Ningekuwa Mfanyakazi wa Serikali ningejipatia $10,800 for 20 days. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa Mfanyakazi wa Serikali ningejipatia $10,800 for 20 days.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Oct 12, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Wana Jf,

  Nilipata kisafari cha kikazi nje ya nchi kwa wiki tatu hivi, nimerudi juzi so weekend hii nikawa kijiweni kwetu nikawa nachat na rafiki yangu anayefanya kazi serikalini ambaye ngazi yake ni Principal officer akaniambia ungekuwa mwajiriwa wa serikali ungerudi na ka kitita ka pesa kama dola 10,800 kwa hizo siku 20 ulizokuwa nje ya nchi, akaniambia perdiem ya serikali ni $540 kwa siku kama ulikuwa hujui, sikuamini sababu huwa sifuatilii mifumo ya malipo serikalini.

  Akaena mbali zaidi akaniambia kwa mwezi mtu anajipatia hadi 3m kwa vikao na posho tu achilia mbali mshahara wake. Hapo nikacheka nikamwambia ki ukweli unaridhia malipo haya kwa wafanyakazi wa umma? akaniambia ndugu yangu serikalini kuna PESA acha mchezo.

  Kwa hiyo ndugu zangu leo hii ningekuwa na karibia dola 10,000 mfukoni kwangu. aisee kile kiwanja changu kingenikoma ule ujenzi ningeupita fasta fasta.

  Nilichojifunza hapa ni kwamba serikali ina pesa nyingi sana, na sijui wamepigaje hizi hesabu na kujilipa kiasi hiki kwa siku, tena unakuta mfanyakazi kalipiwa Malazi tayari.

  Sina wivu na ndugu zangu mnaofanya kazi serikalini lakini kumbukeni haya ndiyo matumizi mabaya ya pesa za umma ki ukweli. na ndiyo maana wengi wenu hamtaki JK na CCM itoke madarakani kwani hii ndiyo mifumo itakayofumuliwa.
   
Loading...