Nini cha kujifunza yanayoendelea Mali, Belarus na Thailand tukiwa tunaelekea Uchaguzi?

Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
4,352
3,532
Kama unafuatilia vyombo vya habari nchi ya Mali moto umefuka. Wananchi waliingia mitaani mpaka raisi aliyetawala miaka 25 na ushee aondoke. Wanajeshi wakamteka Rais na waziri Mkuu, wakakamata nchi. Sema wanajeshi kiroho safi wataandaa uchaguzi wa huru wameahidi.

Belarus, wananchi wameingia kitaa. Raisi atoke hawamtaki kashinda uchaguzi 80% lakini wananchi wanasema wizi mtupu. Wanataka katiba mpya Style ya #sasaBaasi flani hivi. Mpinzani wa karibu ambae ni mwanamama kuona fujo kakimbilia nchi jirani mumewe yuko gerezani

Full fujo. Russia ambaye ni nchi jirani anamtetea Raisi alie madarakani. European Union wanasema rais wa Belarus atoke au uchaguzi urudiwe. Umeiba kura. Kimbembe. Jamaa mbuzi kagoma

Thailand Bangkok huko kitaa kimejaa watu kama sisimizi. Story ndefu lkn ni kama za hapo juu tu.

Duniani siku hizi watu wakisema #sasabaasi uwe muangalifu sana.

Je, tuna la kujifunza hapo kwa matukio hayo matatu?
 
Ni kama hai wananchi walivyoingia mitaani - kumkataa Lissu
Ule ni uhuni na upumbavu na ulofa.

Lisu ana Haki ya kueleza umma wa watanzania na dunia nzima dhulma aliyotendewa.

Hivi wale viongozi wa CCM wanaosimamaga kwenye majukwaa na kusikiliza kero za wananchi waliodhulumiwa viwanja vyao au kuonewa kwa kunyimwa Haki kwenye familia zao na Kuzitolea majibu au kuzitatua wako wapi Leo ?
Kwa nini hawasikilizi kilio na maumivu aliyoyapata Tundu Lisu?

Hivi kuna Kero na madhila makubwa anayoweza kupata binadamu zaidi ya mtu kupigwa Risasi 16 mwilini achilia mbali zilizomkosa?

Ni nani atafanyiwa hivyo halafu akae kimya asilalamike? Na je, waliopaswa kujitokeza na kulaani vukali kitendo kile cha kigaidi walijitokeza hata kutoa pole kwa Lisu na familia yake iliyoumizwa na kitendo kile kiovu hata mbele za Mungu?

Sasa zile kero wanazotatuaga ni za kutafuta umaarufu au ni kuzitatua kweli kwa binadamu wenzao ? Na kwa nini kero ya Lisu haikusikilizwa na haisikilizwi na waliopaswa kuisikiliza na kulaani na kuwakamata waliozembea au waliohusika na uovu ule.?

Kwa sababu nchi ni ya wananchi basi Wameamua kumsikiliza Lisu na kumpa kura za Huruma.

Hata mutume wa zamani wanatajwa Leo kwa sababu ya madhila waliyofanyiwa kwa kupinga dhulma za watawala wa dunia.

Maana mpaka sasa Lisu hajaanza kampeni zaidi ya kuendelea kuwaeleza watanzania nia yake ya kugombea Uraisi , kuwashukuru kwa kumchangia kwenye matibabu na kumwombea pia , kuomba udhamini watu wamdhamini huku akiwaeleza kuwa amepona baada ya kunusurika kifo baada ya kupita kwenye wakati mgumu baada ya serikali na Bunge kumwekea mazingira magumu kwa makusudi bila kujali kuwa anatetea uhai wake ambao kila mwanadam anatamani kuupata.

Nani asiyependa kuishi ! Hata wanaofanya mazuri na makubwa kwa nchi bado wanahitaji ulinzi mkubwa japo wanajiita marafiki na wapenda watu lakini wamezungukwa na mabunduki kila kona ili kujilinda.

Sasa kumfanyia Lisu vurugu ni ujinga. Hajajiteua na hatajichagua ,kura ndio zitaamua kama zilivyoamua kwa aliyepo. Ndio maana tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Tuwe tayari pia kukosa kura na sio kufanya fujo. Wote sisi ni binadamu hakuna malaika anayekuja kuomba kura hivyo tusijisahau kuwa kuna watu zaidi ya wengine.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom