Ningependa Kujua Asili?

Mbongo Asili

Member
Feb 7, 2008
37
2
Ndugu zangu ningependa kujua asili ya majina yafuatayo.

1.Kayumba
2.Mwanantambwe.
3.Kirabiza
4.Mwacheseme

kwa sababu nimewahi kukumbana na familia moja nchini kenya na majina hayo na wanadai eti wao ni wamanyema.
 
Ndugu Mbongo Asili,

Kimsingi na kiasili Wamanyema ni watu wa Maniema/Manyema. Hili ni eneo katika Democratic Republuic of Congo. Nchini Tanzania Wamanyema wamezagaa nchi nzima hasa mijini. Kwa kuwa idadi yao kwa wingi sana wapo Ujiji basi kiujumla wanahesabika kama watu wa Kigoma ambako wenyeji asilia ni Waha.

Kama ninavyoyaona majina hayo, naweza kuamini bila ya wasiwasi wowote kuwa hao uliokutana nao huko Kenya wamekuambia kweli kuwa wao ni Wamanyema.

Kama ninavyofahamu mimi kwa uhakika kabisa Mwanantambwe ni jina la Kimanyema. Ntambwe/Tambwe maana yake ni Simba na Mwana ni kibantu na maana yake ni hiyo hiyo Mwana/Mtoto. Kwa hiyo Mwanantambwe ni Mwana/Mtoto wa Simba. Jina hili ni moja katika majina ya ukooni mwangu.

Nchini Tanzania Wamanyema wanajulikana kama kabila. Ukweli ni kuwa Wamanyema wana makabila yao tofauti. Ni sawa kuwaita watu Watanga. Lakini ukifika katika eneo la Tanga utakuta Wadigo, Wabondei, Wasambaa, Wazigua, Wasegeju na kadhalika.
 
Shukrani kwaminchi,
kwakuwa wew inaonekana kama mmanyema, Hii familia ikitaka kujua asili yake humu tanzania hasa ukoo wao watajuwaje kwani wanadai babu yao mmoja alikuwa akiitwa ALI KIRABIZA alikuwa mkaazi wa daresalaam sijui mtaa wenyewe lakini nitajaribu kufuata. babu yao mwengine aliitwa IDDI KAYUMBA NA Baba yao AItwa Nkongoro Mataka jee kunawezekano wowote wanaweza kufuatilia jadi yao???
 
Shukrani kwaminchi,
kwakuwa wew inaonekana kama mmanyema, Hii familia ikitaka kujua asili yake humu tanzania hasa ukoo wao watajuwaje kwani wanadai babu yao mmoja alikuwa akiitwa ALI KIRABIZA alikuwa mkaazi wa daresalaam sijui mtaa wenyewe lakini nitajaribu kufuata. babu yao mwengine aliitwa IDDI KAYUMBA NA Baba yao AItwa Nkongoro Mataka jee kunawezekano wowote wanaweza kufuatilia jadi yao??? na maana ya 'Ache Nkwanda nini'??
 
Zamani, kwa kuwa safari zilikuwa kwa miguu tena kwa njia za panya, ilionekana kuwa Mani-Ema ni mbali sana na kwamba wazee wetu walishindwa kabisa kurudi kwao, kwa miguu tena.

Na kwa kuwa walikuwa hawana mawasiliano na wa kwao, kama haya mawasiliano tuliyonayo hivi sasa, basi, walikuwa wametengwa kabisa na mizizi yao.

Lazima nikiri, walijitahidi sana kutunza mila na desturi zao na hata ngoma zao walizicheza nyakati za sikuuu kama vile Eid na pia wakati wa matukio, kama vile kupiga "chondo" kutoa taarifa ya mtu kuifariki dunia.

Ushauri wangu kwako na kwa hao ndugu/rafiki zako ni kwamba kama wanataka kujua maana ya majina yao na jadi za koo zao inabidi wajishughulishe kidogo kwanza kujua kabila zao na kisha kusafiri kidogo kama vile watalii waingie U-MANI-EMA-NI.

Kwa ndege wanaweza kwenda Kindu kisha wakasafiri kwa motokari au pikipiki kwenda kwenye vijiji vya makabila yao. Wanaweza kwenda kwa ndege pia au kwa meli kutokea Kigoma mpaka Bujumbura kisha wakaingia Umanyemani kwa motokari kupitia Uvira. Au wanaweza kuvuka Ziwa Tanganyika kwa meli kutokea Kigoma mpaka Kalemie kisha wakapanda gari moshi (train) Kalemie mpaka Kongolo watakuwa wameshaingia Umanyemani kutoka hapo ni motokari au pikipiki mpaka kwenye vijiji vya makabila yao. Ukiniambia wao ni wamanyema wa kabila gani, naweza kuwasaidia kuwaambia waende wapi au kijiji gani.

