Nini athari za Kiuchumi katika kutumia fedha za Ndani Miradi Mikubwa

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,127
Wachumi wetu ebu tusaidieni sisi tulioko vijijini huku (Mwanduhitije) kama kuna athari zozote za kiuchumi katika kutumia pesa za ndani katika Miradi mikubwa kama Standard Gauge Railway (SGR) na tena huu wa Stiglers Gauge tulioambiwa unaanza hivi karibuni !!!

Na Je,ile Gesi ya Mtwara tuliyoambiwa mpaka sasa inatumika asilimia 6 tu kwa nini isitumike kuzalishia umeme kabla ya kwenda kwenye hiyo Project nyingine ya Stiglers Gauge?!
 
Hivi ni gas inatumika kwa 6% au uwezo wa bomba unatumika kwa 6% (not sure with figure)?

Kama ni bomba ndilo linatumika chini ya uwezo wake, tafsiri yake ni kwamba uzalishaji wa gas ni mdogo kuliko ukubwa/uwezo wa bomba kusafirisha gas!!

Kiwango cha uzalishaji chenyewe kinategemea na reserve iliyopo au uwezo/capacity ya uzalishaji wenyewe...!!!

Suala la pesa za ndani na miradi... ni hoja pana! Ni pesa za ndani za aina gani?! Zinatokana na mapato ya serikali au zinazotokana na mikopo ya ndani?

Kama kwa kiasi kikubwa ni zile zinazotokana na mapato ya serikali effect kubwa ni kuchelewesha kwa miradi mbalimbali... hiyo iliyo kwenye pipeline na mingine vile vile!! Ni sawa na mfanyabiashara wa kawaida anayetegemea kufanya biashara kutoka kwenye pesa za mfukoni pekee wakati uwezo huo hana!

Pia inaweza kusababisha kupanda thamani kwa $$$ kwa sababu mapato makubwa ya serikali yanatokana na local currency wakati matumizi makubwa ya hiyo miradi yanahitaji foreign currency jambo linaloweza kusababisha demand for $$ ili ku-finance hizo projects!!!!

Aidha, kama serikali inakopa sana kwa vyombo vya fedha za ndani kuna hatari ya kuzorotesha mikopo kwa sekta binafsi kwa sababu bank zitapenda sana kufanya biashara na serikali ambayo ni less risky kuliko kufanya kazi na individual business persons hasa ukizingatia ukweli kwamba mabenki hayana liquidity ya kutosha.

Hata kama serikali itakuwa inakopa kwa mtindo wa ku-issue government bonds bado athari za hapo juu zitabaki pale pale kwa sababu, mabenki yatakimbilia kununua dhamana za serikali kuliko kutoa mikopo kwa SMEs!!!

Athari za hoja hiyo hapo juu inaweza kusababisha decline in private sector ambayo nayo ina mlolongo wa athari!!!

Hizo ni chache tu... ukinyambua utapata zingine kadhaa!!

Lakini usisahau kuna faida zake vile vile!!!
 
Ni ukichaa tu unasababisha ukosefu wa busara na priorities tulionao watanganyika. kama tungekuwa na viongozi wenye busara na akili japo kidogo wangehakikisha bomba linatumika japo asilimia 60 kabla ya kurukia mradi mpya. kwa sababu riba ya ujenzi wa bomba inaendelea kuzaliana wakati tumeenda kurukia mradi mwengine ambao kwa hakika asilimia 10 tutakopa.

hadithi ya fedha za ndani ni mazingaombwe kwa sababu hata fedha za reli tutakopa tu, kwa uwa hakuna fedha za kutosha kuendesha serikali na kukabiliana na miradi mikubwa kama hii.
 
Mkuu Kimweri sema unatania au umekosea!!!

Mradi mwingine 10% WATAKOPA?! Wakope 10% halafu hiyo 90% waitoe wapi?! Kwa mfano evaluation ya 2006, gharama za phase zote kwa Stiegler's Gorge ilikuwa ni $2Billion... kwahiyo kwa uchache hivi sasa ule mradi utahitaji angalau TZS 5 Trillion!!

Au labda kwavile wanasubiria trillions za Acacia!!!
 
Wachumi wetu ebu tusaidieni sisi tulioko vijijini huku (Mwanduhitije) kama kuna athari zozote za kiuchumi katika kutumia pesa za ndani katika Miradi mikubwa kama Standard Gauge Railway (SGR) na tena huu wa Stiglers Gauge tulioambiwa unaanza hivi karibuni !!!

Na Je,ile Gesi ya Mtwara tuliyoambiwa mpaka sasa inatumika asilimia 6 tu kwa nini isitumike kuzalishia umeme kabla ya kwenda kwenye hiyo Project nyingine ya Stiglers Gauge?!
Kwanza tofautisha kati ya 'gauge' na 'gorge'. Pili hilo bwawa la stiegler's gorge litazalisha umeme mara 10 ya huo wa Kinyerezi kwa gharama nafuu mno, see the logic?
 
Usijali sana mkuu. Hela za ndani zenyewe hakuna. Vumilia tu sababu hakuna madhara.
 
Back
Top Bottom