Avanti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2010
- 1,209
- 239
Hapana, huu ni ujumbe tu wa hadharani kwa viongozi wote - nilio na simu zao na wale ambao sina. Kwamba, waachane na mambo ya siasa za vyama vichanga waelewe wako vitani na kosa moja lina gharama kubwa. Haiwezekani, kila baada ya masaa watu wanakuja kushindana nani anajua zaidi mambo ya chama na nani hajui halafu wakafikiria wanakitendea chama hisani. Hivi, Pentagon mnafikiri wote wanapendana? Hivi mnajua misuguano ya 'ego' ambayo iko kati ya Marines, Army na Navy? Lakini inapokuja vita huwezi kujua kuna tofauti! Wote wanaenda vitani wakipigania chini ya bendera ya Marekani!
Kwanini nitumie mfano wa mbali - tulipoenda vitani dhidi ya Uganda siyo wote walioenda kupigana walikuwa ni JWTZ! Wengine walikuwa recruited kutoka polisi, JKT, Magereza na hata mgambo! Wengine walitoka Zanzibar - haijalishi kama walikuwa hawaupendi Muungano! - lakini wote hawa walipigana na wengine kufa chini ya bendera ya Tanzania.
Hii ni changamoto ya Mwenyekiti mwenyewe kuweza kuhakikisha wapiganaji wake wana focus ya vita - a.k.a Arumeru Mashariki. Nimekaa na kusoma toka wiki ianze na kuona jinsi mada mbalimbali za kuiharibu chadema wakati wa vita zikitokea na watu wanafikiria ni mijadala ya kawaida tu. Well, kweli kabisa kwa vile sina uwezo tu ila ningekuwa na uwezo...
Ndio maana siwezi kuwa mwanasiasa.
Mwanakijiji writes and writes and writes but wapi bana! Watu wameweka gundi masikioni! Ruzuku bana!