G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Naam hilo ni jambo ambalo ningekuwa nimeshalifanya mchana kweupee na staili ambayo ningejiuzulu nayo leo, kwa hakika ningekuja kuwa shujaa huko mbeleni. Ushujaa usio na kifani!
Kwa kweli kwa mwenendo wa serikali ulivyo na aina ya uongozi unaojichimbua ningekuwa nimeondoka. Kazi ya waziri ni kumshauri rais namna bora ya kujenga nchi ili ikue. Kuifanya nchi iwe na vitu vipya vinavyoikuza na kuonekana bora machoni pa wa-nje!
Kinapofanyika kikao cha baraza la mawaziri pia kunakuwa na fursa za kuibua mawazo mapya. Kwa kweli kwa uelekeo wa utawala huu hilo halina hata dalili ya kutokea! Kwa kifupi halipo.
Kama kila agizo la ni nini kifanyike linatoka ikulu. Sasa nikae pale nifanye nini?
Ninayasema haya baada ya kubaini kuwa mawaziri WOTE wa rais Magufuli hawana amani kabisa. Wanatia huruma katika utendaji na wanaonekana wazi kuwa wapowapo tu kwenye nafasi zao! HAWAIJUI KESHO YAO ITAAMKA VIPI! Hiyo kwa hakika ni dalili mbaya kabisa ya utawala uliokosa afya! Mara tuambiwe sasa hata kuhoji jambo haturuhusiwi, kweli?
Baada ya kuandika haya ni dhahiri mawaziri wa rais Magufuli wajitafakari! Wajipambanue kivingine ili kusonga mbele na kuleta ubunifu utakaoliletea maendeleo taifa. Wakishindwa kutokana na vikwazo au woga basi ni ushauri wangu kwao kuachia ngazi kuliko maswali watakayoulizwa huko mbeleni!
Hapa siongelei kuchungwa eti kwa sababu ya wizi. Nauchukia sana wizi wa mali ya umma! Lakini emb tujiulize kweli wakipewa uhuru wa kufanya kazi wataiba? Kwanini tusirudishe rasimu ya Warioba iliyojenga misingi bora kikatiba kwa kila mmoja kuliko ilivyo hivi sasa ambapo mtu mmoja anajiona kuwa hakosei, yeye ndiye mwenye akili sana. Msafi asiye na doa?
Hivi mnaona kama tutaendelea hivi taifa litakuwa?