Nini cha kwanza kabisa kwa binadamu, humsukuma anapoamua kuoa ama kuolewa?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,244
Kulingana na tamaduni mbalimbali za mwanadamu, kumeibuka tathimini isiyo rasmi inayoumiza vichwa vya wanazuoni wa kimahusiano hasa dhana ya kuoa ama kuolewa!

Hivi binadamu anapoamua kuoa/kuolewa, cha kwanza kabisa anaoa/kuolewa kwaajili ya nini?"
 
Mie ukweli nilichoka na sheria za nyumbani mpaka madukani lazima upelekwe ukichelewa kurudi utakiona kilichomtoa kuku
manyoya,nilikua nafanya kazi lakini story ikawa hiyo hiyo nikaona bora niolewe yaishe tutapenda huko huko mbele ya safari
lakini alhamdulilah namshukuru mungu mpaka hapa tulipofikia...
 
.......Ndugu yangu kwa zama hizi zetu hata mtoto wa darasa la pili anajua mtu anaoa au kuolewa kwa lengo gani,hayo mengine hua yanafuatia tu.
 
Umeshasema kuna tamaduni mbalimbali na tathmini isiyo rasmi.

Uta assume vipi kwamba kuna kitu kimoja, cha kwanza kabisa? Kwanza ndoa yenyewe ni dhana pana sana na hata hujai define vizuri unaiongelea kwa wigo upi hapa.

Kwa mfano, unapoongelea ndoa unaongelea ndoa za kidini? Kisheria? Kitamaduni? Common law marriage ni kati ya ndoa unazoongelea ama la?

Mtu akikwambia hakuna kitu kimoja kinachosukuma watu kuoa. Wengine wanaoa kufuata utamaduni.Wengine wanataka kuheshimika, wengine wanataka kupata mtoto ndani ya ndoa, wengine wanataka msaada wa mwanandoa, wengine wanataka makaratasi, wengine wanakuwa pressured na jamii there are so may reasons for so many people. Unaposema "cha kwanza kabisa anaoa/kuolewa kwa ajili ya nini" naona kama unataka kufanya watu wote wanafikiri sawa na wana historia sawa inayowafanya waiangalie ndoa kwa jicho lile lile.

This could not be more misguided.
 
Haahaaa duuuh wewe pole yako, yani uliamua kuolewa kwaajili ya hayo? Haahaa
 
Hapa kinachoongelewa ni NDOA kwa ujumla (general)
Haijalishi ndoa ya aina gani, suala kuu ni nini muoaji au muolewaji kilimsukuma kulekeleza tendo!
 
.......Ndugu yangu kwa zama hizi zetu hata mtoto wa darasa la pili anajua mtu anaoa au kuolewa kwa lengo gani,hayo mengine hua yanafuatia tu.

Umeoa/umeolewa/utaoa/utaolewa nini kitakusukuma/kilikusukuma kufanya hivyo?
 
Hapa kinachoongelewa ni NDOA kwa ujumla (general)
Haijalishi ndoa ya aina gani, suala kuu ni nini muoaji au muolewaji kilimsukuma kulekeleza tendo!

Kuna mwanamke huko Fargo North Dakota, Nadine Schweigert kaamua kujioa yeye mwenyewe, na huyu naye anaingia katika hiyo definition yako isiyo na definition?

http://www.huffingtonpost.com/2012/05/25/nadine-schweigert-woman-marries-herself_n_1546024.html

Unapoandika "Hivi binadamu anapoamua kuoa/kuolewa, cha kwanza kabisa anaoa/kuolewa kwaajili ya nini?" unamuongelea binadamu gani? Swali halijaeleweka kwa sababu halijaeleza kwamba linakusudia kupata jibu moja lililo husika kabisa kwa binadamu wote ama majibu mbalimbali kutoka kwa binadamu mbalimbali.

Kauli.
 
mie nadhani ukipata 'the right person' na wazo la ndoa linaanza kuja.

Kuna mtu anatamanisha kuwa na familia naye lol
 
Kuna mwanamke huko Fargo North Dakota, Nadine Schweigert kaamua kujioa yeye mwenyewe, na huyu naye anaingia katika hiyo definition yako isiyo na definition?

Nadine Schweigert, North Dakota Woman, 'Marries Herself,' Opens Up About Self-Marriage

Unapoandika "Hivi binadamu anapoamua kuoa/kuolewa, cha kwanza kabisa anaoa/kuolewa kwaajili ya nini?" unamuongelea binadamu gani? Swali halijaeleweka kwa sababu halijaeleza kwamba linakusudia kupata jibu moja lililo husika kabisa kwa binadamu wote ama majibu mbalimbali kutoka kwa binadamu mbalimbali.

Kauli.
Mkuu bado narudi palepale kuwa mjadala huu ni wajumla, suala ni kuoa/kuole na hata huyo aliyejioa mawazo yake tunayahitaji kwanini alijioa?

Naamini hapa tutapata majibu mengi na lengo lete ni kupanua wigo wa elimu ya mahusiano huku tukijikita ktk dhamiri kuu ya ndoa nini????

Kwanza umeoa/umeolewa/umejioa kwanini umefanya hivyo?
 
Mie ukweli nilichoka na sheria za nyumbani mpaka madukani lazima upelekwe ukichelewa kurudi utakiona kilichomtoa kuku
manyoya,nilikua nafanya kazi lakini story ikawa hiyo hiyo nikaona bora niolewe yaishe tutapenda huko huko mbele ya safari
lakini alhamdulilah namshukuru mungu mpaka hapa tulipofikia...

ulichaguliwa mume?????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom