Nini cha kufanya gari inapowasili kutoka Japan

mussamoses14

Member
Aug 14, 2017
6
1
WanaForum habari zenu.
Nimegiza gari kutoka Japan Mark x/2005 na ipo karibu na kuwasili. Nahitaji kujua (from technical point of view) nini natakiwa kufanya kabla ya kuiingiza gari barabarani?
Niliwahi kuona thread inaelezea kuwa unatakiwa ubadilishe oil types zote za gari na kuweka mpya. U-replace any fluid/gas uweke mpya na vitu mfano wa hivi.. je ni kweli?
Nahitaji kuelimishwa sina ujuzi sana na hivi vyombo vya usafiri.
 
Gari yoyote ukinunuwa ikiwa used lazima ujiridhishe wewe mwenyewe kwa kuifanyia full service hujui yule aliyokuwa anaitumia aliitumiaje na service alifanya lini. Hapo na matairi jipange kuweka mapya yote. Labda na shocks kama hazina hali nzuri na zinakuwaga za umeme hizo.
 
Nashkuru kwa mchango wako kiongozi
 
actually inategemea na sehemu uliponunua gari yako, now days kuna service 'inspections fee' ukilipia linafanyiwa check up zote na inajazwa card ambayo ilitakiwa utumiwe kabla ya gari kuja kujiridhisha!

otherwise better likifika mtafute fundi afanyie check up kwani its very easy and simple (within 20 minutes) anaweza jua conditions ya fluids zote, matairi its simple anaangalia pembeni atajua namba na expire date.

by the way most time magari yakija 90% yankauwa okey for use na kama lina any fault huwa wana specify problem before
 
LIFANYIE DIAGNOSIS KWANZA, THEN PIGA FULL SERVICE,,,HOPE CHENJI BADO IPO. THEN BAADA YA HAPO IPE MASAFA MAREFU KAMA KILOMETA 800 HIVI AU ZAIDI KWENYE LAMI. BAADA YA HAPO PITA ROUGH ROAD KIDOGO UJUWE UBORA WA SHOCK UPS. THEN TUWE TUNAKUTANA SHELI
 
Nina kaujuz kidogo, maana nimeshaagiza gari zaidi ya mara 3, sikia sasa ikifika tu badilisha engine oil (weka BP Oil) (recommended) , Gear box oil sio muhimu sana kubadilisha ila fundi anaweza akacheki akakuambia, cheki betri kama bado liko poa na matairi,nadhan hvyo ndo vya msingi..ila hongera maana mark X wese lake sio kitoto, zinaingia passo kama 8 hv humo kwenye mark x
 
Nimekuelewa vizuri kiongozi, thanks a lot for info
 
Nashk
Nina kaujuz kidogo, maana nimeshaagiza gari zaidi ya mara 3, sikia sasa ikifika tu badilisha engine oil (weka BP Oil) (recommended) , Gear box oil sio muhimu sana kubadilisha ila fundi anaweza akacheki akakuambia, cheki betri kama bado liko poa na matairi,nadhan hvyo ndo vya msingi..ila hongera maana mark X wese lake sio kitoto, zinaingia passo kama 8 hv humo kwenye mark x
Nashkuru Mkuu , ntafanyia kazi ushaur wako
 
LIFANYIE DIAGNOSIS KWANZA, THEN PIGA FULL SERVICE,,,HOPE CHENJI BADO IPO. THEN BAADA YA HAPO IPE MASAFA MAREFU KAMA KILOMETA 800 HIVI AU ZAIDI KWENYE LAMI. BAADA YA HAPO PITA ROUGH ROAD KIDOGO UJUWE UBORA WA SHOCK UPS. THEN TUWE TUNAKUTANA SHELI
Nashkuru Mkuu , but one more question; hiyo FULL SERVICE inacover nini
 
Nina kaujuz kidogo, maana nimeshaagiza gari zaidi ya mara 3, sikia sasa ikifika tu badilisha engine oil (weka BP Oil) (recommended) , Gear box oil sio muhimu sana kubadilisha ila fundi anaweza akacheki akakuambia, cheki betri kama bado liko poa na matairi,nadhan hvyo ndo vya msingi..ila hongera maana mark X wese lake sio kitoto, zinaingia passo kama 8 hv humo kwenye mark x

Ni kweli. Hata TOTAL iko poa sana. Ila kwenye kubadilisha oil ndio kuna shida. Mafundi wengi wanabahatisha/wanatumia mazoea tu. Na nilishaumbua wengi baada ya kuamua kufuatilia issue za oil za magari na kupata uelewa kiasi fulani.

Kama manual haipo google ujue gari yako inatumia oil gani, 5w30, 10w30, 5w40 n.k. Hizo namba mafundi wengi hawajui maana yake. Wao wanachojua tu "AAh gari ndogo inatumia oil namba 40!" basi; bila kujua kila gari ina specific oil yake. Kingine wasichozingatia ni ujazo wa oil. Mara nyingi wanaweka nyingi hadi inapita kwenye mark yake. Eti ikizidi kidogo sio mbaya! mmmh?? Kwani walioweka hiyo mark ni wajinga? MUHIMU NI KUJUA AINA YA OIL NA KIASI KINACHOTAKIWA.

Regards!
 
Tuseme tukiwaona wenye Mark X tuwape shikamoo!
hata mm najiuliza
lkn huenda mtoa post kamaanisha huo mgari sio wa kupigia misele mitaani, km sokoni, kupeleka watoto shule nk
mMark X ni kwa ajili ya kuendea bara tena kule kusikokuwa na limit ya 50km/h
hayana tofauti na kina Brevis cc 2500 100ltr Dar-es-salaam - Dodoma
wakati Passo kako cc990 20lts Dar - Dodoma
hayo yangu msini Quote
 
Nina kaujuz kidogo, maana nimeshaagiza gari zaidi ya mara 3, sikia sasa ikifika tu badilisha engine oil (weka BP Oil) (recommended) , Gear box oil sio muhimu sana kubadilisha ila fundi anaweza akacheki akakuambia, cheki betri kama bado liko poa na matairi,nadhan hvyo ndo vya msingi..ila hongera maana mark X wese lake sio kitoto, zinaingia passo kama 8 hv humo kwenye mark x
Kwanza tutake radhi wenye passo zetu ila bado najiuliza passo zinaingiaje 8 kwenye mark x tena ya mwaka 2015
 
Mark X inaingia lita 6 za engine oil...gari ikitoka Japan inakuja na inspection report kuwa iko poa na default zilizopo huwa zimeainishwa kwenye Cheti, inakuja na oil nzito kabisa (test viscosity), wewe ni kuweka wese tu na kwenda zako kwako, labda uangalie na coolant (maji ya kupooza engine kama yapo ya kutosha) oil badilisha baada ya km hata 1000 ili uanze na hesabu zako...that's all kwa technical, kingine usisahau comprehensive insurance
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom