Ningekuwa Mh. Mbowe; Kipande cha Hotuba yangu ya Leo Kingekuwa Hivi…… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa Mh. Mbowe; Kipande cha Hotuba yangu ya Leo Kingekuwa Hivi……

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by English Learner, Apr 7, 2012.

 1. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  ……….. …………

  “Ndg. Wananchi, sisi viongozi wa Chadema tunaishukuru sana ccm, serikali yake na vyombo vyake vyoote vya dola. Tunawashukuru kwa jinsi wanavyotusaidia kuujulisha umma kwa vitendo kuwa dhamira ya chama cha mapinduzi:


  • Si kulinda mali na rasilimali za nchi hii bali kuzitelekeza na kuziteketeza!

  • Si kumkomboa Mwananchi bali kumkomoa!

  • Na wala hawapo kwa ajili ya kulinda na kutetea haki zako wewe Mwananchi, bali wapo kuhakikisha hautambui haki zako, na kama haujaelimika ubaki mjinga ili wakutawale milele bila kelele!

  Awali tulipowaambieni hayo ndo malengo na undani wa ccm, wachache walituelewa haraka na wengi polepole wanaendelea kutuelewa. Kumbukeni jinsi Dr. Slaa alivyodhihakiwa baada ya kutoa orodha ya Mafisadi pale Mwembeyanga, kumbukeni jinsi Mh. Zitto Kabwe alivyoadhibiwa na Bunge kwa kufichua Uchafu wa Mawaziri wa ccm, kumbukeni jinsi wananchi wa Zanzibar, Mbeya, Tabora na hapa Arusha walivyokutana na dhahama katika kutetea maamuzi yao na kuutumia uhuru wao wa kikatiba wa kuchagua viongozi wawapendao.  CHADEMA tungekuwa waongo, ccm hata isingekiri baada ya uchaguzi Mkuu kuwa ndani yake si kama kuna mafisadi tu, bali kuna yale yaliyokubuhu, yenye MAGAMBA mazito yaliyoshindikana hata kuvuliwa. Msingesikia kesi (japo gheresha) za EPA. Hata hiyo dharau ya majambazi kurudisha pesa na yasijulikane wala kuchukuliwa hatua za kisheria isingetokea. Viongozi wa CHADEMA wangekuwa waongo, leo hii Dr. Slaa angekuwa gerezani akiwa anatumikia vifungo vya kesi zaidi ya 100, Badala ya Nazir Karamaghi kupotea kabisa kisiasa Mh. Zitto ndiye angepotea, Mbowe naye sijui angekuwa wapi? Lakini kubwa zaidi vijana kama Lema, aliyethibitisha uongo wa Waziri Mkuu tena mbele ya Bunge, kijana kama Lema aliyesimama upande mmoja na wanyonge katika kutetea haki, kijana ambaye sasa kila Mtanzania anamfahamu kama mtu hasiyetishwa na maji ya pilipili, mabomu ya machozi, gereza, kisu, risasi na wala haongeki kwa pesa au cheo! eti serikali-ccm kwa kutumia Mahakama inaamua kumuondoa katika siasa na harakati za ukombozi kwa kipindi wakitakacho wao! Thubutu…haiwezekani na kamwe haitawezekana! Peoplesssss…………


  Makamanda, tuwaambieni ccm, kwa mara nyingine tena imekula kwao! Ilikula kwao na inazidi kula kwao kwa kumbeza Dr. Slaa mara zote, ilikula kwao kwa kumsimamisha Mh. Zitto ubunge, ikala kwao kwa kuwapeleka Wanafunzi wa Elimu ya juu likizo ili wasishirikia uchaguzi Mkuu, inazidi kula kwao kwa kudandia hoja ya Ufisadi huku MAGAMBA magumu yakiwa yamewakwama, mchakato wa Katiba Mpya utakaa sawa na kula kwao, na sasa tunasema na hili la Mh. Lema ishakula kwao! Tunao ujasiri wa kusema kwa hakika kuwa imeishakula kwao kwa sababu CHADEMA daima inasimama na matakwa ya Haki za Wananchi. Na kwa sababu hiyo, ndo maana nanyi daima mnatupa nguvu kwa kutambua kuonewa kwetu na kutupa moyo kwa hali na mali. Vivyo hivyo nasi tunapigana juu ya kuonewa kwenu, kudhulumiwa kwenu na ubadhilifu wa rasilimali za nchi yetu.


  CHADEMA inao na bado inawahitaji sana vijana jasiri kama Mh. Lema. Hasa katika kipindi hiki ambacho tayari Wananchi mmetuhakikishia kutwaa dola hapo mwaka 2015, CDM inahitaji sana nguvu kazi ya watu wanaojituma kama Mh. Lema. Tunaishukuru mahakama ya ccm kwa kutoa kibali kinachompa Mh. Lema muda wa kutosha kukiimarisha chama nje ya Arusha. Mh. Lema tutakuomba likizo yako ikiisha upelekee Taarifa ya Kazi kwa Mzee Mkama na Nakala kwa M/Kiti Kikwete. Mh. Lema, chama kitakupa jukumu jipya. Toka sasa Jimbo lako la Utumishi litakuwa Tanzania nzima. Kwa kadri Allah atakavyokuwezesha, utakwenda kila mkoa, kila wilaya, kijiji na kila tarafa. Ukaamshe, uanzishe, uimarishe na kukomaza fikra za ukombozi. Hii kampeni yako itaitwa “Operation Ukombozi” ………………………………….”
   
 2. v

  vngenge JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Amalizie mkimtoa lema wapo vijana elfu kama lema
   
 3. m

  mtolewa Senior Member

  #3
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  yap umenena kama vile ulikuwepo.
   
 4. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Imekaa vyema mkuu
   
 5. k

  kitero JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na hoja.Ila natumaini Mh Mbowe atakuja najambo kubwa sana leo na lenyekutoa mwanga kwa Arusha inayonyemelewa na magamba.siku zote njiwa ni wajuu akija chini atarudi juu ila chura siku zote ni wakwenye matope siku zote hawezi kuwa msafi kama njiwa.peoplessssssssssssssss.......................
   
 6. S

  Saitoti Member

  #6
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu imetulia ,
   
 7. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mkuu safi sana!
   
 8. N

  Nelia Member

  #8
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bila shaka Mh. Mbowe amepata mchango wako wa mawazo. Safari ya ukombozi ndio imeanza.
   
 9. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  sure... CDM ujumbe wao utakuwa mzito na mrefu. Hiki ni kipande tu kama nilisema awali.

  Pendekezo jingine: CDM ituweke bayana kama Kanumba katika maandalizi yake kugombea Ubunge Shy-Twn alikwishafanya mazungumzo na viongozi wa CDM. Kama ndiyo, basi gwanda la wiki hii kuanzia mkutano wa leo liwe JEUSI.
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Fantastic point.
   
 11. n

  nzanga Member

  #11
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  iko poa sana,lakn kwa nimjuavyo kamanda mbowe atakuja na kali zaidi ya hii,kifupi chadema ni party ya vision tz
   
 12. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,138
  Likes Received: 10,495
  Trophy Points: 280
  imenigusa sana naamini leo hotuba zitakazo tolewa na makamanda zitakuwa ni za ukombozi na kuonesha udhalimu wa ccm.
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Apr 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Uzi mzuri sana English Leaner.
  Watu wanasubiri kwa hamu Mbowe atasema nini kwa mustakbali wa Arusha na Lema!
   
 14. Micha

  Micha JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sound good, tafuta jimbo 2015 itakuwa ni kuchukua tu maana CCM itakuwa hoi kabisa!
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Sasa ndo umeandika nini!
   
 16. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Chadema tuna mungu bali wao ccm wana mahakama, polisi na amri.
  MUNGU MMOJA WA KWELI NDIO MUNGU WA CHADEMA.
   
 17. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  karibu sana JF kwa another new ID, well done kaka. But vipi kuhusu arumeru nasikia CCM mlishinda.?
   
 18. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Tutakutafutia nafasi ya kuandika na kuedit hutuba ya Kamanda wetu safi sana
   
 19. b

  boscomark New Member

  #19
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aitangazie NEC ipange haraka tarehe ya uhaguzi mdogo Arusha mjini ili magamba yavuliwe maana ccm wameshindwa kuwavua, hatuna haja ya kukata rufaa na Lema atarudi kwenye jimbo lake!!!!
   
 20. L

  Lsk Senior Member

  #20
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...iko vizuri. Ningelikuwa ni mchadema wa nafasi,ningelikuhakikishia kukuwekea kabenchi kako pale kwenye ofisi kuu ya chama-kitengo cha habari
   
Loading...