Ningekuwa Meya wa Arusha ningejiuzulu kuepusha maumivu na maafa mengi zaidi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Nadhani 'Meya" Gaudence Lyimo anatambua kwamba yote haya yanatokana na yeye kuwa 'Meya' kwa njia ambazo hazikuwa za halali na kendelea kung'ang'ani wadhifa huo. Sijui ni Wanarusha wangapi wamesha poteza maisha kutokana na 'umeya' wake na nashangaa iwapo atakuwa ana peace of mind hasa akijua yote hayo yanatokana na yeye.

Na sidhani iwapo viongozi wakuu wa CCM akiwemo JK anaweza kumwambia ili kuepusha damu zaidi kumwagika "tafadhali achilia ngazi -- nitakutafutia mlo mahali pengine."

INASIKITISHA SANA!
 
Huo ungekuwa uamuzi mzuri sana kwake, lakini hawezi kufanya hivyo kwa sababu ya tumbo
 
Kwake ni kama tambiko, si unajua hii ni Afrika Bana, wala hawezi kushtuka kwani anatimiza matakwa ya wakubwa wake.
 
umesema kweeli.. yote haya yasingetokea kama uchaguzi wa meya ungefanyika kwa kufuata utaratibu stahili. pia namlauumu Pinda aliyetetea uasi huo hadi bungeni bila aibu..
 
Nadhani 'Meya" Gaudence Lyimo anatambua kwamba yote haya yanatokana na yeye kuwa 'Meya' kwa njia ambazo hazikuwa za halali na kendelea kung'ang'ani wadhifa huo. Sijui ni Wanarusha wangapi wamesha poteza maisha kutokana na 'umeya' wake na nashangaa iwapo atakuwa ana peace of mind hasa akijua yote hayo yanatokana na yeye.

Na sidhani iwapo viongozi wakuu wa CCM akiwemo JK anaweza kumwambia ili kuepusha damu zaidi kumwagika "tafadhali achilia ngazi -- nitakutafutia mlo mahali pengine."

INASIKITISHA SANA!

Haaa kwani uyo meya ndo anaua watu?
 
Kwa nini usiseme Chadema ndio chanzo kwa sababu ya kugombea kitu cha umeya kinguvu?
 
Nafikiri, haya matatizo na maafa yote yasingetokea Kama taratibu zote stahili za kumchagua meya wa Arusha mjini Gaudence Lyimo 2010 zingefuatwa. Hivi huyu Lyimo anajisikiaje kwa haya yanayotokea? ana amani moyoni mwake? kama huu umeya ni halali yake, Mungu ambariki sana pamoja na Pinda, lakini kama utaratibu ulichakachuliwa, damu hii itamlilia Lyimo na Mungu atajibu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom