Ningekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ningeng'atuka

jakarason1974

Senior Member
Apr 3, 2012
103
50
Kama kweli Waziri wa mambo ya ndani ana elewa majukumu yake na umekaa kimya na mambo yanayoendeshwa na RC basi hakika haujui majukumu yako... Na kama ingekuwa mimi ndio Waziri wa mambo ya ndani hakika ningeng'atuka uwaziri.... huu ni udhalilishaji wa nafasi yako ya uwaziri na elimu yako ya first class
 
Kwani majukumu yake ni ni ni mkuu juzi hapa si kasima vita ya kupambana na hao wauza madawa ni vita ya kujitoa rizki??
 
Kwani majukumu yake ni ni ni mkuu juzi hapa si kasima vita ya kupambana na hao wauza madawa ni vita ya kujitoa rizki??
Yeye ni Waziri wa mambo ya ndani na ni mjumbe wa kamati ya Ushauri ya ku deal na madawa ya kulevya... Sheria ya mwaka 2015
 
Mwigulu Nchemba yuko sahihi kutulia, huyo aliyeamua kulibeba zigo bila kumshirikisha ana yake agenda! Amwache Makonda apambane nalo mwenyewe; Makonda na Mwigulu wanajenga nyumba moja, serikali ni moja na vita ni moja, mihadarati; kuna haja gani kugombania fito?!
 
Vita ya drugs inafanyika kimya kimya na kisayansi sio kwenye media unasikia tu kingpin wa drugs ametiwa mbaroni au ameuawa kwenye crossfire sasa kingpin wa ukweli wa drugs utamuita ijumaa atakuja??
 
Vita dhidi ya madawa ya kulevya lazima viwe na mbinu za kijasusi na si staili ya Id Amin. Tutafute uzoefu wa FBI na CIA. Vita hii hapiganwi kama pambono la ngumi na majigambo yake.
 
Vita ya drugs inafanyika kimya kimya na kisayansi sio kwenye media unasikia tu kingpin wa drugs ametiwa mbaroni au ameuawa kwenye crossfire sasa kingpin wa ukweli wa drugs utamuita ijumaa atakuja??
Kuja hawezi tena akiamua mfano wa mexico anamtafuta mkeo anammega kwanza afu ndo anasepa
 
Kama kweli Waziri wa mambo ya ndani ana elewa majukumu yake na umekaa kimya na mambo yanayoendeshwa na RC basi hakika haujui majukumu yako... Na kama ingekuwa mimi ndio Waziri wa mambo ya ndani hakika ningeng'atuka uwaziri.... huu ni udhalilishaji wa nafasi yako ya uwaziri na elimu yako ya first class
Ang'atuke kwa sababu ipi? Amemwachia 'waziri wa mambo ya jikoni' afanye yake, Mwigulu hawezi kukurupuka kushindana na RAYMOND ( nitoke vipi) wakati anatekeleza majukumu yake kwa ufasaha.
 
Piga kimya jembe langu mwigulu
Huyu Mdogo wako ameanzisha vita bila kukushirikisha, mwache tu aendelee maana hakuna namna
 
Ningekua Mwanachama au mbunge wa Chadema ningejiuzuru, yaani Mwenyekiti anauza ngada...
 
Sio ya kwamba ang'atuke
Kaka mkubwa katulia
Huyu mtoto mdogo wa mwisho anaropoka tu sisi kwetu leo tumekula pilau
Kila jambo hufanywa kwa hekima na kufikiria
 
Kwa mfano kwenye hii inshu ya madawa kama ina hela sana
Yapigwe marufuku kutumia na vijana wa Tz ila
Watz wakauze huko nje wajipatie kipato basi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom