Nini athari ya siasa za makundi ndani CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini athari ya siasa za makundi ndani CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teamo, Mar 2, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  KWA MUJIBU WA MAELEZO YA WANASIASA WENGI wakongwe kabisa, inaonekana kuna kile kinachoitwa SIASA ZA MAKUNDI NDANI YA CHAMA TAWALA!

  Imefahamika pia siasa za makundi ZINAATHIRI MAAMUZI YA BUSARA YA SERIKALI KWA MASLAHI YA NCHI.....!

  WANAJAMII NINAOMBA NISAIDIWE UFAFANUZI WA HILI linaloitwa SIASA ZA MAKUNDI NDANI YA CHAMA TAWALA na namna linavyoiathiri serikali ya awamu ya nne.....
   
 2. K

  KGM Senior Member

  #2
  Mar 2, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maelezo yako hapo na michango yako mingine kwenye thread nyingine pamoja na link http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=2809 inaonyensha kuna kitu mzee mnataka kupata kutoka DOWNS. Kama siyo wewe mwenyewe basi umetumwa kutetea DOWNS. na hao wanatetea maamuzi mabovu ambayo wewe unayaita mazuri.

  RUSHWA ni mbaya kwani inapofua waonao. Hayo maamuzi mazuri ya CCM ni yapi!!!!?.
  Ushindwe na Ulegee.
   
 3. K

  KGM Senior Member

  #3
  Mar 2, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dk. Slaa: Ununuzi mitambo ya Dowans utaifa kwanza  na Edward Kinabo
  SAKATA la nia ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kutaka kununua mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura yenye uwezo wa kutoa megawati 100 inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans, linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha.

  Jana Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa, akizungumza kwa simu na Tanzania Daima, alisisitiza kuwa suala hilo linapaswa kujadiliwa na kuamuliwa kwa kuweka mbele maslahi ya taifa na si umaarufu wa kisiasa.

  Alisema suala la kununua au kutonunua mitambo hiyo linaihusu serikali na TANESCO yenyewe kwani ndio wanaohusika na utendaji na si Bunge kama inavyoonekana kupotoshwa.

  Alisema kazi ya Bunge ni kuisimamia serikali na si kufanya kazi ya utendaji kama suala la ununuzi wa mitambo; anatoa wito kwa kamati za bunge zinazohusika na suala hilo kujadili na kutoa ushauri utakaomsaidia mwananchi.

  "Maswala ya ununuzi si ya Bunge; ni ya serikali. Serikali ndiyo inayoweza kuamua kununua au kutonunua, kazi ya Bunge ni kusimamia utekelezaji wa serikali. Cha msingi ni kuweka mbele maslahi ya taifa na kufuata taratibu.

  Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, aliiambia Tanzania Daima kwa simu jana, kuwa siasa za makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndizo zinazochochea baadhi ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kuendeleza malumbano yasiyo na msingi, kuhusu dhamira ya TANESCO kutaka kununua mitambo hiyo.

  Alisema hakuna mgogoro wa msingi kati ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na ile ya Nishati na Madini, kuhusu suala la TANESCO, kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari jana.

  Alisema malumbano kuhusu suala hilo yanakuzwa kwa sababu ya kuwepo chuki za kisiasa na makundi ndani ya CCM, hali inayofanya baadhi ya wabunge wa chama hicho kukataa suala la TANESCO na mitambo ya Dowans lisijadiliwe, kwa sababu tu ya kile kinachoonekana kuwa ni kuendeleza mapambano dhidi ya maadui zao kisiasa.

  Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa kamati hizo mbili kukutana pamoja na TANESCO ili kupata ufumbuzi wa suala hilo badala ya kuendelezwa malumbano yasiyo na msingi kwa mwananchi.
  juu
  Maoni ya Wasomaji
  Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
  Maoni 23 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
  Kijana Zitto angalia hili suala litakushushia umaarufu na heshima kwa wananchi. Wengi tulikuamini lakini sasa inaonekana nawe waweza kutumiwa na aina Rostam kuwanufaisha kwenye mitambo yao iliyoingizwa nchini kifisadi. D. Rashidi ni fisadi na yumo kwenye skendo ya ununuzi wa rada na mzee wa vijisenti. Kwani serikali imewaambia haina pesa za kununua mitambo mipya mpaka kung'ang'ania kununua hii mitambo chakavu ambayo ni kinyume na sheria za manunuzi ya nchi?
  Nanukuu kipengele kaika gazeti la mwananchi la leo kuhusu hili suala:
  Katika mahojiano na gazeti la serikali la Daily News yaliyofanyika Juni 31, 2008, Dk. Rashid alisema kuwa taratibu zote za kuingia mkataba baina ya Richmond na Tanesco zilikiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma na hivyo kuwa batili na kwamba hata kama usingekuwa batili, taratibu za utoaji wa majukumu ya tenda hiyo kutoka Kampuni ya RDEVCO badala ya Dowans Holding SA na baadaye Dowans Tanzania Limited haukuwa na msingi wa makubaliano na hivyo kuwa batili.


  "Ukweli ni kwamba mkataba ulikuwa kati ya Richmond Development Company LLC na Tanesco na na sio Redvco na Tanesco," Dk. Rashid alikaririwa na Daily News wakati huo huku akifafanua kuwa jina la RDC LLC lilikuwa la kufikirika kwenye mkataba na kwamba kampuni hiyo haikusajiliwa Texas, Marekani.


  Alidokeza kuwa Dowans Holding SA ilisajiliwa nchini Costa Rica ikiwa na mtaji wa dola 100 za Marekani (takriban Sh 131,000 za Tanzania).


  Baada ya kuvunja mkataba huo, Dowans iliishtaki Tanesco kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara iliyo Paris, Ufaransa, uamuzi uliolifanya shirika hilo kushikilia mitambo ya Dowans likidai kuwa itatumika kama fidia iwapo Dowans itashindwa kesi"

  Swali: hii kesi kati ya Dowans na Tanesco imeshakwisha na mamuzi yakoje? Mbona mitambo iliyoshikiliwa kwa kufidia kesi kamaTanesco watashinda sasa inauzwa kwa Tanesco wenyewe? Hapa kuna mkanganyiko na kila dalili za rushwa. Bwana Rashid hebu atufafanulie hii kauli yake aliyoitoa kwa gazeti la DailyNews mwaka jana. Ufisadi mtupu hakuna cha maslahi a nchi wala nini.


  na MTZ, TZ, - 28.02.09 @ 17:06 | #13017

  Hongera Kabwe, Hongera slaa. maslahi ya taifa kwanza tukiwa katika giza na uchumi unachuchumaa umaarufu wa kisiasa hautatupa tija. KAMA BISHARA NI NZURI NUNUA MITAMBO HIYO NA SWALI LIISHE.

  Peter

  na Peter - 28.02.09 @ 19:53 | #13048

  Sikutegemea kuwa zitto anaweza akawa mjinga kiasi hiki. Lakini tuliwaona wakina Mrema na Mtikila enzi hizo wakibebwa na mashabiki wao kumbe hamna kitu sasa hivi wamekishwa muflisi wa kisiasa. Kama mambo yenyewe ni haya sitashangaa Zitto na wenzake chadema wanao pigia ngoma ununuzi wa mitambo ya dowans wakijaishia kwastaili hii hii yawenzao. Ila namuonea zitto huruma ukijiingiza kwenye siasa halafu ukafirisika ukiwa bado kijana inakuwa ni mateso matupu.

  na Longii.T, Tanzania, - 28.02.09 @ 21:23 | #13060

  Jamani kama changa la macho wabongo mmekwisha, mbona mnakuwa kama mmelishwa madawa ya kulevya toka mexico jamani mitambo hiyo bomu bomu mbona hamsikii, nunueni mipya difference ni ndogo, watu wanataka wachukue chao kabla ya uchaguzi ujao ili pesa hiyo watumie kwenye kampeni acheni ukame uje msoto kwa mda na solution ya kudumu achana na Dr Idrisa na Zitto wote wasanii tu miminiko usa hiyo mitambo ni gabege yaani takataka ya kutupwa shimo la taka achaneni nayo inahitaji maintenance kubwa sana bora kununua mipya jamani jamani waziri wa nishati achana na hayo maskrepa nunueni mipya.

  na wind, usa, - 1.03.09 @ 01:23 | #13084  Kesi ya TANESCO na DOWANS INTER., imekwisha.

  Mitambo ya DOWANS, iliyokuwa ina shikiliwa na TANESCO, ikiwa kama fidia, kama TANESCO ikishinda kesi, IPO!!!.

  Tanesco imeshinda kesi, kwa hiyo mitambo ni mali ya Tanesco mpaka sasa na wameshabadilishana makaratsi kwa mujibu wa Dr Rashidi.

  Sasa hizo MG-WATTS 100 mbona zina shida tena jamani????.

  na Kweka, NSW - 1.03.09 @ 05:54 | #13096

  Sijaona sura mpya yoyote katika hili sakata, eti kwa vile tu slaa na zitto wameongea...

  na Mima, Tz, - 1.03.09 @ 06:58 | #13097

  HEBU NIPENI E-MAIL ADDRESS YA ZITTO AU NAMBA ZAKE ZA SIMU MAANA NAONA NA YEYE SASA ANAANZA KUCHEMSHA KABLA YA 2010.ANAKUWA MSEMAJI MKUU KWENYE SEREKALI ILIYOOZA YA CCM KWA VIPI?.WAACHIE WAPARANGANE NA UOZO WAO WEWE KIJANA USIJICHAFULIE SIFA ZAKO BURE.

  na OLE LETIPIPI, TANZANIA, - 1.03.09 @ 09:19 | #13109

  Zito Kabwe na DR SILAA,ni viongozi wa Kamati za Bunge ambayo wajumbe wengi ni wabunge wa CCM.Nimegundua kuwa W/viti hao hawawezi kubadili chochote ktk suala la TANESCO na WIZARA YA NISHATI NA MADINI kwani hawa ndio serikali na ndio watendaji wakuu.Suala hilo ni la serikali ya CCM,sio la akina ZITTO na DR SILAA!CHADEMA wanatumia busara sana usipime!Wanajua CCM na serikali yao wakiamua watafanya chochote kutokana na wingi wao bungeni.Mi naona tuwachague wabunge wengi toka upinzani ili tubadili hali ya kisiasa na kiuchumi TZ.

  na Marios, Tz, - 1.03.09 @ 10:19 | #13124

  Serikali kama inagangania kununua mitambo iliyo tumika badala ya mipya je kesho na kesho kutwa watasema mitambo nimibovu ukinunua mashine ambazo ni used hiyo haina grantee maana ujanunua kiwandani sasa sheria ya kuuza na kununuzi wanaifahamu hawa vingozi wa serikali kwa nini wasitumie busala ya kawaida kununua mitambo mipya kuliko hii ya zamani wanacho ga'ngania kuinunua nini? kama wanataka kununua wanunue kitu chenye uhakika mashine mpya

  na daudi na maria - 1.03.09 @ 11:18 | #13126

  TANESCO ni chombo chenye mamlaka kamili ya utendaji. Tuwaachie bodi ya TANESCO iamue sakata hilo ili bdae bunge linapopokea taarifa ya kiutendaji liweze kuamua kwa kuangalia maslahi ya kitaifa.

  na Paresso, arusha, - 1.03.09 @ 11:23 | #13127

  NIJAMBO LA KUSIKTISHA SANA KWA SHIRIKA KUBWA LA KITAIFA KAMA TANESCO,LINALO TEGEMEWA NA TAIFA KUNUNUA MITAMBO CHAKAVU,NA ZAIDI INA KASHFA NA PIA INA KESI YA MADAI NA WAMILIKI WA MTAMBO WENYEWE,WATANZANIA TUMESHAZOEA TABU YA UMEME IKIWA TANESCO ITATUAIDI TUVUMILIE KWA MIEZI 6 ZAIDI ILI WAWEKEZE KWA MTAMBO MPYA WENYE UHAKIKA WA KUTATUA TATIZO LA UMEME TUKO TAYARI INGAWA UCHUMI UTAYUMBA KIDOGO,LAKINI DAWA ITAKUA IMEPATIKANA,SIMSHANGAI ZITO NI VIGUMU SANA KUWA MWADILIFU IKIWA UNAWATUMIKIA MABWANA WAWILI,ATA POTEZA UMAARUFU NA IMANI ALIOJIJENGEA KWA WANANCHI ENDAPO ATA KAZANIA KUNUNULIWA KWA MITAMBO HIYO,JIMBONI KWAKE KUNA TATIZO KUBWA LA UMEME,KMA MBUNGE ANA UWEZO WA KUOMBA MISAADA KATIKA NGO(CHARITY)ZA ULAYA NA MEREKANI YA KASKAZINI,ASAIDIWE USED GENERATOR KWA AJILI YA JIMBO LAKE,NINA AMINI ANGEFANIKIWA,YAMETOKEA HAYO KATIKA NCHI ZA GAMBIA,JIBUTI,NA NCHI NYINGI TU ZINAZO ENDELEA TATIZO YA WABUNGE WETU WENGI WAO WAKO KWA MASLAI BINAFSI NA KUTAFUTA UMARUUFU WAKUJISAFISHIA NJIA NA SIO WABUNIFU KWA AJILI WAKUSAIDIA MAENDELEO YA WAJIRI WAO(WANANCHI),ZITO ALITAKIWA KUZA UZI WA KUSUBIRI MAAMUZI YA KESI KWANZA NDIO LINGEFUATA HILO LA BIASHARA.

  na NGARI, bristol parkway Uk, - 1.03.09 @ 13:42 | #13132

  KAMA BADO KUNA KESI, INAKUAJE TANESCO/SERIKALI BADO MNATAKA KUNUNUA HII MITAMBO?

  UCHAGUZI UNAKARIBIA, CCM HAWANA HELA YA KUTANUA KILA JIMBO!!!

  MWAKA HUU CHANEL ZOTE ZA UFUJAJI ZA CCM LAZIMA ZIFUNGWE.

  DR. IDIRISA NI MUDA WAKO SASA KURUDISHA PESA ZA RADAR NA KURUDI KWENU KIJIJINI.

  na Mzalendo, Arusha, - 1.03.09 @ 13:50 | #13133

  Ni wazi serikali inatumia mabavu. Wacha ituie, wanajua wakipleka bungeni watapita kwa vile wabunge wengi ni wa CCM, hata hivyo uchaguzi unakuja watanzania mnashuhudia maamuzi mabovu bungeni yakiongozwa na wabunge wa CCM, dawa ni moja mwakani tuchague wabunge wengi wa Upinzani kama ilivyokuwa Uingereza mnaona jinsi Waziri kuu Brown anavyoshindwa kuongoza Uingereza, kwa vile wabunge wengi wa upinzani hawakubaliani na upuuzi wa serikali, kuamua mambo kwa ushabiki wa kissisa. Yote hayo watanzania tukiamua, yataisha mwakani TUINGIZE WABUNGE WENGI BUNGENI WA U P I N Z A N I hii ndiyi dawa pekee. CCM na serikali yake inafanya mchezo na maisha ya watz, hapa Kenya mambo ni hayo hayo, na uchaguzi ujao itakuwa mambo kweli kweli, watu wamechoka na uwongo. Watanzania amkeni dawa ni moja, WEKA WAPINZANI WENGI BUNGENI NA MABADILIKO YATAKAUJA. AMINAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!

  na Fr Baptiste Mapunda, Nairobi/Kenya, - 1.03.09 @ 14:24 | #13138

  I'M JUST TRY TO GET MR. ZITTO KABWE INFORMED THAT THE PUBLIC IS WATCHING YOU WITH TWO EYES IN EVERY MOVE YOU ARE TRYING TO MAKE, AND A LOT OF PEOPLE AROUND HAVE BEEN PUT A LOT OF TRUST ON YOU, SO YOU BETTER WATCH YOUR BACK, WHEN YOU COMMENT ON ANYTHING OR WHEN YOU DECIDE TO DEFEND SOMETHING WHICH LOOKS TO BE OF PERSONAL INTEREST. I REMEMBER BACK IN THE DAYS WHEN YOU STARTED TO ARISE, YOU SAID THAT 'YOU WILL NEVER LEAVE US ALONE' NOW IT SEEMS AS IF THINGS NOW ARE TAKING WRONG DIRECTIONS,AND PROBABLY YOU HAVE BEEN ABSORBED AND BE A PART OF THOSE FISADIS, OR THEY ARE TRYING TO USE YOU TO FULFILL THEIR NEEDS BEYOND YOUR KNOWLEDGE,
  MY ADVISE IS THERE IS A LOT OF PEOPLE BEHIND YOU WHO TRUST ON YOU, DON'T LET THEM DOWN JUST BECAUSE OF MONEY, OTHERWISE YOU WILL END UP LOOSING THEM ALL.

  na KILLY - 1.03.09 @ 15:12 | #13145

  Huo umeme DOWN wanaoupigania hadi akina Sala na Zito kwa kisigizio cha kuongezeka kwa mahitaji ya umeme na eti ni masirahi ya taifa, sasa, je na sisi Kigoma tumo katika hayo mahesabu.AU ndio munangalia tu Dar,Arusha; Moshi,dodoma,mwanza nk?.Maana munachefua munaposema nchi isiingie kwenye kiza, wakati sisi tunaishi maisha hayo miaka yote.Na sijasikia Zito wala Salaa kashawahi kusema kigoma kuna giza. Harafu munazidi kupoteza pointi munaposema eti solution ya tatizo ni kununua mitambo iliyotumika ya down, kisa eti ni nafuu!. Munazidi kutudanganya eti ni mipya!Na ninani kaikagua?eti Tanesco(darali).We ZIto kitu kipya na bora kinalazimishwa kununuliwa tena kwa bei nafuu?. Musema kukunua mpya itachukua muda mwingi! kwani mnatoa oder kwanza mitambo itegenezwe kiwandani au munanua iliyotiyari?.Kama biashara fanyeni,lakini musije na mkwara masirahi ya taifa bali ni masirahi ya walewale.Hakuna masirahi ya taifa hapo wala hakuna ufumbuzi wa tatizo hapo.

  na waport, kigoma, - 1.03.09 @ 15:49 | #13147

  Hii inaendana na Maswali Magumu ya leo
  Jumapili.

  Ansbert Ngurumo ninakuandika leo ninapenda Mh. Zitto ayasome pia kwa vile ninachokuandika kina mgusa yeye pia. Yeyote anayeweza kumfikia Zitto mwambie aje kusoma ujumbe wake hapa.

  Ansbert Ngurumo nimekutambua kuwa u- mmoja wa watu wanaofuata falsafa ya ukweli. Nimekutambua kuwa mwanahabari unayeongozwa na hoja za kisayansi na mara nyingi nimekutia moyo hasa pale ninapowaona wakosoaji wenye lengo la kukukatisha tamaa usiendelee na kuitetea nchi yetu kwa kuongozwa na falsafa ya ukweli. Na kwa mbali zaidi- kifalsafa Mungu ni ukweli- kwa hiyo naweza kusema u- mfuasi mwema wa Mungu angalau kwa kusoma maandishi yako.

  Nafurahi umeonesha kuwashaanga wale wanaoitetea Downs- umesema vema kuwa Richmond na Downs ni watoto wa Baba mmoja. Mie nasema ni watoto wa ufisadi dhidi ya nchi yetu. Hapa ndipo namshangaa Zitto ambaye naye naamini huwa anafuata falsafa ya ukweli. Kwa kweli nimeshindwa kumuelewa Zitto ambaye anafahamu kuwa kampuni ya kitapeli na ya kifisadi ya Richmond ilimpasia Downs kazi ya iliyoianzisha. Hivi ni kweli kuwa Zitto haoni Mantiki ya uhusiano wa moja kwa moja kati ya Richmond na Downs? Huu ni upofu na ubishi wa kijinga. Inanikumbusha ****** mmoja katika serikali ya Kikwete aliyetokea kutetea muelekeo wa serikikali kutaka kuvunja katiba. Huyu mtu wa kupuuzwa daima alisema kama una njaa hujali hata kama chakula kinatoka kwa shetani. Nadhani ni Membe. Sasa Zitto anataka kuwa ****** kama Membe eti kwa sababu kutakuwa na tatizo la umeme tununue mitambo ya Downs hata kama Richmond na Downs ni kaka na dada. Kwamba haijalishi nani anatutatulia tatizo la umeme hata kama ni fisadi. This is ridiculous, come on Zitto- je umefikia upeo wako wa kufikiri?. Zitto ninakuheshimu sana na watanzania wengi tunakuamini wewe na Slaa katika mapambano ya ufisadi. Endelea kuongozwa na falsafa ya ukweli acha- upuuzi na ubishi wa kijinga. Unapoona nimetunia muda wangu kukueleza jua nina ujumbe mzito-sikiliza.

  Zitto ninakukumbusha kuwa Barack Hussein Obama alilazimika kuacha kusali kanisa alilokuwa anahudumia pastor wake wa zamani baada ya kutoa matamshi ambao Obama hakuyaunga mkono. Watanzania pamoja na wewe tunaona uhusiano wa moja kwa moja wa Downs na Richmond. Leo bila chembe ya aibu unajitokeza kuitetea Downs. Funguka macho Zitto. Utapeli wa Richmond umeletwa na dharura ya kukosekama kwa umeme. Iweje leo ukose kuona masilahi ya kifisadi ya Downs katika Dharura ileile iliyoleta ufisadi wa Richmond? Zitto jirudi, endelea kuungana na Slaa katika vita vya ufisadi acha upuuzi tutaendelea kukuunga mkono, vita dhidi ya ufisadi bado mbichi.

  Kwako Ansbert kwa kuwa unaandika kisayansi nimekuunga mkono kisayansi na ninakukosoa kisayansi. Baada ya kukuunga mkono katika hoja zako, na japo umekwepa kutaja upuuzi wa Zitto, ninakosoa mtazamo wako karibu na mwisho wa story yako. Umesema wanaotetetea Downs wanafanya siasa na wanaopinga wanafanya siasa. Hapa naona umejichanganya sana. Kwa sababu ingawa ni ngumu kusema lakini ukweli hauongozwi na mapenzi ya kitu fulani. Ukweli hauna mapenzi- unaelekea kule ukweli uliko. Kauli yako kuwa wapinzani na watetezi wa Downs wote wanafanya siasa inatueleza kuwa nawe pia unafanya siasa kupinga Downs. Lakini maelezo yako mengi ya awali na maswali mbalimbali ya kimantiki uliyouliza hayana chembe hata kidogo ya saisa. Ndio maana nasema umepotoka kidogo. Kupinga Downs siyo siasa bali ni kutetea uhai wa taifa letu. Ni kupinga ufisadi, na kupinga ufisadi siyo siasa, inahusu kutetea uhai wa watanzania wanaotaabika na kufa kwa sababu ya ufisadi. Ni kutetea ukweli kuwa kila mtanzania afanye kazi kwa ukweli bila wizi. Na tunapoona mtu, chama au kampuni zinamahusiano ya kifisadi, au watu wake wanafanya ufisadi tunawatosa wote. Kwa hiyo kupinga Downs ni kutetea uhai wa taifa na kutetea Downs ni sawa na kusema hata kama unakaribia kufa basi hata shetani na aje kukuokoa. Downs na Richmond ni ndugu ni mafisadi ni mashetani hatuyataki. Je Zitto unataka kuanza kuwa muumini wa shetani kama Membe? Hapana wewe si mmoja wao rudi kwako kwen

  na Kawala, Niko nyumbani, - 1.03.09 @ 17:12 | #13155

  yaani mimi nawashanga tanesico management mtu unajiita at ni manager wakampuni mhimu kama tanesco halafu unasema mbele ya watu eti mnahitaji kununuwa mitambo ya downson kwa ajili ya kukabiliana ogezeko na mahitaji ya umemw nchini? sasa miaka yote mmekuwa mnafikiria kwamba mihitaji ya umeme yataendelea kuwa tu kwa vigogo wa ccm na ninyi kina rashidi manao kula sahani moja, hela zote zinazo patikana mnatumia kuvijari na kuweka kwenye acount za nje ya nchi badala ya kupanuwa kampuni ili iendana na demand and supply. yaani miaka yote mmeshindwa kuazisha vyazo vigine vya umeme? kama viogozi tulio nao ndio kama hawa wa tenesco basi watanzania tukubali kwamba hatuna elimu kabisa natunao wazani ni wasomi wana vyeti fake. kwani hawezakani ceo wa kampuni kama tenesco anogea matapishi kama haya mbeli ya watu wenye akili halafu aendelea kuongaza shilika mhimu sana kama tanesco. kama tanesco ingekuwa na watu makini sasa hivi tungekuwa tunauwezo wa kuuzia umeme kwa majirani zetu sio kushindwa kuhudumia wananchi wetu.

  na ebita, tanzania , - 1.03.09 @ 17:26 | #13158

  Swala la Dowans ni la CCM kwa sababu wanafuta fedha kwa ajili ya Uchaguzi wa 2010. Dawans ni mali ya ROSHTAM Aziz. Mchezo ule ule uliotumika EPA bado unatumika. Dawans tayari ni mali ya Tanesco vipi mtu anauziwa maLI YAKE. Mtashangaa hata Mh. Zitto haoni hili kwani amekwishalipwa fedha nyingi sana. Kama kuna mbunge amekwisha pata aibu hapa Tanzania, Mh. Zitto atakuwa wa kwanza. POLE SANA MH. ZITTO kwa kutusaliti, tuliweka matumaini makubwa sana kwako. Kama kuna mtu anafaa kupigwa mawe na kufa hapohapo ni Roshtam Aziz kwa sababu hapa Tanzania hakuna mtu, polisi wala court ianaweza kushughulikia Roshtam isipokuwa instant justice.
  Mungu aibariki Tanzania.

  na Gati, dsm/tanzania, - 2.03.09 @ 01:52 | #13180

  Maslahi ya Taifa yanatamka hapa kwamba Ni Busara zaidi kwa Serikali kutafuta Mitambo Mipya na itakayo tumika kwa kipindi kirefu zaidi na ikiwezekana mitambo ambayo itakwenda sambamba na teknolojia ya kisasa zaidi,KULIKO,kununua Mitambo ya Umeme iliyo CHAKAVU na ambayo tayari huko nyuma ilishahusishwa na Kashfa baina ya waletaji wa mitambo hiyo na serikali yenyewe hadi kusababisha baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali kulazimika kujiuzulu nyadhifa zao!Huo ndio Uzalendo na kulinda maslahi ya taifa kwa faida ya vizazi vijavyo!Lakini siyo kujenga mazingira tata ya kuhalalisha ununuzi wa mitambo hiyo chakavu.Absolutely Not.Iwapo Dowans wataiuza mitambo hiyo katika mnada wa hadhara,na kila mdau atashiriki katika mnada huo wa wazi,hapo pia itatazamwa iwapo Bei itakayo tamkwa na Dalali wa Mnada ina lingana na thamani halisi ya uchakavu wa mitambo hiyo.Kuinunua mitambo hiyo yenye harufu ya kashfa na ufisadi na serikali yenyewe kuhusika katika mchakato huo,KUTAHALALISHA MAOVU NA MAPUNGUFU YOTE yaliokwisha fanyika huko nyuma NA KUWASAFISHA VIONGOZI WOTE WALIOHUSISHWA NA KADHIA HIYO NA KULAZIMIKA KUJIUZULU ili wawe safi kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi zijazo!Jambo hilo tumeshalistukia,haramu lisifanyike kwa maslahi ya Taifa!Hata kama Taifa litalazimika kuingia katika msimu wa Giza kwa kukosa umeme wa kutosha,bora iwe hivyo,watanzania tumesha zoea shida na taabu.ISITOSHE NI ASILIMIA 22%TU YA WATANZANIA WOTE NDIO WANAOPATA UMEME KWA HIVI SASA!Hawa asilimia 22% ya watanzania tuko tayari kula nyasi kuliko kuona ujinga mwingine tena wa kuwasafisha viongozi waliokumbwa na kadhia hii ukifanyika kwa kisingizio cha "kutanguliza maslahi ya kitaifa".Lazima tutambue kwamba kulazimisha kitendo kingine chochote kiovu kama hichi kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi kutalitumbukiza Taifa hili katika mpasuko mkubwa zaidi wa kimaslahi na mshikamano wa kitaifa.MNALOTAKA KULIFANYA KINA zitto NA sasa Slaa tumeshaling'amua.Acheni,litawavunjia heshima yenu na kuwapotezea kabisa umaarufu wa kisiasa mliokwisha ujenga.Acheni Kabisa huo Ujinga!We already know what you intend to do!Mtaponzwa na hiyo Tamaa ya kutaka Ukubwa kwa gharama yoyote!Mlianza vizuri,tulieni,tulizeni akili zenu,kila mtanzania kesha tambua nini ambacho mmekusudia kufanya na kwa maslahi ya nani!Very Unfortunate to you Zitto and Slaa!

  na kurutamatata, kariakoo,Dsm,tanzania, - 2.03.09 @ 09:17 | #13201

  Inasemekana Zito amelambishwa asali na mafisadi wa nchi hii hasa wa kwenye sekta ya nishati na madini.
  Wapo wanaodai siku hizi anatembelea gari la nguvu aina ya HAMMERS ambalo alilipata baada ya kupewa kitita kinono hasa wakati wa kamati ya madini chini ya Jaji Bomani.
  Japo hatujathibitisha madai hayo lakini mwenendo wake hivi karibuni umekuwa wa kutilia mashaka makubwa. Leo yeye ni shabiki mkubwa wa ununuzi wa mitambo ya Dowans ambayo wapo wanaodai itamrudishia mbunge mmoja nguvu alizopoteza baada ya kuandamwa na kashfa. Isije ikawa mbunge huyo nae ameanza ukaribu na bwana Zito.
  Zito tulikuamini sana, lakini historia inaonyesha wabunge wa Kigoma hawakawii kubadili misimamo kama kaka yako Walid Amani Kaborou
  Yetu macho!!!

  na Wa kusikitika, London Uk, - 2.03.09 @ 10:34 | #13206

  Zitto ndani ya kapu la mafisadi.Zitto Kabwe ni mropokaji mzuri sana kama mtakumbuka michango ya Zitto kwene kikao cha bunge kuhusiana na EAC fast track.Huyu jamaa aliitia aibu kambi ya upinzani kwa kutoa michango ya ovyo kupitiliza.

  na kweka, Tabora, - 2.03.09 @ 10:54 | #13208

  Chadema mwambieni Zitto asipende kukumbilia hoja bila kuzifanyia utafiti wa kutosha.Zitto asifikiri watanzania ni wavivu wakufikiri kama alivyokuwa akisemayule ***** wa Kiwara.
  Watanzania ni watu makini ukitaka kutuibia tunajua kwa hili tunajua tunataka kuibiwa mchana kweupe mbaya ni pale kijana wetu tuliye mtegemea sana ameamua kutugeuga na kuungana na mafisadi.

  na Juma Kombo, Lindi, - 2.03.09 @ 10:01 | #13210

  Mitambo hiyo iliwekwa rehani. TANESCO imeshinda kesi.Ni mali ya serikali kupitia TANESCO.

  Kama Dowans wangeshinda kesi serikali ingeilipa TANESCO.Sasa TANESCO imeshinda mbona ubabaishaji?!

  Hiki ni kiini macho tu.WEZI wanajuwa tumeshinda kesi na mitambo ni yetu.

  Hapa ndipo ufisadi mpya unaanza.Wananchi tusiwe wajinga tena
  ,kama suala la kukiika sheria ya manunuzi lilisababisha Waziri mkuu kujiuzulu je leo sio muhimu tena.
  Hatuwezi kuvunja sheria kwa ujanja uleule eti kuna hali mbaya inakuja.
  Kesho na kesho kutwa hii ni precedent mbaya kabisa.

  Rashid haaminiki na hajakanusha vipi Vijisent alimwekea kwenye akaunt yake $600,000.

  Je fisadi wanaanzisha kula nyingine tukiangalia tu.

  Nawaunga mkono wanaopinga mpango huu kwani ni kuvunja sheria ya nchi.

  Nini maana ya Bunge kusimamia serikali?
  Zito na Slaa acheni kuwa vigeugeu mnaingizwa kwenye mkenge ,wabuge wa ccm watawamaliza mbele ya macho ya wananchi.
  MTEGO MKUBWA HUU.MMEKWISHA!!

  Baadaye suala hili litakapopelekwa bungeni mtaonekana vituko.Kumbukeni wananchi hatutaki harufu yoyote ya ufisadi tena.Mafisadi hawana chama wanaweza kuwa Slaa,Zito na hasa Zito tunaona nyendo zake hazieleweki.

  TUSUBIRI TU.UKELI UTADHIHIRIKA.


  Kutoka Tanzania daima
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama Zitto kaingizwa mkenge na MAFISADI juu ya DOWANS sintaoina ajabu kwani hao ndio wabunge wa Kigoma; hata Kaborou alianza pole pole hivyo hivyo. Kitu kimoja Zitto atambue kuwa sisi sio mabwege tena na wala umaarufu usimleweshe, yeye bado kijana mdogo asijeakaharibikiwa angali anachipua!!
   
Loading...