Nini chakufanya mara umfumaniapo mpenzio? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini chakufanya mara umfumaniapo mpenzio?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pape, Nov 15, 2009.

 1. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nini chakufanya mara umfumaniapo mpenzio? Je, ni kuachana nae? Kumsamehe na kuendelea nae?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  inategemeana sana...

  hili swali lina majibu marefu sana.

  kwa mfano mpenzi wako katoka nje kwa sababu gani???
  kipato????
  mligombana so analipiza????
  amekuchoka??
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  soma haya yafuatayo kabla ya kutoa uamuzi wako wa busara
  Kuponya Maumivu ya Kuachana (1)  [​IMG]Kawaida mahusiano yoyote ya mapenzi yanapofika kwenye mzozo mkali (battlefields) huwa na matukio matatu tu.
  Kwanza mmoja huamua kuondoka zake na kuanza mbele au pili wote au mmoja huamua kuendelea kuishi katika mahusiano ambayo hata hayaridhishi/bora liende au tatu wote au mmoja huamua kuanza kupenda upya katika hali zote kuhakikisha mahusiano yanarudi kwenye mstari.

  Hata hivyo inakuwaje pale mmoja anaamua kuanza mbele na kumuacha mwenzake kwenye mataa?
  Mara nyingi mahusiano yanapokatika iwe uchumba au iwe ndoa au iwe urafiki a kawaida unaweza kujikuta umechanganyikiwa bila kujali ni wewe uliyeamua kumuacha mwenzako au wewe uliyeachwa (The Dumper and The Dumped).

  Kujiamini hurudi ground zero, maumivu ni makali, unajiona ni failure na kikubwa zaidi maisha yanatakiwa kwenda hata baada ya kumpoteza Yule ulikuwa unampenda.
  Bahati mbaya ni kwamba si wote wenye uwezo na nguvu za kujikusanya na kuendelea na maisha kama kawaida kwani wengine hudhoofishwa na kufikia mahali wanaona maisha hayana maana tena.

  Kila mahusiano lazima yatakufikisha mahali ambapo utajifunza na kukua haijalishi yanaendelea au yamefeli. Hata hivyo mahusiano yanayoshindwa hufundisha zaidi na hutoa uzoefu mkubwa kwani mafanikio huja si kwa kurudia makosa yale tumefanya au kuchukulia vitu for granted bali kuepuka yale tulifeli mara ya kwanza.

  Nimewahi sikia mtu mmoja muhimu sana akiongea maneno haya:
  "Nisingeweza kufikia mafanikio yote haya kama si kuwa na mtazamo mpya na kuongeza juhudi kujenga taaluma yangu baada ya kuachwa na mchumba wangu wa mwanzo na hatimaye kumpata mume bora niliyenaye sasa"

  Inaonesha ilikuwa muhimu kwake uchumba kuvunjika ili akaze kamba kuendeleza taaluma yake na hatimaye akapata liubavu lake; huko si kukaa na kuhuzunika na kujiambia kwamba "I am finished
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  Kwa nini maumivu ya talaka au kuachwa na mpenzi huwa machungu zaidi ya kifo?
  Kawaida inapotokea kifo jamii nzima huhusika kwa kuwa ni suala la jamii nzima yaani msiba, watu wote wanakuja kulia na wewe, kuimba na wewe, kukuliwaza na zaidi hata kutoa michango mbalimbali kuhakikisha unakuwa na maisha.
  Unapoachana na mpenzi wako au kupewa talaka hakuna mtu wa kuwa na wewe ni wewe peke yako (no shoulder to cry).
  Hakuna mkusanyiko wa jadi, dini, jamii, tamaduni, marafiki au mtu wa kuja kukutia moyo na kuombeleza kuachwa bali wewe.
  Unapoachana na mpenzi wako ni shida yako mwenyewe (lonely hell)

  Unapoachwa na mpenzi au kupewa talaka hofu ya future huanza kukuwinda na unaanza kujiuloiza maswali kama vile nani anakuwa responsible kwa majukumu mbalimbali, nani atatunza watoto nani atakupa support ya kifedha.

  Pia unapoachwa na mpenzi au talaka ukienda mtaani siku moja utakutana na yule alikuacha au achana naye na kama una hasira naye hali huwa mbaya zaidi ila kama ni kifo hutaonana naye.
  Unapoachwa hisia zako hujigawa pande mbili ile inayosema unaweza kuwa na mahusiano mapya na ile inasema ukiwa na mahusiano mapya utaishia kuachwa kama mwanzo​
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  Kuachwa (na mpenzi) ni tukio gumu na zito na huja na mabadiliko tofauti na kumpa mtu uzoefu wa aina yake, ni ngumu na inaumiza sana, lakini watu hujifunza kukua, hupata mitazamo mipya kimaisha, uelewa mpya, na uchujaji wa mambo upya na matumaini mapya ingawa huwa ngumu sana kuona mbali au mbele baada ya kukutana na hii patashika.

  Hakuna anayependa kuachwa, kwani ukiachwa unajiona umefeli na tumefundishwa katika maisha jambo la msingi ni kuwa washindi si kufeli au kuwa failrues. (winners not losers).

  Kushindwa ni kubaya na huumiza, huandamana na ncha kali kama za kiwembe ambazo huweza kuchana nerves hadi kutoa maumivu makali sana yasiyovumilika.
  Haijalishi umeshindwa kidogo au kiasi kikubwa vyote huumiza.

  Inaumiza sana kwa sababu hatujafundishwa kutegemea kushindwa na pia hatujafundishwa tukishindwa tufanye namna gani (how to handle).
  Mtu yeyote anapokutana na kushindwa wengine huanza kumlaumu na kumtamkia maneno kama vile:-
  "Angekuwa mke mwema wala asingeachwa na mume wake"
  "Wazazi wake wangekuwa makini mtoto wao asingejiunga na wavuta bangi"
  "Asingekuwa anajifanya mjuaji asingefukuzwa kazi"
  "Wangekuwa wanaishi Kikristo haya yote (mabaya) yasingetokea"
  Je, umewahi kuwa na mawazo ya namna hiyo kwa wanaoshindwa?
  Naamini umewahi na ndivyo binadamu tulivyo.
  Biblia imeeleza wazi pia kwani siku moja wanafunzi wa Yesu walikutana na mtu kipofu na kwa kuwa kipofu waliamini yule kipofu au wazazi wake au ndugu zake walifanya dhambi hata hivyo majibu ya Yesu yalikuwa tofauti.

  Yohana 9:1-3
  Yesu alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza,
  "Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?''
  Yesu akawajibu,
  "Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake.

  Mungu anachukia wanandoa kuachana, anachukia talaka na talaka si mpango wa Mungu bali mwanadamu, hata hivyo Mungu anawapenda walioachwa na waliacha, Mungu anawapenda walipewa talaka na bado ana mpango na maisha yao ingawa sisi binadamu huweza kuwakwepa walioachwa na kutalikiwa na kuwaona ni watu wenye hitilafu katika maisha.

  Kumbuka ni Yesu Peke yake ndiye anajua machungu uliyopitia au unayopitia hata kama umeachwa leo au karibuni au zamani na bado Mungu anampango na maisha yako.

  Yesu ndiye rafiki wa kweli anajua kuachwa na kukanwa kama vile Petro alivyomkataa kwamba hamjui.

  Tumaini bado lipo na maisha bado yapo hata baada ya kuachwa.

  Usikate tamaa.
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  Kuvunjika moyo, kukatishwa tamaa, upweke, nk ni maneno yanayoelezea feelings za uzoefu ambao binadamu hupitia pale mahusiano yanapovunjika iwe urafiki wa kawaida, uchumba au ndoa.

  Wakati mwingine aliyeachwa huamua hata kutishia kwamba atajinyonga wasiporudiana au tishia kufanya kitu chochote au kujitoa hata kuhonga chochote anachoweza na bado juhudi zote huzaa nothing na hali kuwa mbaya zaidi.

  Kuachwa hasa uchumba huumiza sana wakati mwingine kwa sababu aliyekuacha (dump, abandon) anaweza kumuoa/olewa rafiki yako au ndugu yako au mtu kwa karibu na wewe unayemfahamu na zaidi unakutana nao mitaani na inaawezekana wewe ni mzuri zaidi yake.

  Kila survivor wa kuvunjika kwa mahusiano huendelea kuwindwa na mabaki ya hofu na mashaka ya mahusiano yatakayofuata.

  Wapo ambao baada ya mahusiano kuvunjika huanza mahusiano mapya ambayo huvunja moyo tena kama mara ya kwanza na hawakati tamaa na hujifunza kwa kuondoa hofu na mashaka na kujenga trust upya na kuendelea kufurahia mahusiano mapya tena.

  Wengine huruhusu vidonda (emotional) kuendelea kuwatawala na wanakuja wamejifungia (locked) kutoruhusu kupenda na kupendwa upya.

  Jambo la msingi ni kwamba maumivu ya kupotelewa au kuachwa na mtu unayempenda ni moja ya maumivu makali sana na baada ya kuachwa kupenda tena huwa ni moja na hofu kubwa sana mtu anapitia katika maisha yake kwani wengi hujikutana wanakutana na walewale.

  Unapompenda mtu kwa moyo wako wote na hisia zako zote na kwa mapenzi yako yote, mahusiano yanapovunjika maisha hubadilika na kuathiriwa kiasi cha kusimama ghafla.
  Kuna usemi kwamba
  "Usually the first love lost is the most painful"

  Jambo linalostua zaidi ni kwamba wale wanauumia zaidi ni mwanaume au mwanamke ambaye hata baada ya mahusiano kuvunjika (mfano uchumba) bado hung'ang'ania au kuendelea kutaka warudiane kwa kuwa walikuwa deep na attached kwenye hilo penzi, hujisikia bila huyo mtu hupo desperate na hana control.

  Na wakati mwingine hufikiria mbali zaidi kwa kuamua kufanya kitu chochote kuhakikisha wanarudiana kibaya zaidi partners wao huwa walishafanya maamuzi na hawawezi kurudi tena.

  Pia unapoachwa na mpenzi feelings zako hujigawa pande mbili, upande wa kwanza unakwambia unaweza kuanza mahusiano mapya sasa na upande mwingine unakwambia usifanye na ukifanya au jiingiza kwenye kupenda tena utaishia kuumizwa kama mwanzo.

  Pia kuacha au kuachwa hujenga kujisia hatia (guilt) bila kujalisha wewe ni uliyeachwa au uliyeacha, rejected au rejecting, dumped au dumper wote huwa na hisia za kujiona ni failure.
  Kujisikia hatia hujenga hali ya kujisikia kutojiamini na kutojiamini huzaa hofu ambayo huendelea kukuwinda kila mara unapokumbuka mahusiano yalivyovunjika.
  Hiyo hofu huingia akilini na kugonga kama nyundo kukumbushia machungu na makali ya kuachwa hadi unafikia hali unajikuta kuchanganyikiwa kama si kupaniki.
  Vilevile hofu hii huweza kupooza hatua yoyote unayotaka kuchukua ili kuanza mahusiano mapya na unajikuta huwezi kuwekeza tena kwenye kupenda na kupendwa upya, unakuwa mwoga kupenda upya na unaogopa pia kukaa mwenyewe bila mtu wa kukupenda, ni kizunguzungu tu.

  Jambo la kujiuliza kwa nini unajisikia hatia je, ni kweli ni wewe uliyesababisha mahusiano kuvunjika au ni illusions tu?
  Je, ni kweli ulivunja kiapo (vow/covenant) ulichoahidiana na mpenzi wako?
  Je, ni kweli hukuwa responsible kwenye mahusiano hadi hajavunjika?
  Kama si kweli basi unajichukulia lawama ambazo hustahili.

  Je, ni hatua ngapi mtu aliyeachwa anaweza kutumia ili kuponya maumivu yake na kurudi kwenye maisha ya kawaida​
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  [​IMG]HATUA YA NNE NI KUSEMA KWA HERI
  Hii ni hatua ngumu sana kukutana nayo kwani ni hatua ambayo unakubali na kumwambia kwa heri Yule amekuacha.
  Hapa ni hatua ambayo unakubali kwamba ni kweli mahusiano yamefika mwisho.
  Hapa una admit kwamba huyu mtu hayupo tena katika maisha yangu na sasa natakiwa kuendelea mwenyewe.

  Hata hivyo wapo ambao hujikuta wanakwamba wakifika hapa kwani wakati mwingine huamini sasa kwa heri na baada ya wiki mbili anarudi tena kuwaza kama inawezekana wakarudiana kitu ambacho hata aliyemuacha hana mpango kabisa.

  Kumbuka ukitaka kuwa mtu huru na uweze kuendelea mbele jambo la msingi katika hatu hii ni wewe KUMSAMEHE.
  Andika kwenye karatasi yale unaamini mpenzi wako amekukosea na yasome na kuomba Mugu akusamehe na yeye pia umsamehe.
  Bila kusaheme inakuwa ni sababu muhimu sana ya kuzuia Baraka zako kwwa mahusiano yajayo na mahusiano yako wewe na Mungu.
  Tunaweza kusaheme kwa sababu Mungu anatusamehe.

  Inawezekana wakati upon a mpenzi wako kulikuwa na maeneo muhimu ambayo mlikuwa mnaenda pamoja inaweza kuwa ni kanisa, hotel, viwanja na sehemu za vacation na tangu mmeachana ukizikumbuka hizo sehemu unajisikia uchungu sana.
  Kama unapotembelea hizo sehemu unajisikia hofu na uchungu kitu cha msingi kufanya ni wewe kwenda na rafiki zako/yako na ziombee kwa Jina la Yesu.
  Mungu atakupa amani na utajisikia raha kuwepo hizo sehemu tena.

  HATUA YA TANO NA SITA KUJIJENGA NA MATUMAINI MAPYA
  Kwenye hatua hizi mbili sasa unaweza kuiongelea future huku ukiwa na matumaini mapya.
  Hata hivyo tunatakiwa kukumbuka kwamba kukiwa na tukio la kuachana huwa kunakuwa na matokeo ya aina tatu kwa aliyeathirika.

  Kwanza unaweza kubadilika na kuwa maisha mazuri zaidi, pia unaweza kubadilika na kuwa na maisha ya ovyo kabisa au tatu unaweza kubadilika na kurudi katika maisha yako kama kawaida.

  Mara nyingi huwa ngumu sana kuwa na mabadiliko ya kuwa na maisha mazuri kama umekataliwa, umeachwa, upo dumped au rejected hata hivyo ukisimama vizuri na kumwangalia Mungu na kuitopoteza focus ya kuwa positive katika mtazamo wako unaweza kuwa na maisha bora tena na yenye Baraka
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  mpendwa ukiona hayo yote unayaweza kuvumilia good;else

  CHAPALAPA FASTA KWABLA UJAJERUHIWA..........,
   
 9. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  "chapalapa" ndio nini???? otherwise asante mkuuu kwa post hizo hapo juuuu!
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hata tukikushauri, yote hayo yapo ndani ya uwezo wako kuamua. Ushauri wangu, fikiria kwanza kabla ya kuachana nae, kumsamehe au kendelea nae..
   
 11. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  asanteni wakuu
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,744
  Trophy Points: 280
  Wazo la mwisho usichape la fasta kaa chini fikiria omba ushauri,,linganishe na wa wakwako chuja toa gawanya....=kila la kheri
   
Loading...