Ningekuwa mimi nisingethubutu kumsogelea huyu Mama Mjane

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Katika hali ya kushangaza mno, Musiba kaibuka na video ya vitisho na kejeli kwa wale walioenda kumpokea Lissu.

Si nia yangu kuongeza post za huyu mtu, lakini huu ni mtazamo tofauti hasa kwenye nyanja nzima ya tafakuri kwenye matumizi ya vinywa vyetu na kalamu zetu

Tukumbuke maandishi hayafutiki na neno ni kama risasi, likitoka halirudi. Ni chini ya mwaka mmoja Musiba alitoa tuhuma na shutuma za wazi zilizojaa kejeli na dharau kwa marais wastaafu na wake zao, akimtoa mwalimu Nyerere kwamba walikuwa wezi wakubwa

Clip ile ilipelekea malalamiko rasmi chamani lakini hakufanywa kitu, aliachwa aendelee tu kumtuhumu na kumdhihaki kila aliyeona inafaa kufanya hivyo kwa maslahi anayojua mwenyewe.

Leo hii mmoja wa watuhumiwa wake, Mzee Mkapa, kafariki. Tayari keshasahau yote na amejibeba mzima mzima kwenda kwa mama Mkapa.

Sikiliza video hii kisha tazama na hiyo picha hapo chini.



Ni wazi Musiba kama hana msongo mkubwa wa mawazo basi ni mgonjwa wa akili anayehitaji matibabu ya haraka, maana si kwa unafiki ule aliouonesha kwenye kifo cha mzee Mkapa.

Kuna swali muhimu ambalo watu wanajiuliza lakini hawajapata jibu mpaka leo:

NI NANI YUKO NYUMA YA CYPRIAN MUSIBA?

Screenshot_20200729-032001.jpg
 
Mshana Jr yaani umeshindwa kumshangaa Magufuri na hotuba yake ya sifa kwa mkapa wakati kila siku amekuwa anatuambia "WALIOPITA MBONA WALIKUWA HAWAFANYI" unakuja kushangaa mouth piece yake?
Kitabu cha Mithali kimetuasa kuwa werevu kama nyoka....zamani tukiwa form one wakati huo tukijifunza lugha ya kiingereza nilisoma kitabu kimoja kizuri sana kinaitwa LIKE FAZA LIKE SON..Yale maudhui yanaishi hata leo
 
Mshana Jr yaani umeshindwa kumshangaa Magufuri na hotuba yake ya sifa kwa mkapa wakati kila siku amekuwa anatuambia "WALIOPITA MBONA WALIKUWA HAWAFANYI" unakuja kushangaa mouth piece yake?
Hivi hapa nchini kuna hotuba yoyote ambayo inamsema vibaya marehemu? Hasa kwa hawa watu mashuhuri nchini?kila binadamu ana makamilifu na mapungufu yake,ni kawaida kwenye wasifu wakati wa kumpumzisha mtu kwa safari ya milele kumuelezea wasifu wa upande wa mazuri yake.

But kwanini kila mtu mwenye mapungufu na mambo ya ajabu katika matendo yake lawama zinamuendea mh.Rais?,mfano huyu musiba.. kwamba anatumwa na system au magufuli? Hivi kina maneno ambayo huyu mzee magu anashindwa kutamka kavukavu bila chenga? .
 
Back
Top Bottom