Ningemwambia haya Rais Samia endapo ningepata nafasi ya kukutana naye

Charliemic

JF-Expert Member
Feb 17, 2019
585
919
Ningemsalimia kwa unyenyekevu mkubwa na kumshukuru kwa nafasi ya kukutana naye!

Ningemwambia kuhusiana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi katika taifa letu!

Ningetoa mapendekezo yangu kuwa sekta ya kilimo itazamwe upya kwa jicho la tatu kama mkombozi wa changamoto hiyo!

Kuwa yatengwe maeneo kikanda ambayo yatapelekewa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji na kwamba zipelekwe huduma za kijamii katika maeneo hayo.

Vijana walio katika vikundi wasajiliwe kisha wagawiwe hayo maeneo. Wapewe mikopo isiyo na riba! Wapelekewe wataalam wa kilimo pia ziwepo mashine mbalimbali za kuwasaidia! Vijengwe viwanda vya kuprocess mazao kwa ushirikiano wa sekta binafsi na serikali. Yatafutwe masoko nje ya nchi kwa bidhaa zilizochakatwa.

Pia zifanywe jitahada za kufufua mazao ya kimkakati kama kahawa, korosho, pamba, chai na mkonge. Wakulima wapewe ruzuku kupitia vyema vya ushirika!

Serikali ielimishe wananchi kulima chikichi kwa wingi maeneo ya huko Kigoma

Mtaala wa elimu ubadilishwe wanafunzi wa sekondari wajifunze masomo ya ufundi na pia ufugaji wawapo mashuleni.

Veta ziboreshwe na kupewa vitendea kazi, wahitimu wajiunge kwenye makundi yaliyosajiliwa wapewe mikopo isiyokuwa na riba!
 
Back
Top Bottom