Nini chanzo cha mijadala mingi isiyoisha? Je ni mfumo wetu wa Elimu?

Kasheshe,
Mkuu ktk hili nadhani unajaribu ku spin the issue kwa sababu tunachozungumza hapa ni hili swala la mitambo ya Dowans..
Kuna issue mbili hapa ambazo unajaribu kuziunganisha Short na Long term strategies..
Kwanza hakuna mwananchi anayepinga umuhimu wa Umeme na kwa nini serikali yetu imeshindwa kutekeleza long term plan ya kuzalisha umeme..Hilo halina ubishi wala mjadala iwe kwa wanasiasa, wasomi au wananchi kabuntas kama sisi.. mahitaji ya UMEME hayana elimu ya art wala Uhandisi isipokuwa ni chombo gani kinahitajika..tatizo ipo ktk utekelezaji wa short term plan ambayo tayari imekwisha fanyiwa kazi na hao hao wasomi wahandisi unaowazungumza.. wametumia art kutuzuga wananchi wote. sasa sijui walisomea art au Uhandisi.

Mkuu wangu kinachogomba hapa labda nikiweke sawa.. ni Hivi kama sisi tumekwenda kwa daktari na ametuandikia dawa ya maleria iwe Chloroquine, hakuna anayepinga maamuzi hayo, isipokuwa tunachopinga ni maamuzi ya mtu alioyekwenda dukani kununua dawa hiyo..Kwanza kanunua dawa toka kwa mlanguzi feki - made in India kwa gharama ambayo ni kubwa..Kinachogomba zaidi ni madai yake yanayolenga zaidi sababu za maradhi yetu na somo zito kuhusiana na Maleria wakati sisi tunachouliza ni kidogo sana why.. kinahusu hiyo dawa sio maradhi yetu..hatupati jibu!

Nachoomba hawa wahandisi unaotaka kuwasifia watueleze kwa undani kuhusu hii mitambo ya Dowans na sio kiza kinachotuandama, hilo tunafahamu toka mwanzo na ndio maana serikali iliwapa go ahead Tanesco kununua mitambo ya dharura badala yake wao wakatufungashia mitambo ya mashinga!..
Sasa nani artist hapa ikiwa huyo msomi mwenyewe anatumia art kufanya maamuzi yanayohitaji elimu yake..Kulikuwa hakuna wakati una viongozi wsomi na wahandisi kama unavyotaka kuliko wakati wa Mkapa lakini ndio wakati Umeme,Maji na vitu vyote vimetupwa nje ya elimu zao..walichofikiria ni UTAJIRI!.. na ktk swala la mitambo ya Dowans kinaendelea hapa ni imani hiyo ya UTAJIRI..imani ambayo wananchi tumechoka nayo! kwa nini hawa wasomi hawaelewi hilo?
So artist can be anyone, msomi, mwanasiasa na hata raia asokuwa na elimu..Ni kipaji kinachotegemea wajinga wangapi wanaingia!

Mkuu asante kwa maelezo yakinifu
 
Watanzania tunafundishwa kuwa wanasiasa. Profession pekee inayoheshimika na inayolipa ni siasa. Ndio maana hata maprofesa wanaacha kaza zao, madaktari, wanajeshi na hata majambazi wanatafuta kuingia kwenye siasa. MIjadala ikiisha ina maana kutakuwa hakuna siasa.
 
Mkuu Mkandara,

Heshima mbele, yaani nilichoeleza ndio exactly unachofanya... post yako imejaa siasa sana, najua wewe umesoma arts... hivyo ni fani yako!

Maswali yote ya msingi uliyonayo ukipeleka TANESCO wanakupa majibu yote bila hata kukupa tarehe...

Kuacha nchi kuongozwa zaidi na siasa... itatumaliza.

Nchi kuongozwa na siasa sisahihi, lakini ukweli ni kwamba CEO's combines both political interest and technical fact to make decisions. Worse enough to public enterprises political interest is given high weight than technical ones. In this case, a serious political opinion in favour of technical fact is sought for better social outcome, and this is the premise where this argument stands in.
 
Hii Kashshe kweli kweli! Usitetereke umekutana na wanasiasa wa humu ndani-wajibu kwa siasa za humu ndani,.

Kwa kweli uelevu wangu hakuna mijadala inayoisha-nafikiri pale kunapokuwa na makubaliano kidogo basi, wadau(wanasiasa) huwa wanaita huwo mjadala hauendelei- vile vile na wale ambao huwa hawakubaliani- huwa wanachoka kutokubaliana na hivyo kuita mjadala umekwisha ama haupo!

Vyanzo vya mijadala? ni hii hapa kama wewe ulivyoanzisha unatafuta nini?:eek:

Una elimu gani ya kuanzisha huu mjadala? Siasa kama sayansi?:D

Hivi wadau ARTS ni sayansi?

Uelevu wangu arts ni ubobeaji wa kiaina, na sayansi uchunguzi wa kimahesabuhesabu au?
 
Anza kwa kumwuliza BFF wako anayesema kila siku hapa kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari halafu anaanza kumpondea "mwandishi" mwingine wa habari mwenye redio ya mtandaoni...

Wakimuelewa Andy Rooney basi kutakuwa hakuna tena tatizo...

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=jLOJP5LUyZc&feature=related]YouTube - Andy Rooney - Food for thought[/ame]

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=tCMR2ZjPJkI&feature=related]YouTube - Andy Rooney - Newspaper[/ame]

Ni mkanganyiko wa mambo, wanasema dhahama, aidha unajua au hujui!!

Mangwini wanaua nchi....:D
 
Kasheshe,

..mada yako imenifanya nikumbuke habari iliyopata kuandikwa kuhusu ziara ya Robert Mc Namara chuo kikuu cha DSM.

..viongozi walimtembeza maeneo mbalimbali ya chuo, lakini walipofika faculty of Law wakamwambia McNamara kwamba Law ndiyo kitivo kianzilishi na fahari ya UDSM.

..baada ya maelezo hayo, Robert McNamara alitoa kauli kwamba, ikiwa kilimo ndiyo uti wa mgongo uchumi wa Tanzania, ingetegemea kitivo cha kilimo kiwe cha kwanza taifa lilipoamua tulipoamua kuanzisha chuo kikuu.

..nadhani taifa letu limejenga mazingira ya kuwakweza wanasiasa kuliko taaluma yoyote ile. inashangaza kwamba wanasiasa wanalipwa mafao mazuri kuliko wataalamu waliobobea ktk fani zao.
 
Watanzania tunafundishwa kuwa wanasiasa. Profession pekee inayoheshimika na inayolipa ni siasa. Ndio maana hata maprofesa wanaacha kaza zao, madaktari, wanajeshi na hata majambazi wanatafuta kuingia kwenye siasa. MIjadala ikiisha ina maana kutakuwa hakuna siasa.

Kwa nini wataalamu wetu hukimbilia kujifanya "victims" na kutafuta visingizio vya kulaumu wanasiasa?

I am sick and tired of this fingerpointing.

Kama wataalamu walishafanya utafiti wao katika hili tangu mwaka 47, kwa nini kama wanasiasa walionekana kulegalega hawakuuambia umma wa Watanzania ukweli?

Kwa nini iwe sisi wakimbizi humu JF ndio tuwe na uzalendo wa kuongea na kubainisha matatizo bila woga, na wataalamu wetu wawe kunguru mwoga?

Kingine ni hicho cha kusema ni kwenye siasa pekee ndipo kuna uponeo.

Tabaka la wasomi wetu ni sawa na wanasiasa wetu wanavyopenda misaada na kuziba viraka. Msimsingize Nyerere na University College kuwa ndio shina lwa Sayansi kuyumba.

Tuna wataalamu kibao katika kila nyanja ya sayansi, anza kilimo, hali yahewa, mifugo, afya, lishe, kemia, fizikia, uhandisi, umeme, kompyuta, mawasiliano na mengine kem kem, lakini badala ya wataalamu hawa kujitutumua na kuwa wabunifu wa kufanya kazi bila kuambiwa na wanasiasa, wanasubiri kila siku wanasiasa waongee au wapewe amri.

Why play victim and inferiority complex mentality?

Same is those in ni Science, fields, Lawyers, Accounts, Economists etc. Every Msomi in Tanzania enjoys to play a victim and later point a finger to a Politician kuwa eti Politician ni tatizo.

No tatizo la kwanza ni wewe mtaalamu ambaye unashindwa kufanya kazi yako kwa umakini na ufanisi!
 
Rev.Kishoka said:
Kwa nini iwe sisi wakimbizi humu JF ndio tuwe na uzalendo wa kuongea na kubainisha matatizo bila woga, na wataalamu wetu wawe kunguru mwoga?

Kishoka,

..lawama zako ni rahisi sana kuzitoa ukizingatia kwamba uko kwenye mtandao huku ukitumia jina la bandia.
 
Kishoka,

..lawama zako ni rahisi sana kuzitoa ukizingatia kwamba uko kwenye mtandao huku ukitumia jina la bandia.

Well iwe lawama au kubaini ufisadi, kama hao wataalamu wote wnajua ni kazi kulipua ngoma, kwa nini wasije basi huku JF au wakatafuta watu watuletee khabri tuzilipue kama lile sakata la ATCL au Benki ya Posta?
 
Tatizo ni UWEKEZAJI mdogo kwenye mashirika yetu ya HUDUMA kama TANESCO, DAWASA,... Na hata hicho kinachowekeza kinatafunwa kwelikweli na Wanasayansi na Watawala.
DAWASA inaongozwa na Mhandisi aliyebobea kwa masuala ya maji. Mwaka 2003 walipewa dola milioni 164 kwa ajili ukarabati wa miundombinu ya maji na majitaka. Waulize sasa wamefikia wapi katika kupunguza kero ya huduma ya maji na majitaka katika jiji letu! Wizi mtupu.
 
Kasheshe hivi hapa tuna wanasayansi nchi hii? Kwani wamefanya kipi hasa? Niambie mtu mmoja aliye na sifa kubwa ya kauvumbuzi katika nchi hii, maana hata vyura tu tumeamua kuwatunzia Marekani maana hakuna mwanasayansi anayeweza kuwatunza hapa Bongo.
Mimi niliamua kuiacha Sayansi sekondari na kujikita katika masomo ya biashara. Nimefanya kazi there after kwa miaka takribani 13 na nikaacha na sasa nafanya biashara. Sioni faida ya sayansi nchi hii maana waliosoma sayansi hawaheshimiki wala hawana maslahi.
Niliosoma nao Sekondari wakiwa na vichwa vizuri katika masomo ya Sayansi they are nothing now. Wanajuta kwa nini waliamua kusoma Sayansi. Wengine waliamua kugeuza muelekeo baadaye na kwenda kusomea uhasibu na uanasheria na wengine kuwa wanasiasa mfano huyu mbunge Esther Kabadi Nyawazwa.
Wale waliojikita katika arts leo ni mamilionea na wana nafasi nzuri katika nchi hii. Sayansi ya nini katika nchi hii? hapa hata ukiwa mvumbuzi no honor.
Wanangu wote nawashawishi kabisa wasisome masomo ya sayansi ingawa baadhi likes them. Kwa nini? kwa sababu hayana prospects mbele katika nchi hii.
Najua utapinga lakini ndio ukweli tena ukweli mtupu!

Rejea dokezo hili kuhusu 'Mpemba Effect' lililotumwa na Msomi wa Kitanzania:

This was a discovery by a Tanzanian student at the former Mkwawa High
School (now MUCE), the results of which were published in Phys. Educ.
1969, 4, pp. 172-5. This work is cited by many researchers. For more
information visit at Mpemba effect - Wikipedia, the free encyclopedia. Below
is a short description of the discovery.

The Mpemba effect is the observation that, in certain specific
circumstances, warmer water freezes faster than colder water. New
Scientist recommends starting the experiment with containers at 35 °C (95
°F) and 5 °C (41 °F) to maximize the effect.[1]

The effect is named for the Tanzanian high-school student Erasto B.
Mpemba. Mpemba first encountered the phenomenon in 1963 in Form 3 of
Magamba Secondary School, Tanzania when freezing hot ice cream mix in
cookery classes and noticing that they froze before cold mixes. After
passing his O-level examinations, he became a student at Mkwawa Secondary
(formerly High) School, Iringa, Tanzania. The headmaster invited Dr. Denis
G. Osborne from the University College in Dar Es Salaam to give a lecture
on physics. After the lecture, Erasto Mpemba asked him the question "If
you take two similar containers with equal volumes of water, one at 35 °C
(95 °F) and the other at 100 °C (212 °F), and put them into a freezer, the
one that started at 100 °C (212 °F) freezes first. Why?" only to be
ridiculed by his classmates and teacher. After initial consternation, Dr.
Osborne confirmed Erasto's finding and they published the results together
in 1969.[2][3] Erasto Mpemba currently works for the African Forestry and
Wildlife Commission.[4]

Osborne observed that the top is warmer than the bottom in a beaker of
water being cooled, the difference being sustained by convection. Blocking
heat transfer from the top with a film of oil drastically slowed cooling.
Also, the effect of dissolved air was accounted for by using boiled water.
The beakers were also insulated from the bottom.
 
Kasheshe,

..mada yako imenifanya nikumbuke habari iliyopata kuandikwa kuhusu ziara ya Robert Mc Namara chuo kikuu cha DSM.

..viongozi walimtembeza maeneo mbalimbali ya chuo, lakini walipofika faculty of Law wakamwambia McNamara kwamba Law ndiyo kitivo kianzilishi na fahari ya UDSM.

..baada ya maelezo hayo, Robert McNamara alitoa kauli kwamba, ikiwa kilimo ndiyo uti wa mgongo uchumi wa Tanzania, ingetegemea kitivo cha kilimo kiwe cha kwanza taifa lilipoamua tulipoamua kuanzisha chuo kikuu.

..nadhani taifa letu limejenga mazingira ya kuwakweza wanasiasa kuliko taaluma yoyote ile. inashangaza kwamba wanasiasa wanalipwa mafao mazuri kuliko wataalamu waliobobea ktk fani zao.

Jokakuu,

I salute you sir!
 
Kwenye bandiko langu hili la 2000:

Naomba niseme kwamba nashukuru kwamba niliweka thread hii, bado imenionyesha kwamba sikukosea na kweli Taifa lina tatizo kubwa la uwiano usikuwa sawa kati ya wataalamu au wahitimu wa sayansi jamii na sayansi ile nyingine.

Ndio maana hata mjadala huu utaona wanasayansi jamii wameuteka...

Nawatakia mafanikio mema... lakini taifa bila kuwa na uwiano mzuri wa wasomi wa nyanja zote litaparanganyika kama ilivyosasa...

All the best.....
 
Rejea dokezo hili kuhusu 'Mpemba Effect' lililotumwa na Msomi wa Kitanzania:

This was a discovery by a Tanzanian student at the former Mkwawa High
School (now MUCE), the results of which were published in Phys. Educ.
1969, 4, pp. 172-5. This work is cited by many researchers. For more
information visit at Mpemba effect - Wikipedia, the free encyclopedia. Below
is a short description of the discovery.

The Mpemba effect is the observation that, in certain specific
circumstances, warmer water freezes faster than colder water. New
Scientist recommends starting the experiment with containers at 35 °C (95
°F) and 5 °C (41 °F) to maximize the effect.[1]

The effect is named for the Tanzanian high-school student Erasto B.
Mpemba. Mpemba first encountered the phenomenon in 1963 in Form 3 of
Magamba Secondary School, Tanzania when freezing hot ice cream mix in
cookery classes and noticing that they froze before cold mixes. After
passing his O-level examinations, he became a student at Mkwawa Secondary
(formerly High) School, Iringa, Tanzania. The headmaster invited Dr. Denis
G. Osborne from the University College in Dar Es Salaam to give a lecture
on physics. After the lecture, Erasto Mpemba asked him the question "If
you take two similar containers with equal volumes of water, one at 35 °C
(95 °F) and the other at 100 °C (212 °F), and put them into a freezer, the
one that started at 100 °C (212 °F) freezes first. Why?" only to be
ridiculed by his classmates and teacher. After initial consternation, Dr.
Osborne confirmed Erasto's finding and they published the results together
in 1969.[2][3] Erasto Mpemba currently works for the African Forestry and
Wildlife Commission.[4]

Osborne observed that the top is warmer than the bottom in a beaker of
water being cooled, the difference being sustained by convection. Blocking
heat transfer from the top with a film of oil drastically slowed cooling.
Also, the effect of dissolved air was accounted for by using boiled water.
The beakers were also insulated from the bottom.

Companero bandiko lako ni zuri sana na ni kitu cha kujivunia. Sasa nenda uangalie huyu Mpemba kama hatakujulikana katika taasisi aliyomo kuwa alivumbua kitu! utashangaa kwamba hana status yoyote pale.
Mshahara na marupu rupu hana, hata usafiri utakuta hana wakati aliyesoma naye O level na akaenda A level Arts si gari tu bali ana hata hekalu.
Mi nakwambia ukweli wacha tu hizi hadithi za wanasayansi hapa Tanzania hamna kitu. May be ukibahatika ukapata kazi Boswana au Ulaya na Marekani hapo uanasayansi wako utaonekana wa maana. Lakini hapa Bongo we acha tu. Wengi wamekuwa frustrated.
 
Kwenye bandiko langu hili la 2000:

Naomba niseme kwamba nashukuru kwamba niliweka thread hii, bado imenionyesha kwamba sikukosea na kweli Taifa lina tatizo kubwa la uwiano usikuwa sawa kati ya wataalamu au wahitimu wa sayansi jamii na sayansi ile nyingine.

Ndio maana hata mjadala huu utaona wanasayansi jamii wameuteka...

Nawatakia mafanikio mema... lakini taifa bila kuwa na uwiano mzuri wa wasomi wa nyanja zote litaparanganyika kama ilivyosasa...

All the best.....

Ukifanya hivyo, utakuwa umekata tamaa Kasheshe, na hakuna itakaye faidika. Swala la msingi, tafuta hao wataalamu wa mitambo watuletee facts my friend. Positions here, are defined following the current political and technical context of which tanzania have been used most of the times. People, like me, I am not sure, which said to stand because i don't know what are the technical facts of the issue. However, my ears lean with the public sentiments at the moment, but yet so open to hear factoids. So, if you bring basic facts, the conversation might take different direction.
 
Taabu ni kuwa hatujapata Raisi Tz aliyechukuwa masomo ya Uhandisi, Sayansi, Udaktari tiba hadi sasa wote wamekuwa ni ngwini tu! Hata mawaziri wakuu!!!

Angalia

1. Nyerere ---MA History!!
2. Mwinyi----BA? Diploma?? Political Science??
3. Mkapa----BA Journalism!!!
4. JK---BA Economics!!!

Na hata angalia Lowasa ..BA Fine Arts??, Pinda... LLB?? Sita..LLB???

Zote hizi ni ngwini tu!

Tuwe na raisi sasa wa sayansi kama raisi yule wa India .ndo tutaanza kuona mapinduzi ya fikra na kupungua kwa Uswahili na Ngwini! Ili kuweka maneno yetu mengi ktk vitendo!

Ni wakati wa kuwapa nafasi Raisi na Viongozi wa Juu Natural Scientists ndo tupime matokeo!
 
Kwa nini wataalamu wetu hukimbilia kujifanya "victims" na kutafuta visingizio vya kulaumu wanasiasa?

I am sick and tired of this fingerpointing.

Kama wataalamu walishafanya utafiti wao katika hili tangu mwaka 47, kwa nini kama wanasiasa walionekana kulegalega hawakuuambia umma wa Watanzania ukweli?

Kwa nini iwe sisi wakimbizi humu JF ndio tuwe na uzalendo wa kuongea na kubainisha matatizo bila woga, na wataalamu wetu wawe kunguru mwoga?

Kingine ni hicho cha kusema ni kwenye siasa pekee ndipo kuna uponeo.

Tabaka la wasomi wetu ni sawa na wanasiasa wetu wanavyopenda misaada na kuziba viraka. Msimsingize Nyerere na University College kuwa ndio shina lwa Sayansi kuyumba.

Tuna wataalamu kibao katika kila nyanja ya sayansi, anza kilimo, hali yahewa, mifugo, afya, lishe, kemia, fizikia, uhandisi, umeme, kompyuta, mawasiliano na mengine kem kem, lakini badala ya wataalamu hawa kujitutumua na kuwa wabunifu wa kufanya kazi bila kuambiwa na wanasiasa, wanasubiri kila siku wanasiasa waongee au wapewe amri.

Why play victim and inferiority complex mentality?

Same is those in ni Science, fields, Lawyers, Accounts, Economists etc. Every Msomi in Tanzania enjoys to play a victim and later point a finger to a Politician kuwa eti Politician ni tatizo.

No tatizo la kwanza ni wewe mtaalamu ambaye unashindwa kufanya kazi yako kwa umakini na ufanisi!

Unayosema ni kweli mkuu. Lakini ukumbuke kuwa Sumaye alisema ukitaka biashara zako zikunyokee uwe mwana CCM, otherwise utaishia kufilisiwa au kuigizwa mikenge ya ajabu. Same is true kwa watu wa taaluma nyingine, Lamwai anajua kilichomkuta, list goes on. Kwa hiyo utaona kuwa wanasiasa wanaplay part kubwa kuwafanya wataalamu na wasomi kutodeliver.
 
Taabu ni kuwa hatujapata Raisi Tz aliyechukuwa masomo ya Uhandisi, Sayansi, Udaktari tiba hadi sasa wote wamekuwa ni ngwini tu! Hata mawaziri wakuu!!!

Angalia

1. Nyerere ---MA History!!
2. Mwinyi----BA? Diploma?? Political Science??
3. Mkapa----BA Journalism!!!
4. JK---BA Economics!!!

Na hata angalia Lowasa ..BA Fine Arts??, Pinda... LLB?? Sita..LLB???

Zote hizi ni ngwini tu!

Tuwe na raisi sasa wa sayansi kama raisi yule wa India .ndo tutaanza kuona mapinduzi ya fikra na kupungua kwa Uswahili na Ngwini! Ili kuweka maneno yetu mengi ktk vitendo!

Ni wakati wa kuwapa nafasi Raisi na Viongozi wa Juu Natural Scientists ndo tupime matokeo!

wacha matani wewe! Gwini wametawala kiuongozi duniani, angalia historia ya marekani kwa mfano kidogo tu! check the link http://www.ipl.org/div/potus . Leading a country is not about academic background, it is about a leader to understand collective individuals which called nation that must have character, vision and attitude to interact with other collectives for its progress.
 
Last edited:
Taabu ni kuwa hatujapata Raisi Tz aliyechukuwa masomo ya Uhandisi, Sayansi, Udaktari tiba hadi sasa wote wamekuwa ni ngwini tu! Hata mawaziri wakuu!!!

Angalia

1. Nyerere ---MA History!!
2. Mwinyi----BA? Diploma?? Political Science??
3. Mkapa----BA Journalism!!!
4. JK---BA Economics!!!

Na hata angalia Lowasa ..BA Fine Arts??, Pinda... LLB?? Sita..LLB???

Zote hizi ni ngwini tu!

Tuwe na raisi sasa wa sayansi kama raisi yule wa India .ndo tutaanza kuona mapinduzi ya fikra na kupungua kwa Uswahili na Ngwini! Ili kuweka maneno yetu mengi ktk vitendo!

Ni wakati wa kuwapa nafasi Raisi na Viongozi wa Juu Natural Scientists ndo tupime matokeo!

Bwahahaha nimecheka kweli yaani...LOL!! Sasa kama Lowassa na digrii yake ya kutengeneza "vinyago" na mambo ya umeme wapi na wapi? Mangwini jamani, waacheni wataalamu wafanye kazi zao......mweh!
 
Back
Top Bottom