Lugha - wengi wao wanazungumza Kiswahili kibovu, wenyewe wanakiita Kingwana ambacho wanakichanganya na Kilingala na Kifaransa kibovu pia. Ukiwasikiliza vizuri ni rahisi kuelewana nao.

Fedha - japokuwa mnasema sio msingi ni muhimu kuwa nazo na kuzilinda ni muhimu zaidi, wanaweza kukuingiza mjini.

Malazi - katika vimiji kama Kindu, Kasongo, Kabambare, Kongolo,
Lusangi na mingine ya aina hii wanazo Guest Houses. Lakini ndio hivyo tena usafi wa kijijini.

Chakula - masurufu kibindoni, hata hivyo wana mikahawa yao wanaiita restaurants.

Hii inakuwa ni adventure "akili mkichwa." Ukoo mara nyingi ni vigumu kwisha wote. Wakiwapata wenye majina kama yao, utafiti wao utaanzia hapo. Kwa kawaida wanaamini sana kuwa ndugu zao wengi walipotelea Tanganyika. Kwa hiyo, wakiwapata, watapokelewa kama Wafalme na kukubaliwa kuondoka ni kwa mbinde.
 
Shukrani ndugu pengine nilisahau kukfafanua kabila lao maana niliwahi kuwadadisi na wakasema kabila lao hawana uhakika lakini wame wahi kumsikia baba yao akisema kuwa kabila lao ni WAYAO WASHIRAZI. jee lipo kabila kama hili umanyemani??? kabla sijaendelea ningependa kukuomba razi kwa usumbufu wowote ule ninao kupa. pili wamewahi pia kumsikia baba yao akisema yakuwa babu yake yeye alikuwa kitu kama Chifu wa ukoo wao. sielewi lakini nitajaribu kuwasiliana nao nipate habari zaidi.
 
Ndugu Mbongo Asili,

Hapa umenichanganya sana. Majina ya jamaa zako, hasa yale matatu ya mwanzo ni ya kimanyema kabisa. Lakini, hayo makabila uliyoyataja si ya umanyemani.

Umanyemani kuna Wabangubangu, Wakusu, Wagenya, Wabembe, Wahoholo, Warege, Wabwari, Wagoma, Wabembe na makabila mengine mengi. Najua hakuna Wayao au Washirazi.

Ninavyofahamu mimi wayao ni watu wa Tunduru upande wa kusini mwa Tanzania katika mkoa wa Ruvuma. Washirazi ni watu wa Persian Gulf na nchini Tanzania wengi wao wako katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Labda katika kutafiti, itawabidi waende sehemu zote hizo. Kigoma/Ujiji, Manyema, Tunduru, Unguja na Pemba na ikiwezekana Persian Gulf.

Penye nia hapakosekani njia.

BTW: Mimi hujanisumbua. Haya ndio baadhi ya matunda ya Jambo Forums.
 
yawezekana kuwa pengine kachanganya Kabila baba mmanyema mama kawa myao hiyo issu ya ushirazi naona ni katika wale wanao taka uyakhe na uswahili, lakini kwa upande mwengine Baba yao yuaitwa Nkongoro Mataka ampbapo mataka ni machifu wakizamani wakiyao na pia yawezekana yakuwa Huo umanyema pengine walikuwa watumwa yaani slaves ambao waliachwa uhuru, Issue nyengine Huyu mataka pengine katoroka na mwanamke wakimamyema aliye mtumwa lololol anyway issue hapa imekuwa ngumu kidogo unless wamanyema wanatumia majina ya nkongoro na mataka....Je maana ya Ache Nkwanda, Ache mataka pengine waijuwa lakini naona hapa hiki ni kiyao. Au laa sivyo huyu Nkongoro Alikuwa mtumwa au slave wa che mataka pengine ikabidi atumie jina lakini kwa sababu Nkongoro ina sound ki Congo kidogo
 
Niliwahi kusikia zamani watu wakisema kuwa neno manyema ni msitu au watu wa msituni (Una-Ma-Nyema, eaters of flesh), wala watu na walikuwa watu wanao penda sana vita yani kupigana na kula nyama za watu...! Je hii ni kweli?
 
Hapa sasa kazi.

Lisemwalo lipo, kuhusu kula watu hili lina-uwezekano mkubwa sana, kwani kwa hapa Dar, na kutokana na minong'ono ya hapa na pale, ni kuwa "wamanyema ni wachawi sana na wengi wao ni wanga". Keeping that in mind na kama wengi tusikiavyo ya kuwa 'wanga' huhusishwa sana na misosi ya nyama za watu. Sishangai baada ya kufanya one plus one.
 
Ndugu X-paster na Dar-Es-Salaam,

Mimi ni Mmanyema-Mtanzania. Babu yangu mzaa Baba yangu alikuja katika nchi yetu hii kabla haijaitwa Tanganyika. Ilikuwa ikiitwa Afrika ya Mashariki ya Wadachi. Aliwahi kuwa Askari Jeshi wa Jeshi la Kivita la Wadachi na alishiriki katika Vita Kuu ya Kwanza 1914-1918, akiwa upande wa Wadachi (Wajerumani).

Nimebahatika kufika huko Maniema mara tatu kwenye kijiji chetu cha asili na kukutana na baadhi ya jamaa zetu wa huko na hiki ninachojaribu kuwaeleza hapa si cha kusikia peke yake bali na kuona pia.

Mani-Ema si msitu ni Eneo la Falme ya Mfalme Ema. Kabla ya Wazungu kuingia katika ardhi ya Kongo, kulikuwa na Falme nyingi sana katika nchi hiyo. Moja wapo iliyokuwa kubwa na ndio iliyokutana na Wazungu kwanza upande wa Atlantic Ocean ilikuwa ni ile Falme ya Mani-Kongo (ndio maana wenzetu wanajiita Wa-Kongo-Mani). Hawa wa Mani-Ema walipambana mwanzo na Waarabu.

Hivi sasa Maniema ni moja ya majimbo (Province) ya DRC. Ikiwa na Makao Makuu ya Jimbo (mkoa) mjini Kindu. Zamani ilikuwa ndani ya Jimbo la Kivu-Maniema na Makao Makuu wakati huo yalikuwa mjini Bukavu.

Ndani ya Jimbo la Maniema zaidi ya Makao Makuu ya Jimbo, Kindu, kuna miji midogo midogo kama vile Kasongo, Kabambare, Kailo, Pangi, Kibombo, Punia, Lobutu na mingineyo.

Hawa jamaa wa Maniema ni watu kama mimi, wewe na yule. Wanamajeraha yaliyowapata Waafrika wote kwa kuingiliwa na wageni ama wakizungu au wakiarabu. Wao walipambana na Waarabu walioingia katika ardhi yao kwa mara ya kwanza mnamo miaka ya 1840 wakitafuta biashara ya watumwa na pembe za ndovu.

Historia ya vita vya makabila iliyolikumba Bara zima la Afrika wao haikuwaachia. Wamaniema wa Kabambare wa kabila la Wabangubangu ndio wanaosemekana walikuwa wakila watu hususan mateka wa vita ili kutisha wenzao wa makabila mengine wasiwachokoze.

Lakini Dr. David Livingstone, ambaye alikaa kwa muda mrefu mjini Kabambare, katika barua zake anadai kwamba si kweli kuwa Wabangubangu walikuwa wakila watu. Yeye anadai kuwa walikuwa wanakula masokwe na kuhifadhi mafuvu yao kuwatishia wengine kwamba mafuvu hayo ni ya watu walioliwa.

Siwezi kukubali wala kukataa juu ya suala hili la watu kutafunwa.

Kuhusu hili la kuwa Wamaniema ni wanga nadhani ni lile lile la uwanga wa Bagamoyo (mlingotini), Tanga (chumbageni), Pangani (mbweni), Sumbawanga, Umakondeni na Kigoma. Kuna waganga na wachawi kila mahali (myth).
 
Salaam Ndugu kwaminchi,
sasa basi niliwahi kuwasiliana na hawa marafiki zangu kutoka kenya na wamenieleza yakuwa Nyanya yao mzaa baba ndiealiyekuwa mmanyema, na babu yao NiMyao na ndio maana baba yao anaitwa Nkongoro mataka ambalo hilo ni jina la Kiyao, natumai sasa hivi hali itakuwa rahisi mno kwa wao kujua asili yao kutoka hapo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom