Ningekuwa na Ndoto ya Urais 2015 ndani ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa na Ndoto ya Urais 2015 ndani ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumba-Wanga, Mar 23, 2012.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Najiuliza kama ningekuwa na ndoto ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015 ningefanya nini?
  Ningeeleza mambo ambayo yangewavutia wapiga kura wangu ili wanichague. Ningewasaidiaje watanzania ili waondokane na umaskini waliona leo? Haya ni baadhi ya mambo ambayo nafikiria ningejipanga kuyakabili:

  1) Jinsi nitakavyoshughulikia swala zima la ufisadi ambalo limekuwa ni tatizo kubwa kwa maendeleo ya taifa letu

  2) Jinsi ya kukuza sekta kuu katika uchumi wetu;

  a) Madini: jinsi ambavyo wataznania watafaidika na madini yetu, tofauti na ilivyo sasa mbavyo wawekezaji ndio wanaofaidika zaidi, na kuacha wananchi wakitaabika
  b) Jinsi ya kukuza Kilimo ambao ni muhimili wa uchumi wetu: kwa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo na kupunguza tegeemzi la jembe la mkono. Jinsi ya kuongeza productivity na masomo ya mkulima (kama kutumia MVIWATA model katika masoko ya wakulima wado wadogo). Kwa kufanya hivi, tungeongeza kipato na ajira vijijini, na SWALA LA MAISHA BORA KWA WOTE lingekuwa na mwanga.
  c) Utalii: Jinsi ya kukuza sekta ya utalii na kuepuka kupgwa bao na Wakenye wanaotumia rasilimali zetu kama Mlima Kilimanjaro kwa faida yao.

  3: kuongeza mapato ya serikali kwenye Kodi: Kuwabana zaidi wafanya biashara wakubwa walipe kodi wanayostahili ili kuwapa nafuaa wananchi wa kawaida ambao wamebebesha mzigo mkubwa wa kulipa kodi, na kuongeza uwezo wa serikali kuwasaidia wananchi wake katika

  a) Kuwahudumia kwenye huduma muhimu za jamii
  b) Kuwalipa mishahara wanayostahili na kwa muda wake
  c) Kuongeza ajira kwa vijana


  Kwa kuanza na haya mammbo makubwa 3, kutakuwa na mwanga kwenye tunnel.

  Haya ni baadhi tu, the list is endless

  4)

  5)
  6)
  7)
   
Loading...