fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,065
Sijui hata lina maana gani katika maisha, ni jina tu sio lazima liwa na maana sana
Kuna mijadala mingi imepita humu JF juu ya ujio wa Tanganyika kufuatia Rasmi ya pili ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 2013,lakini katika mijadala yote sijaona ikitoa tafsiri na asili ya hili neno Tanganyika zaidi ya baadhi ya members kusema kuwa asili ya neno Tanganyika ni Tanga bila ya kusema maana ya neno lenyewe.Hata hivyo nimeshawahi kusoma mahali kuwa asili ya neno Tanganyika ni Kigoma, (Lake Tanganyika),na neno hili limetokana na aina flani ya samaki (electric eels) anayeitwa NTANGA na samaki huyu huwa anatoa umeme na anapatikana ziwa Tanganyika hence neno Tanganyika.Kuna wengine wakisema kuwa neno hili asili yake ni Kigoma hukohuko likiwa na maana ya makutano ya watu yaliyokuwa yakifanyika ziwani hence Tanganyika yaani kuchanganyika.
Sisi wengine watu wa bara na kwa lugha ya kwetu neno NYIKA hata hivyo lina maana pori ,sasa lilivyokuja kuunganishwa na Tanga hapa ndo kitendawili kingine. Naomba wadau wenye kujua maana na asili ya hili neno watuelimishe tafadhali.
Tanga means first
Nyika means counrty
TangaNyika means First country
TANGA .......ILIKUWA NDIO NJIA YAO YA KUINGILIA KATIKA ENEO HILI LA ARDHI, AMBALO LIMETAWANYIKA MPAKA KIGOMA, SASA BAADA YA MAENEO MENGINE YOTE KUPEWA MAJINA LIKAWA LINATAMBULISHWA KWA KI SIRI (PENGINE KWA SASABU WANAZOZIJUA WAO......(LABDA MALI ZILIZOMO N.K.)........1.UTAMBULISHO WA KWANZA ULIKUWA NI KWAMBA KIPANDE HICHO CHA ARDHI KIMEZUNGUKWA NA MAZIWA (LAKES).....2.LAND MARK ZAO ZILIKUWA BAADA YA KUINGIA TANGA......KWA UPANDE WA KASKAZINI WALIKUBALI MWISHO WAKE UWE NI MLIMA KILIMANARO NA KUANZIA HAPO UNAENDELEA MBELE MPAKA UKUTE ZIWA LINGINE KUBWA(VICTORIA).3.PIA WALIKUBALIANA BAADA YA KUINGIA TANGA KWA UPANDE WA KUSINI UKIAMBA AMBAA NA BAHARI MWISHO WAKE UWE NI MTO MKUBWA (RUVUMA),TENA UKIUFUATA MWISHO WAKE UTAKUTA ZIWA (NYASA/MALAWI).....HIVYO BASI UPANDE WA KASKAZINI WALIPATA LAND MARK MBILI KWANZA MLIMA PILI ZIWA...NA UPANDE WA KUSINI WALIPATA LAND MARK MBILI KWANZA MTO THEN ZIWA....SASA KIPANDE CHA KATI CHOOTE KIKAITWA NYIKA...NYIKA .....NA MWISHO WA NYIKA HIYO...PIA KUNA ZIWA..NDIO KISA NA MAANA YA ZIWA HILO KUITWA TANGANYIKA......NASIKITIKA DOCUMENT HIZI HAZIKUMFIKIA MWL.JK.NYERERE MANAKE HATA YEYE ALIKUWA ANATAFUTA ASILI YA NENO TANGANYIKA...........to be continued......Hili Tanganyika lililetwa na wajerumani kwa hiyo lazima kutakua na maelezo chanzo cha jina hili. Nilivyosikia kabla ni kuwa jina ni mjumuisho wa mji wa Tanga na Nyika iliozunguka kuliko upeo wa macho - sijui kama ni kweli.
Kuna mijadala mingi imepita humu JF juu ya ujio wa Tanganyika kufuatia Rasmi ya pili ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 2013,lakini katika mijadala yote sijaona ikitoa tafsiri na asili ya hili neno Tanganyika zaidi ya baadhi ya members kusema kuwa asili ya neno Tanganyika ni Tanga bila ya kusema maana ya neno lenyewe.Hata hivyo nimeshawahi kusoma mahali kuwa asili ya neno Tanganyika ni Kigoma, (Lake Tanganyika),na neno hili limetokana na aina flani ya samaki (electric eels) anayeitwa NTANGA na samaki huyu huwa anatoa umeme na anapatikana ziwa Tanganyika hence neno Tanganyika.Kuna wengine wakisema kuwa neno hili asili yake ni Kigoma hukohuko likiwa na maana ya makutano ya watu yaliyokuwa yakifanyika ziwani hence Tanganyika yaani kuchanganyika.
Sisi wengine watu wa bara na kwa lugha ya kwetu neno NYIKA hata hivyo lina maana pori ,sasa lilivyokuja kuunganishwa na Tanga hapa ndo kitendawili kingine. Naomba wadau wenye kujua maana na asili ya hili neno watuelimishe tafadhali.
Kwa kisambaa na kibondei (makabila ya Tanga) mnyika ni mtu wakuja(asie mwenyeji). Na hili neno lilitumika zaidi kwa waliotoka bara kuja kulima mkonge. Tanga ni lile kama shuka hivi linalotumika kwenye madau(mitumbwi) kusafirisha chombo kwa msaada wa upepo. Pia tanga ina maana ya shughuli za msiba. Mfano, kuinua Tanga ni kumaliza msiba... Ni mtazamo wangu, malizieni.