Ningekuwa na uwezo ningecharaza bakora viongozi wote wa CHADEMA Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa na uwezo ningecharaza bakora viongozi wote wa CHADEMA Taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 18, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa!! Kama kuna vitu vinanitibua sasa hivi - na sijachangia sana - ni haya malumbano, vijembe, uchimvi na mashambulizi ya "wao kwa wao". Vitani kunakuwa na "friendly fire" lakini hii siyo "friendly fire" tunachoshuhudia ni silaha zimegeuzwa toka kwa CCM na kuelekezwa kwa CDM wenyewe ndani kwa ndani. Badala ya wapiganaji wote kusimama kupigana na kusonga mbele, muda mwingine unatumiwa kupigana wenyewe, kujeruhiana na kutafuta muda kugangana.

  Sasa hivi CCM hawagombani! Wana tofauti kubwa zaidi kuliko zilizoko ndani ya CDM lakini wanajua kabisa kuwa mkiwa vitani akili, mikakati, silaha zenu zote zinaelekezwa kwa adui! Lakini, kwa vyovyote vile inaonekana CDM itajikuta inatumia muda mwingi zaidi kujitetea na kujibu hoja za wao kwa wao ndani ya Chama badala ya kutulia kupanga mikakati ya kushinda! Na hapa ndipo unapoona mkakati wa Wassira kwa mfano na wengine tuliowaona siku hizi chache, wote wanajitahidi kuwapa CDM sababu ya kugongana wao kwa wao kiasi kwamba wakishawatupia hoja CDM wanabaki kujibizana na kutafutana badala ya kupigana na adui!

  Ndio maana ninasema ningekuwa na uwezo - bahati mbaya sina - ningehakikisha watu wanaoitwa wapiganaji wanakuwa na akili ya kivita (war mentality). When you are fighting in a war your collective mentality is shaped in such a way that you are absolutely focused on defeating the enemy! You don't spend your time to start worrying about your generals!

  Binafsi ningewaita hawa wote wanaotajwa pamoja - ningejaribu kuwaweka pamoja waseme tofauti zao ni nini - halafu kama bado hawataki kusikilizana na kurudisha akili zao kwwenye vita ningewacharaza bakora kama "Mzee Kifimbo"! Halafu ningewaondoa kabisa kwenye mambo ya kampeni! Mwenyekiti yuko wapi?

  C'mmon now! mnataka kushinda au kushindana? CDM Taifa safisheni migongano yenu hatutaki mtafute kisingizio cha kutofanya vizuri au kuendeleza malumbano baada ya uchaguzi. Hakuna mtu mwenye uwezo wakuonesha uongozi na kutuliza hivi vita vya wenyewe kwa wenyewe? Waacheni CCM wawashambulie kwani ni haki yao; na nyinyi msiwaonee huruma!

  Hivi huu muda wa kuandika na kuchunguzana na kujibizana wakati mko vitani mnautoa wapi? Sijaona mtu kaandika kitu cha maana kuelezea kushindwa kwa sera za CCM Arumeru Mashariki? Sijaona mtu akikosoa kushindwa kwa sera hizo wakati wa Mkapa - zaidi ya watu kutumia muda kufurahia majibu ya Vincent Nyerere!; Vincent Nyerere angemchambua Mkapa na kushindwa kwa sera zake ingekuwa bora zaidi kuliko kugombania jina; hilo angemuachia Madaraka! grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!

  Nitafafanua zaidi katika "Arumeru East Contest: CHADEMA'S own Battle for Fallujah"
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  me too
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kweli wafaa kuchapwa
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Usisahau kipindi kama hiki na hasa baada ya kibano cha Igunga CCM wameongeza fungu la 'mamluki', hivyo fujo ni nyingi sana. Lakini naona kama wanajitahidi sana (CHADEMA) given the circumtances! Haimaanishi hakuna room for improvement lakini wanajitahidi.

  Wanachotakiwa sasa ni kupaza sauti kwa nguvu zote kabisa kuhusu issues zinazowagusa wananchi wa kawaida huko Arumeru Mashariki. Waziongelee moja moja, kuanzia ushuru wa ndizi sokoni, hadi madawati yasiyojaa kwenye majengo yale yale ya shule!
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  MM, una maanisha "kuwachapa viboko" literally !?
  Mbona maandiko yako ni fimbo tosha? Nadhan huu ndio wakati ambapo wazee wa chama wanapokuwa na faida, logic ya kawaida inawata wachukue jukumu hilo la kuziita pande zote zinazohasimiana kama zipo ili frontline ikae mkao wa kivita na mentality ya kivita.

  Lakin sidhani kama ni busara kuwachapa viboko viongozi wa CDM pekee, kwani vita hii si ya CDM pekee, bali ni ya CDM pamoja na Wanaarumeru. Hivyo basi wote kwa pamoja au kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kutambua hilo na kutimiza wajibu wake. Hizi siasa uchwara za mitandaoni na kuchafuana zinapandikizwa na CCM kwa style ile ile inayotumiwa na CIA- "Data Sowing"

  Hivyo ni vyema na wananchi wakaeleweshwa juu ya nguvu waliyonayo ili wawachukulie hatua hawa wanasiasa uchwara

  View attachment 49625
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  mawazo mazuri but sio mda muafaka kwa chadema kupata mawazo haya kwan ndan ya chadema hakuna malumbano kama vile unavyofikiria ww alafu hzi siasa za mitandaoni zisikuchanganye mpaka ukahisi eti kuna ugomvi chadema, sema kuna wahuni au muhuni m1anayepiga siasa chafu juu ya chadema kutokana na chuki zake binafsi na ukweli wote tumeshaujua na tutawapuuzia mpaka wajione mavi, bkoz kama ni kashfa za kweli basi tungeshazisikia kwan wanafiki wangeshazipeleka majukwaani, SO USICHANGANYWE NA SIASA CHAFU ZA MITANDAONI KWANI ZIPO CONTROLED NA MPUMBAFU MMOJA AU WAWILI BUT CHADEMA STIL IPO IMARA NA KAMA UNABISHA NJOO KITAA PENYEWE KWANI UGUMU WA MAISHA YA KUSABABISHIWA NA CCM NDO UNAOAMUA NA UTAKAOAMUA HATIMA YA MAGAMBA.BRAVOOOOOOOOO CHADEMAAAAA.
   
 7. A

  Awo JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Nakubali. CCM wana mkakati wa kuwatoa CDM mstarini. Wawe makini, wajibu mapigo lkn wasisahau lengo la ushindi.
   
 8. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Na hili ndiyo tatizo kubwa la vyama vya upinzani Tanzania. CCM huwabomoa kirahiisi kabisa. Hapo ni kuwa kuna mamluki yuko kati yao ambaye ameshalipwa mapesa, yuko kazini. Kabla hawajampata ni kizunguzungu watapata.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hivi hawajasikia yaliyomkuta yule "rogue soldier" wa US kule Afghanistan? Badala ya kupigana na Taleban kaenda kuwaua watu 16 wasio na hatia? Unafikiria jeshi lingemuacha huko huko? No, wamemchukua na kumrudisha US na kumsweka kwenye gereza lenye ulinzi mkali. Huwezi ukiwa vitani ugeuze silaha kwa wenzako au watu wasio maadui haalafu ukaendelea. Kama kuna "mhuni" mmoja kama ulivyosema itanishangaza kama CDM haina intelligence capabilities ya kumjua na kumuondoa kabisa. Haya ya kuvumiliana na kuoneana huruma ndio mwanzo wa kuvurugana. Its war out there!
   
 10. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji,
  Ushauri wa kuwasaidia chadema ni kuwataka wakae chini, wazungumze matatizo yanayowakabili na namna ya kuyatatua.
  Kushughulikia anaeyaleta maneno haya hapa jamvini haina tija, kwanza wataishia ku guess tu ni mara huyu mara yule. La muhimu ni kuangalia yaliyo ya kweli, na kuona namna ya kuyatatua, wasonge mbele. Wakiwa safi ndani ya nyumba yao, hata hao wanaohangaika kuyaleta hapa watakuwa hawana hoja!
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  kumbe ni mmoja tu?
   
 12. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  huku arumeru mapambano yanendelea bila kujali kinachotokea mtandaoni,wapiga kura hawasomi hizi propaganda za wahuni wachache.
   
 13. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kweli MMM, ni vizuri uiandae vyema bakora yako....

  Natamani Ben (wa JF) aje hapa, maana kuna fukuto nimelipata sijalielewa.

  Na naomba ukianza kuwachapa uwaulize na maswali ya wanatutaka nini watz!
   
 14. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu usikubali tu wanafaa kuchapa bila kuitazama battle ground. Hata tatizo linalosemwa lipo ndani ya CDM sio kubwa kama linavyozungumzwa hapa
  Cha nsingi ni kuwa engage Wanaarumeru ili wajue nguvu waliyokuwa nayo. Hebu jiulize, ni kwa nini wanasiasa uchwara walete fujo halafu wananchi wawaangalie, eti mpaka RED BRIGADE watokee.
  Nimeshasema kwenye thread fulani na hapa nitasema tena. Wananchi waelimishwe juu ya nguvu waliyonayo ili vita hii isiwe kati ya Green Guard na Red Brigade, au CDM na CCM tu bali wanaarumeru na wanasiasa uchwara. Wananchi wakishajua nguvu waliyonayo, ndipo wanasiasa uchwara na wafuasi wao watakapoipata
   
 15. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sioni sababu ya msingi katika hizi kelele .....Wakati mwingine kukaa kimya nijibu tosha kabisa
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nice 2, wanaoleta haya mambo hadharani na kulumbana hadharani hawana sababu ya kutaka kutatua matatizo. Lengo lao ni kuwaabisha wengine, kukidunisha chama na kwa kweli kabisa kukidhoofisha wakati wa kuelekea uchaguzi wa Arumeru. Kama wangekuwa na nia nzuri - ya kuonesha matatizo - wangeweza kabisa kutumia njia nzuri. Jeshini kuna kitu kinaitwa nidhamu ya kijeshi ambapo askari anatakiwa kuifuata. Askari hawezi kuwa na tatizo na askari mwingine na badala yake anaenda kanisani kulalamikia au msikitini!

  Ni jukumu la uongozi kujua nani ana matatizo au kuwaalika hao walio na matatizo na kama ni watu wanaotajwa humu basi waitwe wahojiwe ili wakanushe kuwa siyo wao. Ila kunarrow down field of suspects. Ni rahisi kuweza kuwajua watu hawa ni kina nani kwa kwa kutumia counter intelligence moves. Hapa ningependa kujua sana Rwakatare anafanya nini au yeye ni ulinzi tu na siyo kiongozi wa Intelligence. Kwanza CDM inayo Intelligence Unit?
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hivi alichosema Wassira hadharani si kimeanzia hapa? DON'T UNDERESTIMATE YOUR ENEMY!
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,267
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, bora useme wewe kiazi maana ni kitamu, nikisema mimi muhogo nitaambiwa mchungu!.

  Niliposema "CCM Imechokwa!, Chadema Hawajajipanga!" nilishukiwa ipasavyo!. Sasa CCM chovu ndio hiyo inajipanga!, Chadema imara inayotakiwa kujipanga, ndio hii inapiga mark time, kufanya mazoezi siku ya mechi na kuchezea shilingi chooni!.

  Afadhali maneno haya umeyasema wewe, tungeyasema sisi wa damu ya kunguni saa hizi mood zingeshatubadilikia!.

  Thanks

  Pasco.
   
 19. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hakuna busara ya kujadiliana na mtu anayetoboa mtumbwi kwa makusudi wakati anajua mpo ktk kina kirefu cha maji ambako mtumbwi ukipasuka hatasalimika yeyote. Uongozi wa CDM uondoe mamluki hawa kurudisha nidhamu ktk chama.
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Kwenye ile thread nyingine Kitila amejaribu kutoa ufafanuzi and according to him all is well. Hata hivyo tatizo la CHADEMA linabakiwa kwenye mawasiliano hafifu (poor communication). Naamini kwa sasa hii role imechukuliwa na Mnyika lakini wakati umefika kwa CHADEMA kuwa na mtu (professional) ili afanye kazi ya mawasialino -full time. Mnyika ni mbunge ana watu zaidi ya laki 4 ubungo wanaomhitaji, bado ana kazi nyingine za kichama. Hivyo anaweza, ndiyo, ku-oversee mawasiliano lakini kama nilivyosema kuwepo na mtu - full time.

  Na kunapokuwa na issue -propaganda or not, basi wajibu haraka and move on. Kwa sasa wanazongwa sana maana wabunge ni wachache , kazi nyingi, mamluki nao wanazidi kuongezeka. Hata hivyo kuna haja ya kuimairisha kitengo cha mawasiliano hasa sasa wakati Wassira na wenzake wameaamua kupindisha mada.

  Kwenye ugomvi wa ndani. Si vibaya wakawa wanafanya scanning mara kwa mara, virus ni tatizo la siku zote!
   
Loading...