Nini cha kufanya endapo utapewa likizo ya yeye kujitafakari kama muendele au muachane?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Baada ya misukosuko ya hapa na pale ya Mimi na mpenzi hatua tuliofikia ni kupeana likizo kwa muda.

Ambapo mpenzi wangu ameniomba nimpe miezi mitatu ya kutulia na kujitafakari kama tuendelee au tuachane kila mmoja ajitathimi na kujitafakari kama ni kuendelea au kupotezea Mimi upande wangu nilishaonesha nia kukubali kusemeana pale tulipokoseana baada ya mmoja ya rafiki yangu kujaribu kutusuluhisha.

Ila mwenzangu upande wake ameomba apumzike kidogo huku akinipa Mimi muda wa kujitathimini na yeye kujitathimini.

Sasa naombeni ushauli kipindi cha kujitafakari nini cha kufanya kwani mahusiano yenyewe yako rehani muda wowote yatavunjika?
 
Tafuta demu mwingine wa kula nae starehe huo muda akiwa bado yeye anatafakari, pia usimtafute

Kwanza miezi mitatu si ni kuachana na kabsa huko, mwanaume usiwe king'ang'anizi achana nae.
 
Kwahiyo hapo bado unahitaji nini ili kujua kuwa mwanamke hakutaki tena.? Kidogo kutakuwa na matumaini kama huyo mwanamke ni mke wako, hata ivyo nina imami sio mkeo, kwasababu angekua, huo mgogoro usingeishia kwa rafiki, ungepelekwa kawa wazazi, maana unaonekana kuwa mkubwa sana, kiasi cha kupeana likizo.

NB:Kama sio mkeo, jiulize hiyo likizo atakuwa wapi? Huenda atakuwa kwa rafiki yako, aliwasuluhisha.
 
Duh! Pole sana tena sana,,
Kwanza tafuta pesa,,kisha tafuta tena pesa ,
Baada ya hapo endelea kuwa busy na kutafuta pesa,
Sasa ruhusu mrembo mwingine akupetipeti,,
Huku ukiwa umesha futa mawasiliano na huyu wa likizo za kujitafakari,na siku akikutafuta mpe mwaka mmoja kwanza kujitafakari kipindi akiwa likizo ya kupumzika
 
Ungekua baharia kuna mambo yakufanya tu mpaka akajikuta analiwa bila hata kusamehe.


Ila kwakua wee ni Mstaharabu, basi achana naye, miezi mitatu????


Ulimkosea nn???
 
Yalinikuta hayo sema mimi aliniambia aende kwao mwezi mmoja

kumbe alikuwa ananipima imani yangu......sikumtafuta mwezi huo mzma na yeye hakunitafuta.

Baada ya miezi miwili akarudi home kwangu akanikuta nmeshaweka demu mwingine MIMBA ya mwezi mmoja na nusu na alimkuta ananiandalia msosi.

Nakumbuka ilikuwa usiku.....akaanza kujililisha akiniambia eti mimi nilikuwa nakupima tu kama unanipenda au laah....kumbe ulikuwa hunipendi wewe.....lakini mimi bado nakupenda mpenzi wangu.

Nikawa sina chakumsaidia tukamtoa njee saa tano za usiku....tukamwacha anajililisha huko nje tukalala zetu.

Mpaka leo cjui yuko wapi yule mwanamke.
 
Well sijasikia the other side kuna nini hadi ikafikia hapo but kuiwa mpole, kama unadhani uko na future nae basi subiri kama unaoan ni kupitishia muda kubali tu kuwa yamefikia mwisho. Asikudanganye tu wote tunapitia hizo situation though kwa mitazamo tofauti, pole sana.
 
Mweeeeeeh Dunia inaenda kasi sana, hadi mahusiano ya mapenzi yana likizo. Uwiiiiiiiiih
 
Bora ukae kimya na kufanya mambo yako coz ukifanya juhudi za kulazimisha penzi lisivunjike jiandae kuwa mtumwa wake,hakupendi tena
 
Polee mkuu,
Akufukazaye akwambi toka.
Huyo amekuheshimu sana, hila hiyo ni namna yakusema it's Over.
Usisahau kumsikiliza Melanie C, never be the same again
 
Tafuta demu mkali zaidi yake alafu tulia nae wakati unasubiria mda wa kutafakari kuisha.
 
Baada ya misukosuko ya hapa na pale ya Mimi na mpenzi hatua tuliofikia ni kupeana likizo kwa muda .

Ambapo mpenzi wangu ameniomba nimpe miezi mitatu ya kutulia na kujitafakari kama tuendelee au tuachane kila mmoja ajitathimi na kujitafakari kama ni kuendelea au kupotezea Mimi upande wangu nilishaonesha nia kukubali kusemeana pale tulipokoseana baada ya mmoja ya rafiki yangu kujaribu kutusuluhishaaa.

Ila mwenzangu upande wake ameomba apumzike kidogo huku akinipa Mimi muda wa kujitathimini na yeye kujitathimini.

Sasa naombeni ushauli kipindi cha kujitafakari nini cha kufanya kwani mahusiano yenyewe yako rehani muda wowote yatavunjika
Kwa kifupi tuu mkuu hapo kuna mambo makuu matatu unatakiwa uelewee

1.cha kwanza kuna uwezekano mkubwa binti amepata mwanaume mwingine hivyo yuko kwenye process ya kukuacha taratibu bila kukuachia maumivu.

2.cha pili inawezekana binti alikuwa na matarajio makubwa mfano kuolewa nawe au pesa sasa anapoona Yale matarajio yake hakuna basi huanza proccess ya kukuacha taratibu

3.cha tatu binti kapata mtonyo unamuingizia hela hivyo mazingira mapya ya kupata pesa humjengea kiburi na kukuzalau .

Sasa nini unachotakiwa kufanya ukiona hivyo aanza kujitenga mbali na binti, punguza mawasiliano nae, kuwa bize na mambo yako hali hapo kuhusu mapenzi hapo disco kaingia mmasai
 
Back
Top Bottom