari za uelekeo mmoja zisikutane na za uelekeo mwingine hii itapunguza ajali.
 
Hii kwa bongo ngumu sna sabab ya rushwa ilioyokithiri. Kama barabarani tu trafick wanashindwa kuzuia gari bovu lisiendelee na safari itakuwa sembuse wamiliki wa garage ambao wanataka kazi?.

Tatizo traffic wana njaa nilishuhudia jamaa alipewa buku akapokea bila aibu
Wapo wanaoruhusu gari liendelee na safari likiwa limejaza kwa hongo

Huu upumbavu niliwasarukia traffic walipoturuhusu kuendelea na safari mimi niligoma nikashuka nikawaambia tena waambieni hao warudishe nauli yangu

Konda akanipa changu nikawaambia wanitafutie usafiri mwingine
Kiasi niko nao hawakuongea hata neno moja mpaka Bus lingine lilipofika

Hawa sio wa kuwachekea kama wote tukiwa na msimamo rushwa ingepungua
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom