Kwanini Morogoro iitwe ‘Mji kasoro bahari’?

chaUkucha

JF-Expert Member
May 28, 2012
3,382
1,208
Kwanini Morogoro unaitwa mji kasoro bahari wakati ni mikoa mingi Tanzania haina bahari?
 
Long time kitambo, mji wa Morogoro ulikuwa unakimbizana na Dar kiburudani. Moro kulikuwa Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, Salim Abdallah wote marehemu, band zao ziliufanya mji kuchangamka hasa,ndiyo maana wakafananisha na Dar kwamba kote kumekucha kwa burudani tofauti ni bahari pekee..
 
Kuna miji mingi hapa nchini ambayo haijapakana bahari lakini haiitwi miji kasoro bahari. Kwa ajuae, asili ya mji wa Morogoro kuita Mji kasoro bahari anijuze tafadhali.
 
Wakija pia wanioneshe na ziwa lililopo huko
Kifupi usemi huu maarufu umetokana na maudhui yaliyotumiwa ktk vibwagizo vya nyimbo za muziki za aliyekuwa msanii maarufu nchini marehemu Mbaraka Mwishehe aliyekuwa kiongozi wa bendi mashuhuri enzi hizo ya Super Volkano iliyokuwa na makazi yake mjini Morogoro. Msanii huyu alikuwa na mapenzi makubwa sana na mji wa Moro na alichangia sana kuu-promote kupitia nyimbo zake zilizokuwa zikipendwa sana Afrika mashariki yote. Nuru ya msanii huyu aliyekuwa kipenzi cha wengi Ilizima ghafla baada ya kupata ajali na kufariki akiwa ziarani nchini Kenya.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Wakija pia wanioneshe na ziwa lililopo huko
3028422243ae622f3ff2b15352107d5f.jpg
2daa95d96a8013f8094c1ecd0e9c72be.jpg
485257593a8fc35487474cff65529533.jpg
b32c067d765f52fb6478b63ad6f4b85b.jpg
924b6b3a420e751c5c494ed111286402.jpg
. mindu
 
Kifupi usemi huu maarufu umetokana na maudhui yaliyotumiwa ktk vibwagizo vya nyimbo za muziki za aliyekuwa msanii maarufu nchini marehemu Mbaraka Mwishehe aliyekuwa kiongozi wa bendi mashuhuri enzi hizo ya Super Volkano iliyokuwa na makazi yake mjini Morogoro. Msanii huyu alikuwa na mapenzi makubwa sana na mji wa Moro na alichangia sana kuu-promote kupitia nyimbo zake zilizokuwa zikipendwa sana Afrika mashariki yote. Nuru ya msanii huyu aliyekuwa kipenzi cha wengi Ilizima ghafla baada ya kupata ajali na kufariki akiwa ziarani nchini Kenya.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
nifuate instagram.utajua mengi (morogo yetu)
 
Mji kasoro bahari. Wanasema Ni mkoa wenye sifa zote zakuitwa jiji ila imekosekana bahari ili kujiongezea sifa pale kwenye kuitwa jiji
 
Ni kwanini morogoro a.k.a uitwe mjii kasoro bahari wakati Kuna miji mingi haina bahari
Ulikua usemi maarufu uliotokana na maudhui yaliyotumiwa kama vibwagizo vya nyimbo za muziki za aliyekuwa msanii maarufu nchini marehemu Mbaraka Mwishehe aliyekuwa kiongozi wa bendi mashuhuri enzi hizo ya Super Volkano iliyokuwa na makazi yake mjini Morogoro. Msanii huyu alikuwa na mapenzi makubwa sana na mji wa Moro na alichangia sana kuitangaza Morogoro kupitia nyimbo zake zilizokuwa zikipendwa zaidi Afrika mashariki.
 
Back
Top Bottom