Hapa sasa kazi.
Lisemwalo lipo, kuhusu kula watu hili lina-uwezekano mkubwa sana, kwani kwa hapa Dar, na kutokana na minong'ono ya hapa na pale, ni kuwa "wamanyema ni wachawi sana na wengi wao ni wanga". Keeping that in mind na kama wengi tusikiavyo ya kuwa 'wanga' huhusishwa sana na misosi ya nyama za watu. Sishangai baada ya kufanya one plus one.
Ndugu X-paster na Dar-Es-Salaam,
Mimi ni Mmanyema-Mtanzania. Babu yangu mzaa Baba yangu alikuja katika nchi yetu hii kabla haijaitwa Tanganyika. Ilikuwa ikiitwa Afrika ya Mashariki ya Wadachi. Aliwahi kuwa Askari Jeshi wa Jeshi la Kivita la Wadachi na alishiriki katika Vita Kuu ya Kwanza 1914-1918, akiwa upande wa Wadachi (Wajerumani).
Nimebahatika kufika huko Maniema mara tatu kwenye kijiji chetu cha asili na kukutana na baadhi ya jamaa zetu wa huko na hiki ninachojaribu kuwaeleza hapa si cha kusikia peke yake bali na kuona pia.
Mani-Ema si msitu ni Eneo la Falme ya Mfalme Ema. Kabla ya Wazungu kuingia katika ardhi ya Kongo, kulikuwa na Falme nyingi sana katika nchi hiyo. Moja wapo iliyokuwa kubwa na ndio iliyokutana na Wazungu kwanza upande wa Atlantic Ocean ilikuwa ni ile Falme ya Mani-Kongo (ndio maana wenzetu wanajiita Wa-Kongo-Mani). Hawa wa Mani-Ema walipambana mwanzo na Waarabu.
Hivi sasa Maniema ni moja ya majimbo (Province) ya DRC. Ikiwa na Makao Makuu ya Jimbo (mkoa) mjini Kindu. Zamani ilikuwa ndani ya Jimbo la Kivu-Maniema na Makao Makuu wakati huo yalikuwa mjini Bukavu.
Ndani ya Jimbo la Maniema zaidi ya Makao Makuu ya Jimbo, Kindu, kuna miji midogo midogo kama vile Kasongo, Kabambare, Kailo, Pangi, Kibombo, Punia, Lobutu na mingineyo.
Hawa jamaa wa Maniema ni watu kama mimi, wewe na yule. Wanamajeraha yaliyowapata Waafrika wote kwa kuingiliwa na wageni ama wakizungu au wakiarabu. Wao walipambana na Waarabu walioingia katika ardhi yao kwa mara ya kwanza mnamo miaka ya 1840 wakitafuta biashara ya watumwa na pembe za ndovu.
Historia ya vita vya makabila iliyolikumba Bara zima la Afrika wao haikuwaachia. Wamaniema wa Kabambare wa kabila la Wabangubangu ndio wanaosemekana walikuwa wakila watu hususan mateka wa vita ili kutisha wenzao wa makabila mengine wasiwachokoze.
Lakini Dr. David Livingstone, ambaye alikaa kwa muda mrefu mjini Kabambare, katika barua zake anadai kwamba si kweli kuwa Wabangubangu walikuwa wakila watu. Yeye anadai kuwa walikuwa wanakula masokwe na kuhifadhi mafuvu yao kuwatishia wengine kwamba mafuvu hayo ni ya watu walioliwa.
Siwezi kukubali wala kukataa juu ya suala hili la watu kutafunwa.
Kuhusu hili la kuwa Wamaniema ni wanga nadhani ni lile lile la uwanga wa Bagamoyo (mlingotini), Tanga (chumbageni), Pangani (mbweni), Sumbawanga, Umakondeni na Kigoma. Kuna waganga na wachawi kila mahali (myth).