Nini chanzo cha mijadala mingi isiyoisha? Je ni mfumo wetu wa Elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini chanzo cha mijadala mingi isiyoisha? Je ni mfumo wetu wa Elimu?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Kasheshe, Mar 8, 2009.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wanabodi,

  Naanza kushitukia kwamba kuna mambo yamekuwa yakijadiliwa muda mrefu na wakati mwingine hata hayana tija, wakati mwingine yaki-engage mahakama, serikali na bunge!

  Je hii haiwezeki kuwa ni mojawapo za athari ya kusomesha wataalamu wa sayansi(arts) jamii wengi!

  Je suala la TANESCO kuonekana la kisiasa ndio dalili za mfumo huo wa elimu kuwa na waatalaamu wa arts zaidi kuliko wahandisi?

  Ninachalea kusema haya kwa kuwa hoja ya TANESCO inaonekana kutosikilizwa kabisa. concern yao ya kuwepo umeme usiotosha mahitaji na kwamba serikali imekuwa ikijivutavuta kuwekeza haionekani kuonekana machoni mwa wanasiasa... nini tatizo?
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu ndio maana kwenye ile hoja ya ip attacking jf nilimuuliza mtu can we be profesional nilichosema pale nilimaanisha kama vitu ni profesional waache profesional wanaojua waongee na wawa shauri kutokana na uelewa wao na mambo hayo --
   
 3. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kasheshe salam,
  Mbali na elimu ya fani hii au ile kuna kitu kingine muhimu ambacho viongozi wengi wana upungufu nacho; UWEZO WA KUZALIWA NAO katika kutoa uamuzi na kutekeleza uliyoamua. hayo mawili yanakwenda pamoja na kwa maoni yangu, utapata mwongozo wa hayo kutoka Shule/Elimu lakini atakuwa bora yule aliezaliwa na kuondokea kuwa na POWER hiyo toka udogo wake naamini kuna viongzi wengi Duniani waliothibitisha hivyo akiwemo Abaham Lincon (USA) na Mzee Jomo Kenyata(kenya).nk.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kasheshe,
  Mkuu ktk hili nadhani unajaribu ku spin the issue kwa sababu tunachozungumza hapa ni hili swala la mitambo ya Dowans..
  Kuna issue mbili hapa ambazo unajaribu kuziunganisha Short na Long term strategies..
  Kwanza hakuna mwananchi anayepinga umuhimu wa Umeme na kwa nini serikali yetu imeshindwa kutekeleza long term plan ya kuzalisha umeme..Hilo halina ubishi wala mjadala iwe kwa wanasiasa, wasomi au wananchi kabuntas kama sisi.. mahitaji ya UMEME hayana elimu ya art wala Uhandisi isipokuwa ni chombo gani kinahitajika..tatizo ipo ktk utekelezaji wa short term plan ambayo tayari imekwisha fanyiwa kazi na hao hao wasomi wahandisi unaowazungumza.. wametumia art kutuzuga wananchi wote. sasa sijui walisomea art au Uhandisi.

  Mkuu wangu kinachogomba hapa labda nikiweke sawa.. ni Hivi kama sisi tumekwenda kwa daktari na ametuandikia dawa ya maleria iwe Chloroquine, hakuna anayepinga maamuzi hayo, isipokuwa tunachopinga ni maamuzi ya mtu alioyekwenda dukani kununua dawa hiyo..Kwanza kanunua dawa toka kwa mlanguzi feki - made in India kwa gharama ambayo ni kubwa..Kinachogomba zaidi ni madai yake yanayolenga zaidi sababu za maradhi yetu na somo zito kuhusiana na Maleria wakati sisi tunachouliza ni kidogo sana why.. kinahusu hiyo dawa sio maradhi yetu..hatupati jibu!

  Nachoomba hawa wahandisi unaotaka kuwasifia watueleze kwa undani kuhusu hii mitambo ya Dowans na sio kiza kinachotuandama, hilo tunafahamu toka mwanzo na ndio maana serikali iliwapa go ahead Tanesco kununua mitambo ya dharura badala yake wao wakatufungashia mitambo ya mashinga!..
  Sasa nani artist hapa ikiwa huyo msomi mwenyewe anatumia art kufanya maamuzi yanayohitaji elimu yake..Kulikuwa hakuna wakati una viongozi wsomi na wahandisi kama unavyotaka kuliko wakati wa Mkapa lakini ndio wakati Umeme,Maji na vitu vyote vimetupwa nje ya elimu zao..walichofikiria ni UTAJIRI!.. na ktk swala la mitambo ya Dowans kinaendelea hapa ni imani hiyo ya UTAJIRI..imani ambayo wananchi tumechoka nayo! kwa nini hawa wasomi hawaelewi hilo?
  So artist can be anyone, msomi, mwanasiasa na hata raia asokuwa na elimu..Ni kipaji kinachotegemea wajinga wangapi wanaingia!
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mkandara,

  Heshima mbele, yaani nilichoeleza ndio exactly unachofanya... post yako imejaa siasa sana, najua wewe umesoma arts... hivyo ni fani yako!

  Maswali yote ya msingi uliyonayo ukipeleka TANESCO wanakupa majibu yote bila hata kukupa tarehe...

  Kuacha nchi kuongozwa zaidi na siasa... itatumaliza.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Mar 8, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha short term wala long term strategies, issue ni kuwa mpaka sasa tumeshindw kuonyesha uwezo wetu si kwa viongozi wala wahandisi!

  Kama alivyosema mtoa maada kuna tatizo pengine kwenye mifumo ya elimu, elimu means to solve problems, not bla bla.

  Mpaka leo sijajua tangu enzi za Nyerere kwa nini tuna tatizo hili?? LABDA MSIO JUA, WATAALAMU WETU WA UMEME WENGI NI WALE WENYE UWEZO MAALUMU/VIPAJI MAALUMU. WENGI WAMEMALIZA ILBORU, KIBAHA, MZUMBE NA TABORA BOYS! HAWA WENGI HUSOMA ELECTRICAL ENGINEERING!

  LAZIMA KUNA TATIZO SEHEMU!!!!!!!!!!lazima
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kasheshe,
  Mkuu wangu acha matusi, na wewe umesomea kitu gani! Kama hao Tanesco wangekuwa wamesomea Uhandisi basi wasingemleta huyo mzungu kutoka ng'ambo kuitazama hiyo mitambo..walishindwa kipi ambacho hakikuwa ktk elimu yao au ndio mzungu kasema!
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba jamii inawasikiliza wanasiasa sana wana-bla bla bla... labda nikuulize swali...

  Tangu sakata hili lianze,,, ni kina nani wame-be-interviewed.... ni wanasiasa tu...

  Hakuna hata interview moja iliyofanywa kwa ERB etc... au kwa mhandisi wowote...

  Nakuambia nyererea alianza kukosea pale University of East Africa, sisi badala ya kuanza na Wahandisi na Madakrai sisi tulianza na wanasiasa... angalia enrolment yetu... arts ni asilimia kubwa sana...

  Angalia wanafunzi wanavyofeli hesabu... Nakubwambia hilo ndio Tatizo... jamii inawasikiliza wanasiasa, wana-arts sana kuliko wahandisi, wahasibu... etc...
   
 9. O

  Ogah JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tha ball is inyour court....fanya hiyo research halafu uje na findings......

  This is Jamii Forums....soma madhumuni yake na kwa nini ipo hivi ilivyo....
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ......umemshtukia eeh......
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,385
  Trophy Points: 280
  Kasheshe.. nitaandika hapa kwa kifupi:

  Kutenganisha siasa na maisha ya kawaida haiwezekani. Siasa encompass everything and exclude nothing. Kujaribu kuondoa siasa kwenye masuala yoyote yanayohusu jamii ya watu ambapo muhusika ni zaidi ya mtu mmoja haiwezekani. Hivyo, iwe katika taaluma mbalimbali, fani au mtazamo wa kimaisha siasa haiepukiki.

  Tanesco kama taasisi ya kiweledi ingeweza kufanya mambo itakavyo. Hata hivyo sera, mwelekeo wa maono na ufadhili wa kifedha wa Tanesco unategemea maamuzi ya kisiasa. Tanesco wanaweza kuwa na hoja nzuri sana na hoja ambazo unazisema wengine tulizisema miaka mitatu sasa. Hakuna lililo geni katika hoja za Tanesco. Bahati mbaya Tanesco wameshindwa kuwashawishi wanasiasa.

  So, wanasiasa hawawezi kuepukika, maamuzi ya kisiasa hayawezi kuepukika. Haiwezekini Tanesco wasema "tunahitaji bilioni 60 kununua mitambo ya umeme" halafu wanasiasa waseme tu "ok here is 60 billion tsh!" huo utakuwa ni wazimu.

  Gharama kubwa tuliyoilipa hadi sasa ni mambo kama hayo kwamba watu ambao ni weledi wameachwa kuchukua maamuzi yao wao wenyewe huku wanasiasa wakifuata nyuma kuyahalalisha. TUmeona Benki Kuu, tumeyaona kwenye wizara mbalimbali, wakala na idara. Matokeo yake professionals wengi ndiyo wamekuwa kiini cha ufisadi nchini! Ni wao ambao wamekuwa wahasibu waliochota mabilioni au wataalamu walioandika miradi ya kifisadi. Ni wao wamegeana mabilioni ya fedha za per diem katika warsha na semina zao za "kitaalamu". KUwachia wafanye wapendavyo ni kujitakia matatizo ambayo tayari tunayo.

  HIvyo wanasiasa sasa wanachukua nafasi yao sahihi, nayo ni kusimamia serikali na by extension wale wote wanaohusiaana na serikali. Maprofessional wasitarajie tena kupewa a blank check ati kwa vile wao ni "wataalamu". Tukifanya hivyo (kuwaachia tu) basi itakuwa ni "wizi mtupu!".

  Tanesco wameshindwa kuangalia political ramification ya maamuzi yao na matokeo yake wanalipa. Kama Dr. Idris hajasikilizwa muda wote aliokuwa madarakani hadi miradi mingine imedoda (kama alivyosema) alitakiwa kujiuzulu muda mrefu uliopita.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ogah!
  siku nyingi nilishamshitukia, unajua tena wapambe wengi...nchi haiongozwi kwa elimu bali wale wanaofikiria wana elimu.
  Miezi michache iliyopita kuna mshikaji wangu kanunua gari kwa dollar 500 akalifanyia ukarabati likapita both emission test na sefty kwa gaharama ya kitu kama 800 in total..
  Sasa jamaa kaingia wazimu ati anataka kuliuza gari kwa dollar 3,000 nikamwambia aache wazimu atumie gari lake hadi litakapo kufa maanake hakuna mjinga atakaye nunua gari hilo kwa kiasi hicho.
  well I was wrong, kuna msomi mjinga aliyeuvaa mkenge akalinunua, sasa matatizo yalipoanza ananifuata mimi nimwambie mshikaji wangu anakaa wapi! ati alimbambika gari bovu.. damn,
  Nikamwambia kwani ile ownership card haina address?...
  Ikawa mimi naleta siasa, msomi kanuna ndio haya ya Kasheshe!
   
 13. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nchi daima itaongozwa na SIASA wakati UTAALAMU unahitajika katika kupanga na kutekeleza mikakati/sera za kuendesha nchi. Suala ni aina gani ya siasa. Na hii ni changamoto yetu sote kuredifine aina ya siasa tunayopaswa kuitumia katika kuongoza nchi. Ni wazi hili ni zoezi gumu lenye kuhitaji ujasiri mkubwa kwani wengi tunapenda kufanya mambo ikiwemo siasa kwa kutumia uzoefu kwakuwa tunauhakika na matokeo. watanzania kwa ujumla ni wahafidhina wasiopenda mawazo na mitindo mipya hivyo inahitaji wanasiasa wali tayari kupata kurisk mafanikio yao binafsi kuweza kukabiliana na athari za kukiuka utamaduni ulio zoeleka wa siasa hohehahe kama ambavyo umegubika nchi yetu.

  Kuhusu mijadala mingi isiyoisha hiyo ni dalili ya kukua kidemokrasia. Ni alama muhimu ya kujengeka kwa jamii inayoanza kutambua umuhimu wa kuwa na tofauti za kimitazamo. Kinachohitajika ni kujenga mifumo muhimu ya kiasasi ambayo itaweza kutumia utamaduni huu tofauti za kimitazamo kwa umakini na kusaidia katika kujenga taifa na kupunguza uwezekano wa tofauti hizo kuwa chachu ya matatizo.

  omarilyas
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Unatuhumu kuwa wengi wetu post zetu imejaa siasa isipokuwa zako wewe mtaalamu - lakini kama majibu uliyotoa kwa Ndugu Mwanzange is anything to go by, wewe ni mtu hatari na moja kwa moja chanzo cha mijadala isiyokwisha.

  Majibu yako:-

  Huyu ni Mkapa aliyeanzisha biashara akiwa Ikulu, akajiuzia Kiwira !! Hapa tunapata sababu kubwa ya kuendeleza mijadala mpaka pale mafisadi na makuwadi wao watuelewe kuwa hatuwapi hata hiyo nafasi ya kufaidi mali walizotuibia kwa amani. Vitendo vyao haviwezi kuhalalishwa asilani kwa sababu nyepesi unazotoa, hatuwezi kumsifia mwizi wetu na kumwona kama mkombozi.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kasheshe hivi hapa tuna wanasayansi nchi hii? Kwani wamefanya kipi hasa? Niambie mtu mmoja aliye na sifa kubwa ya kauvumbuzi katika nchi hii, maana hata vyura tu tumeamua kuwatunzia Marekani maana hakuna mwanasayansi anayeweza kuwatunza hapa Bongo.
  Mimi niliamua kuiacha Sayansi sekondari na kujikita katika masomo ya biashara. Nimefanya kazi there after kwa miaka takribani 13 na nikaacha na sasa nafanya biashara. Sioni faida ya sayansi nchi hii maana waliosoma sayansi hawaheshimiki wala hawana maslahi.
  Niliosoma nao Sekondari wakiwa na vichwa vizuri katika masomo ya Sayansi they are nothing now. Wanajuta kwa nini waliamua kusoma Sayansi. Wengine waliamua kugeuza muelekeo baadaye na kwenda kusomea uhasibu na uanasheria na wengine kuwa wanasiasa mfano huyu mbunge Esther Kabadi Nyawazwa.
  Wale waliojikita katika arts leo ni mamilionea na wana nafasi nzuri katika nchi hii. Sayansi ya nini katika nchi hii? hapa hata ukiwa mvumbuzi no honor.
  Wanangu wote nawashawishi kabisa wasisome masomo ya sayansi ingawa baadhi likes them. Kwa nini? kwa sababu hayana prospects mbele katika nchi hii.
  Najua utapinga lakini ndio ukweli tena ukweli mtupu!
   
 16. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Kwanza umesema hakuna wanasayansi, then unafuatia kusema wasayansi hawaheshimiki? Upi ni ukweli katika hayo mawili?
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Mar 9, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Anza kwa kumwuliza BFF wako anayesema kila siku hapa kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari halafu anaanza kumpondea "mwandishi" mwingine wa habari mwenye redio ya mtandaoni...
   
 18. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Una maana gani ?
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,385
  Trophy Points: 280
  halafu kuomba radhi au kusahihisha hawezi... mgumu utadhani nundu.
   
 20. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Let me add some pilipili and chumvi here. Why did Tanesco had to hire a foreigner to evaluate the Dowans turbines? Ni uhaba gani au ufupi wa upeo ambao watalamu wahandisi wetu wamekosa kuweza kung'amua tangu mapema kuwa mitambo hiyo ni bomu? Je ilipoletwa nchini kwa mara ya kwanza, kwa nini Tanesco haikupeleka timu ya wataalamu kuifanyia utafiti ili ijue kama mitambo hiyo itaweza kuhimili kishindo cha kuzalisha umeme?

  Sometimes we rush to think it is about experticse in sense of education qulification while what e need is simply someone who is exposed to think outside the box.

  Lets focus on this issue of scientist being ignored a litle further. Why does TBS fail t sanction majority of bogus products locally produced or imported while majority of people working for TBS are scientist?

  Je huko nako wanaingiliwa wakiwa maabara na Mangwini kama mimi?
   
Loading...