Ningekuwa Mwenyekiti wa CCM ningefuta mchakato wa kura za maoni na kuanza upya

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Mchakato wa kura za maoni ulitawaliwa na vitendo vya Rushwa kwa wajumbe wa mkutano kiasi kwamba aliyetoa pesa nyingi kwa wajumbe ndiye aliyepata Kura nyingi.

Kwa mantiki hii, wagombea wote waliofanikiwa kujizolea kura nyingi Ni wale ambao kwa kutumia utajiri wa pesa walionao waliofanikiwa kuwahonga wajumbe ambao wengi wao wanaishi katika umaskini wa Hali ya juu.

Maamuzi haya ya wajumbe yamesababisha kurudi kwa watu wale wale ambao wamekuwa wakilalamimiwa kushindwa kuleta maendeleo katika majimbo yao.
 
Ulikuwa huko? Wengi walioshindwa wanapesa sana na pia wengine wamekuwa serikalini. Sema kama unamtetea ambayo nirushwa pia
 
umeandika ukweli mtupu, angalia majimbo km karatu, mbulu mjini, mbulu vijijini, hanang hata babati mjini wote ni ngombaru elimu sifuri eti ndio wabunge. watawezaje kuchangia muswada au budget vitu ambavyo vimeandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu. sijaona aibu km hii ktk nchi hii. wengine hata hawajafika darasa la saba. wajumbe wa CCM hayo matumbo yenu yasiyoshiba ni maangamizi yetu.
 
Peleka ushahidi wako Takukuru ili hao uliowaona wakitoa na kupokea Rushwa wachukuliwe hatua. Ingawa naona kama umechelewa kdg maana ingependeza zaidi pale tu ulipoona hivyo vitendo vya rushwa ulipaswa utoe taarifa, badala ya kuja kusema leo wafute kura kwa vile wewe uliona watu wakishindana kutoa rushwa.
 
Kama TAKUKURU wangekuwa na Nia ya kupambana na Rushwa wangeweza kukamata karibu wote waliotia Nia. Kwa hiyo itoshe kusema kuwa wahongaji walianzia TAKUKURU huko huko Kisha Waka kumalizia na Wajumbe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom