Nini CHADEMA, CCM na CUF wafanye kulinda kura zao Kinondoni, Siha na pengine kote!!!

kimpango

JF-Expert Member
Apr 24, 2011
602
1,000
Kumekuwa na malalamiko ya vyama vya siasa kuhusu kuchezewa faulo kwenye chaguzi mbali mbali ikiwemo mawakala kukamatwa, siku ya uchaguzi ,kutokupewa fomu za kiapo, na kuhongwa ili kupindisha matokeo.

Ninaamini vyama hivi vina wanachama na wapenzi waaminifu ..pamoja na kuweka mawakala watiifu vinaweza kupanga watu wa kutosha wenye vigezo vya kupiga kura kuenda kupiga kura kwa kupokokezana yaani kuingia mmoja moja mpaka muda a kufunga kituo yaani wasiende wote mara moja asubuhi au mchana.

Mfano ccm ina wana chama labda waaminifu wa wazi 5000 tu kinononi inaweza kukubaliana kwenda kupiga kura kwa muda flani tofauti ili kuzuia manover.

Pia kuwa na CAMERA za siri zinazoweza kurekodi watu wote wanaoingia kwenye vituo vyote either kwa kuwavalisha mawakala au namna yoyote ili kuweza kuwa na ushahidi wa idadi ya watu walioingia kupiga kura siku hiyo kuzuia kura za maruhani.

Pia ulinza wa kura ni muhimu na ikiwezekana CCM iwaalike hata waandishi wa habari wa nje vyombo kama bbc, cnn ,dw ,aljazeera kuangazia yote kwenye uchaguzi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom