Ningekuwa mimi ndio Magufuli kipindi hiki cha lala salama ningemwaga ajira za kutosha kila sekta

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,548
6,102
Kama mtakumbuka Kikwete zilipokuwa zinakaribia hizi dakika za majeruhi au za lala salama alikuwa na mtindo wa kumwaga ajira nyingi sana kila sekta. Sio kwamba alikuwa anatoa rushwa hapana ila hakutaka kuishi kwa mazoea maana huwezi jua ni nani anayefuata baada ya uchaguzi.

Hivyo alitoa ajira nyingi na kuboresha maslahi ya wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kwani hakutaka kuondoka huku akiwaacha vijana na wananchi wakimlalamikia that way mwamba mpaka leo hasahauliki kizembe kwenye mioyo ya watu kwani aligusa sana maisha ya watu kuliko vitu.

Magufuli na wewe fuata nyayo za mzee Kikwete sio tu kwa ajili ya kushinda uchaguzi lakini pia kuacha alama. Leo hii Kikwete ameacha ameajiri walimu wengi, polisi wengi, wanajeshi wengi, madaktari wengi, manesi wengi, askari magereza wengi yaani watumishi wengi ambao hawa wote wanamkumbuka.

Tusiishi kwa kukariri maana hakuna aijuaye kesho yake. No one know tomorrow.
 
Hivi kwa roho mbaya aliyonayo huyu msukuma unafikiri anaweza kuyafanya hayo? ,anapenda yeye ndoo apate posho nzuri na mishahara minono.
 
Then atawalipa nini wakati hazina imekauka na akili ya kutafuta pesa hana?
 
Back
Top Bottom