Ningekuwa Magufuri ningefanya haya,ili kuepusha kelele

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,589
2,000
Kwanza tunatakiwa tujue na kutambua kwamba kulalamika na kutoridhika ni hulka ya mwanadamu tangu enzi za zamani kabla ya kristo.mfano ni jinsi wana wa Israeli walivokuwa wanamlalamikia Musa alipokuwa anawatoa Misri.ilifikia wakati wanamwambia "bora ungetuacha kwa farao",na kuna wakati MUNGU aliwaambia watakula bila kufanya kazi ila wao wakaanza lawama"haiwezekani tule bila kufanya kazi"...hii inatujuza kwamba mwanadamu ni mtu wa kutoridhika na ndii ameumbwa hivo.hata yule kijana pia aliacha mali na utajiri kwa baba yake akaenda huko mbali(ughaibuni) kuishi kwa shida.hii ni funzo tu kwamba mwanadamu haridhiki hata umpe nini,umpe majumba,fedha na mkate wa kila siku ila haridhiki.sasa mimi ningekuwa ni Magufuri ningeruhusu mikutano ya vyama vya siasa(maana havina madhara na haiwezekani kufanya mikutano kila siku)
Pia ningeonesha bunge live maana hakuna madhara
Ningeruhusu watu wanikosoe ila kwa kunijenga na sio kudhalilishana maana uraisi ni taasisi pana haifai kuidhalilisha
Ningewaambia wabunge walete muswada wa vyombo vya habari mzuri,ningepeleka zile milioni 50 kila kijiji ili kuwaziba mdomo wapingaji,kila mwanafunzi angepata mkopo ilimradi tu kafaulu vizuri.ningetoa ajira za kumwaga..sasa sijui hapo ningesemwa kwa lipi? Je wewe ungekuwa ni Magufuri ungefanyaje?ili wapinzani wakose hoja?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom