Ningeweza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza katika bidhaa mpya zenye thamani kwa sasa duniani

HiVi unadhani hakuna bunifu nzuri kwenye hii nchii .... Kunabunifu za kipekee na kama zitatiliwa mkazo basi hii nchi ingekuwa mbali Sana tatizo siasa kila mahali pia secta binafsi azipewi kipaombele hii nchi kila kitu ni serikali serikali...hii inasababisha mambo mengi na bunifu nyingi nzuri kukwama.

kusema ni rahisi sana, ni hulka ya binadam
 
Ni rahisi kuwatupia Wananchi mzigo kwa sababu hata ninyi wenye Mamlaka hamjui cha kufanya.

Hivi unajua ubunifu una gharama kabla kuwa bidhaa ya kuuza? na tena kuna gharama zenye nafasi kubwa ya kupotea bila ubunifu kufikia matarajio.

Ndio yanahitajika mazingira wezeshi na ni Serikali pekee wenye nafasi hiyo, taasisi binafsi zaweza kuwepo lakini kwao ni uchaguzi zaidi ukilinganisha kama kungekuwa na sera nzuri za Serikali kuthamini ubunifu na Wabunifu.

Si rahisi kujua hili kama sio sehemu ya Wabunifu/Wagunduzi.

Mtu/Watu wanapobuni/kugundua kifaa au bidhaa yenye tija na uhitaji basi Mbunifu afikiwe na awezeshwe ili aboreshe kifaa/bidhaa husika...ndivyo wanavyofanya wenzetu hizi bidhaa tunazoziona zinafurika huku.

Ukiangalia Wenzetu huko nje Mtu anayetengenza kifaa uwani kwake bado utastaajabu mashine na malighafi alizonazo ambazo kiukweli Mtanzania wa kawaida ni vigumu kuwa navyo hata kama ana wazo linalofanania hivyohivyo.

Ulichoongea ni tafauti kabisa, watu wengi wanaanza kwa shida hakuna sehem duniani unakuta mazingira malaini ya kunyoosha tu wazo, hata google wenyewe walianza kwenye gerej kwenye nchi yenye uchumi mkubwa sana duniani, tafauti yake ni nn na uku??? Lawama ni nyingi sana kwa serikali lakini ukweli wa maisha yetu ni rahisi kuyajua, angalia mtu aliemaliza chuo kilichopo cha kwanza kichwan kwake ni nn alafu uje kupitia comment yako tena, na wale wote tunaowaita wabunifu tanzania angalia nn wamefanikisha, ni hata aibu kusema ni ubunifu, nn tunaweza jivunia? Ukiachana na MPEMBA ambae huyu ndo mbunifu pekee nchini nnaemjua mtaje mwingine
 
kikubwa zaidi ni kuwekeza kikubwa kwenye elimu, hizo ulizotaja ni mapendekezo yako ila uchumi imara unatokana na wananchi wenyewe, ubunifu wao na umbali wanaoweza kwenda katika uchumi wa dunia kwa jumla, sasa shida uko kila mtu anawaza ajira na hata hio ajira anaiwazia kutoka serikalini kujaribu nchi zingine hawataki hata private sector za apa apa hawataki, kilio serikalini
Shida ni ccm wamejaa wapumbavu wasio na elimu Wala upeo, kipaumbele chenu ni uchawi tu na uroho wa madaraka
 
Ulichoongea ni tafauti kabisa, watu wengi wanaanza kwa shida hakuna sehem duniani unakuta mazingira malaini ya kunyoosha tu wazo, hata google wenyewe walianza kwenye gerej kwenye nchi yenye uchumi mkubwa sana duniani, tafauti yake ni nn na uku??? Lawama ni nyingi sana kwa serikali lakini ukweli wa maisha yetu ni rahisi kuyajua, angalia mtu aliemaliza chuo kilichopo cha kwanza kichwan kwake ni nn alafu uje kupitia comment yako tena, na wale wote tunaowaita wabunifu tanzania angalia nn wamefanikisha, ni hata aibu kusema ni ubunifu, nn tunaweza jivunia? Ukiachana na MPEMBA ambae huyu ndo mbunifu pekee nchini nnaemjua mtaje mwingine
Huenda ubunifu ni dhana pana na wewe upo kwenye kona nyingine kabisa, na labda huenda tunazungumzia maeneo tofauti ya ubunifu.

Kwanza ukumbuke hatupo kwenye Ulimwengu sawa haswa kwa karne tuliyopo ambapo mambo sasa yanavyokwenda kwa kasi...ubunifu wowote usioweza kushindana sokoni hauna maana, hauna tija...yaani huwezi kubuni kifaa cha kusafishia nyumba ukakiweka sokoni ambako tayari kuna kifaa kama hicho na tena kimerahisishwa zaidi na Muuzaji anauza bei robo ya gharama zako za kukizalisha.

Mimi huwa nafuatilia sana bunifu mbalimbali zinazofanywa na Mtu wa kawaida tena uwani kwake.....Mimi huwa siamini kwamba kuna anachoweza kufikiria Binaadamu mwingine mahali na sisi Watu milioni60 tukakosa kabisa mwenye mawazo ya kibunifu kama hayo au yanayokaribiana na hayo.

Huwezi kufananisha Mwananchi mmoja mmoja wa huku kwetu na yule wa nchi zilizokwishaendelea...huku kwetu Mkulima tu wa kawaida akiwa na wazo la kifaa cha kupukuchua mahindi atapitia safari ndefu sana kukamilisha kazi yake na au hata akaishia njiani....ilihali Mkulima Mwenzake kama huyo aliyepo Urusi utaona tayari uwani kwake ana kifaa cha kukatia au kutobolea chuma kwa vipimo anavyokusudia.

Hivi hujaona sokoni kuna Majembe na Mapanga kutoka China? sasa je hatuna uwezo wa kutengeneza walau hata hizo zana na kutosheleza soko? wako wapi wale Wapare waliokuwa wameshapiga hatua kwenye ufuaji wa chuma tangu karne ya 19? kwa hiyo kwako huoni uhitaji wa sera na utashi wa Serikali kuona Wabunifu wanafika mbali...kwamba wale Wapare walipaswa kupambana wao wenyewe mpaka kufikia kumiliki Viwanda vikubwa vya kufua vyuma huku serikali ikiachia zana kama hizo kutoka China kujaa sokoni? Mpare angefanyaje?.

Kwa hizi nchi zetu Serikali isijivue lawama, kwa kuwa tu hawajui la kufanya ambapo huamua kukimbilia shortcut.
 
Una mawazo mazuri kaka ila nakusihi usiweke matumaini yako kwa serikali kaka , wew buni bidhaa nzuri ingia sokoni ukitegemea serikali ipige marufuku majembe toka china ili wew ndo uuze yako jua kabisa unafeli na lazima utawaumiza wengi ie wanunuaji kwa kuwapa either bei kubwa au poor standard product

Mbna soda zinaletwa toka nje na bado kina Mo na SSB wanapambana ? Mbona bia zinaletwa toka nje ila TBL bado wanakomaa hawalilii kuzuiwa kwa bidhaa za nje ?
Kikubwa tufocus as individual kuliko kusubiri serikali ije ifanye hiki na kile, mfano wew hapo anzisha kiwanda cha majembe mazuri kwa bei nzuri ingia sokon ukawatoe wachina
 
Bado sioni kwa nini Nchi Masikini hizi tuziache serikali zetu kubaki kama dubwana fulani tu linalopaswa kukaa upande mmoja na kututazama Wananchi wengine kama Waburudishaji.

Lazima tutengeneze serikali zinazokuwa sehemu ya Wananchi, kama Serikali inasimama na kusema hatutaki kandambili za Nje basi na msimamo wa Wananchi unakuwa hivyo kwa kutengeneza na kutumia za kwetu....mazingira mengine wala hayahitaji kelele ni vitendo tu tunaona mabadiliko.

Ubunifu wa Masikini una mazingira magumu haswa kwa zama hizi za ushindani....nimekupa mfano hapo wa Mkulima wa Urusi ambaye tayari ana umeme na mashine ya kutoboa na kukata chuma uwani kwake...kwa mazingira kama hayo yeye atabuni kifaa, atatengeneza na hata akikosea atarudia mara kadhaa mpaka kitokee...huyu wa kwetu akusanye vyuma na kukata kwa msumeno alafu bado tutarajie bidhaa imara kama ile ya Mwenzake?.

Wabunifu wapo ila watahitaji mkono wa hali, mali na sera za Serikali kuboresha bunifu zao zikidhi haja ya soko....au la Taasisi kama Sido, Temdo, Tirdo n.k wanunue mawazo ya Mtu mmoja mmoja wayaendeleze kwa nyenzo zao.
 
Kama kichwa cha bandiko hili kinavyojieleza kwamba.

"Ningeweza kupandisha uchumi wa Tanzania kwa kuwekeza katika bidhaa mpya zenye thamani kwa sasa duniani".

Ndugu zangu,
Naomba nianze kwa kueleza sababu moja inayofanya Gross Domestic Product per capital yetu kuwa ndogo.

Gross Domestic Product (GDP) yetu per capital ni ndogo mnoo na hii ni kwasababu hatuzalishi bidhaa mpya ambazo zina thamani kwasasa bado tupo na bidhaa za zamani zilezile.

Hebu Tujiongeze tuanze kuzalisha bidhaa mpya ambazo zinahitajika na mataifa mbalimbali hizi ndio zenye thamani kubwa kwa sasa.

Tuzalishe bidhaa zifuatazo
1. Natural Gas, LNG:

2. Kemikali: Kemikali zinazotokana na gesi mfano ammonia, Sulphuric acid, mbolea mbalimbali, methanol, n.k:

3. Gesi ya Helium. Hii gesi ina dili kuliko gesi zote duniani kwasasa.

4. Madini ya Lithium kwaajili ya betri za magari ya umeme.

5. Madini ya Nickel

6. Madini Cobalt

7. Madini ya platinum

8. Madini ya Chromium

9. Madini ya Manganes

10. Madini ya Copper

11. Nishati ya umeme (tuzalishe nishati kwa wingi tuwezavyo tuuze kwenye mataifa mbalimbali).

Tukiuza bidhaa hizo zenye thamani tutapata fedha nyingi zitakuza GDP yetu, mwishowe tutajikuta tunaacha kutoza kodi. Lakini hatuwezi kuacha kutoza kodi kwasasa kwasababu hatuna vyanzo mbadala vya mapato ya uhakika ya kuaminika ambayo yanaweza kufinance miradi yetu ya maendeleo na huduma za jamii katika taifa letu.

Hivyo tuweke mikakati huko kwenye bidhaa mpya. Lakini ili kulifanikisha hilo rasilimali watu ndio nyenzo muhimu kwenye kuzalisha hizo bidha mpya.

Tuna wataalam wa madini, wataalam wa mafuta na gesi tuwatumie ili kuwezesha uchumi wetu. Leo tunakimbizana na kodi za miamala ya simu ni kwasababu hatuna uwezo wa kuzigeuza rasilimali zetu kuwa pesa. Tuna madini, tuna gesi ya kawaida, tuna helium tunakwama wapi. Lazima tuwe serious tukitaka kufikia uchumi tunaoutaka ni lazima tuwekeze kwenye rasilimali zetu za asili na rasilimali watu.

Karibuni kwa maoni.

Je, wewe ungefanyaje?
Hiyo copper ni copper kama copper tu au hata blue copper?
 
Kwa Afrika ni ngumu sana hii. Bila ya uongozi bora unaozingatia haki na teknolojia, hayo yatabaki ndoto tu.

Sisi hatuna mikakati thabiti ya namna ya kuweza kujiletea maendeleo ila tuna pigana kufa na kupona kutafuta namna ya kuhodhi madaraka.

Hivyo vyote ulivyovitaja hata tuwe navyo havitakuwa mwarobaini wa kutuondolea dhiki tuliyonayo na sana sana vitazidisha zaidi dhiki yetu kwa hulka ya watawala tuliyonao.
 
Mawazo hayo hayatakiwi ccm.Ccm na umasikini kiroho ni pacha.Umasikini ukiondoka ccm itakufa.
 
Kwa Afrika ni ngumu sana hii. Bila ya uongozi bora unaozingatia haki na teknolojia, hayo yatabaki ndoto tu.

Sisi hatuna mikakati thabiti ya namna ya kuweza kujiletea maendeleo ila tuna pigana kufa na kupona kutafuta namna ya kuhodhi madaraka.

Hivyo vyote ulivyovitaja hata tuwe navyo havitakuwa mwarobaini wa kutuondolea dhiki tuliyonayo na sana sana vitazidisha zaidi dhiki yetu kwa hulka ya watawala tuliyonao.
Uchungu mkweli.Kaburu Botha alisema."mtu mweusi hawezi ongoza jamii ikafanikiwa" hapa sijaelewa dhana hii ni kweli au ni kauli za kutufifisha.Chek zimbabwe ilikuwa na maendeleo SAwa na nchi za ulaya,check South Africa kabla ya uhuru, baada ya UHURU Hakuna nchi yeyeto ya afrika iliyosonga shida ni no hapa
 
Ongeza na hili "watu weusi wape bunduki uone wanavyo anza kuuana wao kwa wao"Botha
 
Huenda ubunifu ni dhana pana na wewe upo kwenye kona nyingine kabisa, na labda huenda tunazungumzia maeneo tofauti ya ubunifu.

Kwanza ukumbuke hatupo kwenye Ulimwengu sawa haswa kwa karne tuliyopo ambapo mambo sasa yanavyokwenda kwa kasi...ubunifu wowote usioweza kushindana sokoni hauna maana, hauna tija...yaani huwezi kubuni kifaa cha kusafishia nyumba ukakiweka sokoni ambako tayari kuna kifaa kama hicho na tena kimerahisishwa zaidi na Muuzaji anauza bei robo ya gharama zako za kukizalisha.

Mimi huwa nafuatilia sana bunifu mbalimbali zinazofanywa na Mtu wa kawaida tena uwani kwake.....Mimi huwa siamini kwamba kuna anachoweza kufikiria Binaadamu mwingine mahali na sisi Watu milioni60 tukakosa kabisa mwenye mawazo ya kibunifu kama hayo au yanayokaribiana na hayo.

Huwezi kufananisha Mwananchi mmoja mmoja wa huku kwetu na yule wa nchi zilizokwishaendelea...huku kwetu Mkulima tu wa kawaida akiwa na wazo la kifaa cha kupukuchua mahindi atapitia safari ndefu sana kukamilisha kazi yake na au hata akaishia njiani....ilihali Mkulima Mwenzake kama huyo aliyepo Urusi utaona tayari uwani kwake ana kifaa cha kukatia au kutobolea chuma kwa vipimo anavyokusudia.

Hivi hujaona sokoni kuna Majembe na Mapanga kutoka China? sasa je hatuna uwezo wa kutengeneza walau hata hizo zana na kutosheleza soko? wako wapi wale Wapare waliokuwa wameshapiga hatua kwenye ufuaji wa chuma tangu karne ya 19? kwa hiyo kwako huoni uhitaji wa sera na utashi wa Serikali kuona Wabunifu wanafika mbali...kwamba wale Wapare walipaswa kupambana wao wenyewe mpaka kufikia kumiliki Viwanda vikubwa vya kufua vyuma huku serikali ikiachia zana kama hizo kutoka China kujaa sokoni? Mpare angefanyaje?.

Kwa hizi nchi zetu Serikali isijivue lawama, kwa kuwa tu hawajui la kufanya ambapo huamua kukimbilia shortcut.
Umenena vyema hata china nasikia miaka ya nyuma uchumi wake ulikuwa kama wa TZ lkn kutokana na sera na utaratibu wake imefika mbal
 
Back
Top Bottom