Nini amekifanya Mbunge wako jimboni kwako toka 2010 hadi sasa?

Mbunge wangu Jeremia Sumari(ccm) arumeru toka alipochaguliwa hajawahi fika bungeni. hata kuapishwa bado ni mgonjwa.[/QUOTE

pole sana,
hivi sheria zinasemaje ktk hili maana muwakilishi wa wananchi ni mgonjwa kwa muda mrefu sasa
wanasheria tusaidieni hapa
 
Sheria haiweki bayana juu ya ugonjwa wa muda mrefu ila anaweza kutumia busara na kujiuzulu. Lakini jinsi miafrika inavyopenda uongozi uamuzi wa kujiuluzulu ni wa mwisho kabisa kwao. Mtu yuko radhi azikwe na ubunge au uwaziri wake.
 
Mbunge wangu Jeremia Sumari(ccm) arumeru toka alipochaguliwa hajawahi fika bungeni. hata kuapishwa bado ni mgonjwa.

Huyu Mzee baada ya kuona hataweza kumshinda Nasar Joshua uchaguzi uliopita akaweka mipango iliyofanikiwa ya kuchakachua kura na kutangazwa mshindi. Alipokamilisha mipango hiyo haramu akaanza kuugua kabla hata ya uchaguzi kutokana na laana ya wameru walioapa kwamba akichakachua kura zao hatatia mguu dodoma!
Hadi leo yupo mahututi kitandani hata kuapishwa bado akitafunwa na kansa ya ubongo. From financial deputy minister to the bed for a year! Poor him!
R. I. P broda!
 
Mkuu nimesoma leo kwenye gazeti kwamba Filikunjombe amewaomba wananchi wa Ludewa wampatie eneo awajengee uwanja wa ndege wa kisasa kwa pesa zake mwenyewe.

Mimi mbunge wangu alichofanya hadi sasa ni kuwa mahiri wa kuomba miongozo bungeni na kupiga makelele ili spika ampe nafasi ya kuomba mwongozo juu ya mwongozo.

Mbunge gani huyo au unaona aibu kumtaja?
 
Mbunge wangu Azzan Zungu, kahakikisha kuwa Ilala inaendelea kuwa wilaya tajiri katika Tanzania.

Kivipi?
be a great thinker na utuambie kafanya nini kinacho ifanya au kinacho changia
Ilala kuwa tajiri,.... na vipi wananchi wake ?
Amefanya nini kuhakikisha utajiri wa wilaya yake una nufaisha wananchi wa ilala?
 
Nimesoma thread iliyoandikwa kuwa " Filikunjombe afanya makubwa Ludewa " hii imekuja kutokana na Mbuge huyu kijana kutoa gari la kubebea wagonjwa la Tsh mil 90.

Naomba tuangalie kwa kina Wabunge wengine wamefanya nini tangu walipo chaguliwa hadi sasa ili kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa ni pamoja na kutimiza baadhi ya ahadi alizo ahidi kipindi cha kampeni.

Mfano SUGU - Mbeya Mjini ( CHADEMA), Barabara nyingi za mitaani zina wekwa changalawe chini ya uongozi wake

Filikunjombe - Ludewa (CCM), Ametoa gari la wagonjwa na kuahidi kutoa zaidi kila kata ikiwa ni pamoja na kufuatilia ahadi ya Mh. Rais

NOTE: Hii itasaidiakujua nani hawajibiki kwa kutimiza ahadi zake kwa hiyo atapoteza nafasi yake 2015
Kumbuka siku njema huonekana tangu asubuhi

Naomba kuwasilisha

Wow,umetoa mifano mizuri sana.
Kwa mfano sugu sikuwahi dhani anafanya chochote.Good job
 
Asiyejuwa maana haambiwi maana, Kahama bado kwa sasa, wachimbaji wanalipa mtaji wao, haijaanza kuwa na faida. Ilala is the biggest trading Market in East Africa, kwa kukujuza tu.

Kwa hiyo zungu ndo kafanya iwe "the biggest trading market"?
kama ndio how?
 
Mbunge wangu wa Arusha. Mh. Godbless Lema amefanikiwa kuanzisha mfuko wa elimu ambapo mwaka huu watoto zaidi ya 100 (mia moja) wanaotoka kwenye familia zisizokuwa na uwezo wanasomeshwa sekondari na mfuko huo. Ukarabati kwenye wodi za hosp ya mkoa unamalizika. Hatua za awali za ujenzi wa "mlimani city" maarufu kama "Machinga complex" hapa Arusha zimeanza.
Kimsingi anaendelea vzuri na naamini atatufikisha mbali kimaendeleo!
 
Nakwenda Kesho kukagua madaraja na shule kama ajafanya lolote tutamtoa speed kwani sisi wananchi ndio tuliomwajiri.
 
Sheria haiweki bayana juu ya ugonjwa wa muda mrefu ila anaweza kutumia busara na kujiuzulu. Lakini jinsi miafrika inavyopenda uongozi uamuzi wa kujiuluzulu ni wa mwisho kabisa kwao. Mtu yuko radhi azikwe na ubunge au uwaziri wake.

Wabunge wetu wangekua wanagombea
kwa ajili ya kutumikia wananchi,sumari angesha jiuzuru.

Lakini kwakua wanagombea ili kutibu njaa zao,ajiuzuru ili nani amsifu?
Atakula nini mda huu ni mgonjwa?

Ndo maana pamoja na mapungufu yake yote namsifu rostam kwa kujiuzuru,hakuna mbunge
mwingine anaweza fanya hivo.
 
Jimboni kwetu kuna wa wabunge watatu wawili hawaendi Bungeni ni Joseph Tadayo wa Trust Mark atorney na Cleopa David Msuya hawaendi Bungeni lakini wanafanya kazi zilizomshinda Maghembe. Huyu anayekwenda Bungeni yeye ni Majungu, Ushirikina tu hamna kitu
 
Mbunge wangu wa Arusha. Mh. Godbless Lema amefanikiwa kuanzisha mfuko wa elimu ambapo mwaka huu watoto zaidi ya 100 (mia moja) wanaotoka kwenye familia zisizokuwa na uwezo wanasomeshwa sekondari na mfuko huo. Ukarabati kwenye wodi za hosp ya mkoa unamalizika. Hatua za awali za ujenzi wa "mlimani city" maarufu kama "Machinga complex" hapa Arusha zimeanza.
Kimsingi anaendelea vzuri na naamini atatufikisha mbali kimaendeleo!

Lile daraja la Mt. Meru hotel kupandisha Sekei, Ni Lema au Medeye, maana ilikuaga bonge ya kero kipindi cha mvua.
 
Mbunge wangu Lema, kajenga Machinga Complex mbili.
Na kajenga (Skyover) katikati ya jiji la Arusha
 
Mfano SUGU - Mbeya Mjini ( CHADEMA), Barabara nyingi za mitaani zina wekwa changalawe chini ya uongozi wake

Hapo kwa Sugu naona umechapia, nilikuwa Mbeya kwa mwezi mzima ulipopita, na sijaona barabara inayowekwa changarawe, zaidi ya vifusi vya hapa na pale kama ilivyo kawaida ya Halmashauri ya Jiji.

...ILA kuna mradi mkubwa wa kupitia Tanzania Cities Project (TSCP) unaofadhiriwa na World Bank wa kujenga barabara za mitaani mjini Mbeya kwa kiwango cha lami. Mradi huu ulisainiwa mwezi September mwaka 2010, hivyo Sugu hana mkono wowote kwenye uwepo kwa mradi huu.

Pia kuna mradi mkubwa wa usambazaji wa mtandao wa maji mjini Mbeya kwa kupitia Wizara ya Maji kwa ufadhiri wa European Union ( http://www.fwt.fichtner.de/php/main...t_id/2/idc1/148/z1/4/map/1/sprache/e/li/0re_s), mradi huu nao ulianza kabla ya uchaguzi uliopita.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom