Nini chanzo cha madereva wengi wanaoendesha magari kukosa uungwana pale tukio la ajali linapohusisha magari yao?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,557
46,104
Mara kadhaa ajali nilizowahi kushuhudia madereva wa vyombo husika vilivyohusika na ajali walikuwa ni watu walio katika hali ya taharuki, hamaki, wanafoka, wanatukana, wanapayuka na mambo mengine ya hovyo kama hiyo.

Hali hii ya taharuki hutokea hata pale dereva husika ndio chanzo dhahiri cha ajali yenyewe, hali hii pia hutokea hata kama ajali yenyewe ni ndogo sana na watu wangeweza kuzungumza kwa uungwana wakaelewana.

Hii hali ya kukosa uungwana kwa madereva wanapokuwa barabarani huchangiwa na nini?
 
Back
Top Bottom