Nini amekifanya Mbunge wako jimboni kwako toka 2010 hadi sasa?

Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,481
564
Nimesoma thread iliyoandikwa kuwa " Filikunjombe afanya makubwa Ludewa " hii imekuja kutokana na Mbuge huyu kijana kutoa gari la kubebea wagonjwa la Tsh mil 90.

Naomba tuangalie kwa kina Wabunge wengine wamefanya nini tangu walipo chaguliwa hadi sasa ili kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa ni pamoja na kutimiza baadhi ya ahadi alizo ahidi kipindi cha kampeni.

Mfano SUGU - Mbeya Mjini ( CHADEMA), Barabara nyingi za mitaani zina wekwa changalawe chini ya uongozi wake

Filikunjombe - Ludewa (CCM), Ametoa gari la wagonjwa na kuahidi kutoa zaidi kila kata ikiwa ni pamoja na kufuatilia ahadi ya Mh. Rais

NOTE: Hii itasaidiakujua nani hawajibiki kwa kutimiza ahadi zake kwa hiyo atapoteza nafasi yake 2015
Kumbuka siku njema huonekana tangu asubuhi

Naomba kuwasilisha
 
Mkuu nimesoma leo kwenye gazeti kwamba Filikunjombe amewaomba wananchi wa Ludewa wampatie eneo awajengee uwanja wa ndege wa kisasa kwa pesa zake mwenyewe.

Mimi mbunge wangu alichofanya hadi sasa ni kuwa mahiri wa kuomba miongozo bungeni na kupiga makelele ili spika ampe nafasi ya kuomba mwongozo juu ya mwongozo.
 
mi mbunge wangu anang'ara kwenye vyombo vya habari hasa magazeti wakimuonyesha hakiwa amelala mjengoni na kutililisha udenda.
 
Mimi mbunge wangu amenisaidia kunifanya niichukie Magwanda kama upupu.
 
mi mbunge wangu anang'ara kwenye vyombo vya habari hasa magazeti wakimuonyesha hakiwa amelala mjengoni na kutililisha udenda.
Mbunge wangu ni Prof. Maji Marefu, tangu amekuwa mbunge katusaidia sana kupunguza wanga na wachawi hapa jimboni kwetu.
 
Mbunge wangu Azzan Zungu, kahakikisha kuwa Ilala inaendelea kuwa wilaya tajiri katika Tanzania.
 
Mbunge wangu ni Lusinde. Kazi yake ni kuropoka tu bila mpangilio na hajui kuisoma audience. Anaropoka hovyo hata mahali walipo watu wa umri wa baba yake
 
Mkuu nimesoma leo kwenye gazeti kwamba Filikunjombe amewaomba wananchi wa Ludewa wampatie eneo awajengee uwanja wa ndege wa kisasa kwa pesa zake mwenyewe.

Mimi mbunge wangu alichofanya hadi sasa ni kuwa mahiri wa kuomba miongozo bungeni na kupiga makelele ili spika ampe nafasi ya kuomba mwongozo juu ya mwongozo.

kanuni za bunge zinakataza mbunge kuomba mwongozo?
 
Mbunge wangu (Mtemvu) hakosi shughuli hapa temeke. Hakosi graduation za tae kwon doo. Thats all we want from him. Mengine tutafanya wenyewe.
Tunataka kumwandikia mapendekezo juu ya muswaada wa kuwasaidia walioathirika na bwimbwi, linatuua huku jamani!
 
Mbunge wangu Azzan Zungu, kahakikisha kuwa Ilala inaendelea kuwa wilaya tajiri katika Tanzania.

ilala?! Kwa resources zipi? Mi naona anajitahidi kuifanya ilala iwe na machinga wengi kuliko wilaya yyte tanzania. Wilaya tajiri iache kuwa kahama iwe ilala! You must be not serious
 
ilala?! Kwa resources zipi? Mi naona anajitahidi kuifanya ilala iwe na machinga wengi kuliko wilaya yyte tanzania. Wilaya tajiri iache kuwa kahama iwe ilala! You must be not serious
Lol... mzee kahama hata asilimia moja ya ilala haifikii!
 
Hiyo migodi inaingizia taifa/wanakahama kiasi gani kwa mwaka?
Linganisha GDP ya ilala na kahama. Ilala ndio financial centre ya TZ kama ilivyo manhattan district,
Manhattan peke yake ni ya ishirini na moja duniani kwa GDP.
Hizo dhahabu sio zenu. Au hujui hilo?
 
Kahama iko juu sana kuliko Ilala. Kuna madini ya kumwaga kule
Hiyo ni sawa na kusema tuna njaa ila ardhi yetu ina rutuba.
Au, tuna shida ya umeme ila tuna makaa ya mawe.
Huwezi kujiita tajiri kwa sababuuna resources.Fedha zote za migodi zinakuwa traded wal street na London stock exchange.
 
Mbunge wangu Jeremia Sumari(ccm) arumeru toka alipochaguliwa hajawahi fika bungeni. hata kuapishwa bado ni mgonjwa.
 
ilala?! Kwa resources zipi? Mi naona anajitahidi kuifanya ilala iwe na machinga wengi kuliko wilaya yyte tanzania. Wilaya tajiri iache kuwa kahama iwe ilala! You must be not serious

Asiyejuwa maana haambiwi maana, Kahama bado kwa sasa, wachimbaji wanalipa mtaji wao, haijaanza kuwa na faida. Ilala is the biggest trading Market in East Africa, kwa kukujuza tu.
 
Mie sijamwonapo Jimboni tangu Zilipomalizka kampeni.Hii ndio Njombe Kaskazini kwa Deo Sanga (Jah People)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom