Ningependa sana nikifa nisipelekwe mochwari, nichomwe moto

Kuna watu maekwepa majanga mbalimbali katika hali zisizo za kawaida mfano maskini kuwa tajiri, kipofu kuona, n.k lakini hakuna ujanja, ujuzi wala bahati itayokukwepesha na kifo, HAIWEZEKANI!! siku ikifika imefika tu na ni lazima ifike, Hakuna namna.

Ni nani asiejua adha za mochuari, Yani ukifa mkono au mguu umekaa katika namna ambayo hutaweza kuingia kwenye kaburi basi utavunjwa tu hio mifupa hata kwa nyundo ili mwili uingie kwenye jeneza, Kama mdomo ulikuwa wazi unapokufa basi utafungwa kwa nguvu na kupigwa super glue, Msishangae hata kidogo haya ndio mambo yanayofanyika huko mochuari ndio maana inashauriwa maiti muioshe tu huko huko nyumbani kama mkono au mguu haukukaa sawa basi itakandwa na maji ya moto hata saa zima ili kuuweka vizuri ila kwa bahati mbaya mochuari wale wenzetu hawana huo muda wa kubembelezana na ninawaonea huruma wanaotoa pesa ili maiti za ndugu zao zioshwe vizuri ila kinachoendelea huko ni siri.

Huko huko mochuari kuna ushirikina wa hali ya juu, Wafanya biashara wakubwa na wanasiasa wanaotegemea nguvu za giza pamoja na walozi wenye pesa zao zamani walikuwa wanakutwa wanachimba makaburi na kilichofata kilikuwa ni kipigo kitakatifu ila kwa sasa hizi mochuari zimerahisha mno hii kazi na imekuwa salama kwa hao watu, Siku hizi hao watu wanaongea na wanaoosha hizi maiti na kuwapa donge nono kwa kutekeleza wanayotaka, katika ulimwangu wa nguvu za giza maiti ina vifaa vingi, yaweza ikawa ni maji yaliyoogesha maiti, viungo flani vya mwili uliopigwa radi, na mbali zaidi kuna tetesi kwamba watu wenye viungo adimu mfano mtu mwenye kidole cha tatu kirefu huwa anakatwa, Mtu mwenye uume wenye saizi flani huchomolewa korodani, n.k Nisingependa haya yanikute.

Tukija swala la pili la kuchomwa moto nadhani hili ndio muhimu zaidi, Nisingependa mwili wangu uoze taratibu huko chini na kuliwa na mafilifili na kuwa na harufu ya ajabu, Nataka mambo yawe fasta fasta tu tumalizane. Pia hii miili katika ulimwengu wa giza wengi tumeshuhudia huko mbeya mtu anazikwa live ila anapatikana msukule huko mbele. Ningependa tu mwili wangu uchomwe majivu yamwagwe hata huko mlima kilimanjaro, ila pia ni gharama nafuu

Ni hayo tu ndugu zanguni, najua wengi mtanishambulia lakini that is what i wish

Mshana Jr karibu
Ukishakufa wewe ni chakula cha funza unaogopa nini?
You will be nobody don't worry be happy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah sijui nijibuje hapa.. Mimi sio vyote hivyo mkuu
Hii naisoma sasa hivi, wacha tu nisome maana kuna mambo watu hawawez yaelezea ana kwa ana, ngoja nisome.

Kaka Mshana, wewe ni mlozi? Mchawi?; mlogaji? Mshirikina?; mganga wa kienyeji? Ama ni nani? Mbali na muhudumu wa mochwari!

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Duu umeeleza na kuandika mengi lawama nyingi zikituendea sisi wahudumu wa mochwari.

Kuna vingine am sure havina ukweli hasa hapo kwenye kuvunja viungo vya marehemu

Tambua ya kwamba wafu wana nguvu sana na uki temper naye anaweza kukufanya kitu mbaya mno.

Vile vile hujazungumzia vituko vya wafu subiri kuna mada nitakuwekea hapa
mkuu huwa mnavunja

1585639067092.png


REF
 
Hii simple sana Nenda kaibe sokoni.. Kama mkazi wa Mbeya nenda kaibe Isengo.. Wanachoma moto unabakia majivu tu..
 
Back
Top Bottom