Alexander The Great
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 4,502
- 23,582
Habari Wana Kijiji,
Kwa muda tunapost thread nyingi ni za kuomba msaada/umbea/habari na kupeana ushauri. Leo nimeamua kuja na thread hii ya kufundisha/kukumbusha/kuelimisha na kutahadharisha.
Ukimwi (H.I.V) kwa maisha ya sasa si HUKUMU YA KIFO TENA kama ilivyokua hapo awali. Gonjwa hili limeshaua mamilioni ya watu hapo mwanzoni, tofauti na sasa unaweza kuishi miaka mingi sana hata kama ni muathirika, japo bado linaendelea kupoteza maisha ya watu wengi sana duniani.
NOTE THAT: Nikumbushe tu, chukua tahadhari kwani gonjwa hili bado lipo na linaangamiza watoto/vijana na wazee wa kila jinsia kila siku ipitayo.
Nirudi kwenye mada husika.
"POST EXPOSURE PROPHYLAXIS au kwa kifupi PEP" ni njia ya dharura sawa na njia ya kutumia ARV au ART.
Hii PEP ni dose ya dawa kama ilivyo ARV au ART ambayo mtu hutumia mara tu baada ya kukutana kimwili na muathirika wa ukimwi au kujichoma na kitu chenye ncha kali ambacho kimetumiwa na muathirika huyo.
Lengo la dawa za PEP ni kuzuia mtu asiathirike na gonjwa hili la ukimwi mara tu baada ya kugundua au kuhisi anaweza kuwa amepokea vinasaba vya damu iliokwisha athirika na ukimwi kutoka kwa muahirika. Dose hii ya dawa inapaswa mtu kuanza kutumia mara tu baada ya kuhisi anaweza akawa amepokea vinasaba hivyo vya damu iliokwisha athirika kwa muda usiozidi masaa 72 (Yani mtu aanze kutumia dose kabla ya masaa 72 hayajapita), au lasivyo dawa hazitofanya kazi.
PEP ni dose ya dawa ya kuzuia maambukizi ya ukwimi kwa dharura mara tu mtu anapokua amefanya mapenzi au kupokea vinasaba vya damu na mtu alie athirika (Yasizidi masaa 72). Sio kwaajili ya mtu aliekwisha athirika tayari.
Wana kijiji, tujilinde, ukimwi upo na unauwa kama hatutoji kinga.