Ningekuwa Magufuli, ningemrudisha balozi wa Msumbiji nyumbani

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,281
6,697
Kwa watu ambao hawajawahi kuishi Msumbiji wanaweza kuhisi kuwa Watanzania wanaofukuzwa huko ni wale ambao wamekosa uhalali tu, Si Kweli nimeshuhudia mara kadhaa watu wakichaniwa hati zao za muda na askari wa Msumbiji, Kilichokuwa kinaheshimiwa ni pasport kubwa tu!

Kwa taarifa niliyonayo mpaka sasa ni kuwa hata hizo pasport kubwa wananyang'anywa, Pamoja na msaada mkubwa ambao serikali ya Tanzania imeufanya kwa nchi ya Msumbiji lakini ni wazi kuwa askari wa Msumbiji wamekuwa na chuki kubwa na Watanzania kuliko Taifa lolote jingine, kwa wale ambao wamevuka mpaka wa msumbiji watakubaliana na mimi kuwa askari wa Mozambique hata kama utatimiza vigezo vyote bado watahitaji fedha kwa namna fulani ya kulazimisha.

Mheshimiwa Magufuli, hawa watu tumewavumilia kiasi cha kutosha,hakuna haja ya kugombana nao, tuwaoneshe tu kuwa na sisi tunaumia kwa yale wanayotutendea, Mrudishe balozi wetu nyumbani.

Kama Rais wa nchi unajisikiaje unaposikia raia wako wanabakwa na Askari wa nchi ambayo inajinasibu kuwa ni RAFIKI?
 
Hapa Tanzania kuna raia wa Msumbiji maelfu kwa maelfu na wengi wana vitambulisho vya kupiga kura hapa Tanzania na wakati wa uchaguzi wa Msumbiji wanapiga (kwa maandalizi ya ubalozi wao) kura kuchagua Rais wa Msumbiji. Nendeni sehemu nyingi wanapoishi utawakuta na wengine ni viongozi/wajumbe wa serikali za mitaa! Mhe Makonda ndiye atakayeweza kazi hii kwani mambo ya ndani.........polisi na uhamiaji!!!!!! are dormant.
 
Kwa watu ambao hawajawahi kuishi Msumbiji wanaweza kuhisi kuwa Watanzania wanaofukuzwa huko ni wale ambao wamekosa uhalali tu, Si Kweli nimeshuhudia mara kadhaa watu wakichaniwa hati zao za muda na askari wa Msumbiji, Kilichokuwa kinaheshimiwa ni pasport kubwa tu!

Kwa taarifa niliyonayo mpaka sasa ni kuwa hata hizo pasport kubwa wananyang'anywa, Pamoja na msaada mkubwa ambao serikali ya Tanzania imeufanya kwa nchi ya Msumbiji lakini ni wazi kuwa askari wa Msumbiji wamekuwa na chuki kubwa na Watanzania kuliko Taifa lolote jingine, kwa wale ambao wamevuka mpaka wa msumbiji watakubaliana na mimi kuwa askari wa Mozambique hata kama utatimiza vigezo vyote bado watahitaji fedha kwa namna fulani ya kulazimisha.

Mheshimiwa Magufuli, hawa watu tumewavumilia kiasi cha kutosha,hakuna haja ya kugombana nao, tuwaoneshe tu kuwa na sisi tunaumia kwa yale wanayotutendea, Mrudishe balozi wetu nyumbani.

Kama Rais wa nchi unajisikiaje unaposikia raia wako wanabakwa na Askari wa nchi ambayo inajinasibu kuwa ni RAFIKI?

Kwa sababu ya umaskini unaoielemea Dunia, kipindi hiki ni hatari sana mtu kuishi na kujijenga kwenye Taifa lisilo lake maana dunia inavaa upya sera za ukabila na utaifa uchwara!
 
inasikitisha sana mimi kiukweli nimeshawahi kuishi msumbiji wale jamaa kwa kifupi wana ROHO MBAYA SANA,

haya mambo mnayoyasikia hayakuanza leo wala jana yalianza muda mrefu sana watanzania kufanyiwa unyama .

kuna mwaka flani nyuma cha mji wa BEIRA kuna watanzania walitupwa kwenye MTO WENYE MAMBA WAKALIWA KAMA samaki
 
ingekuwa enzi Jk na membe sasa hivi ungepigwa msako wa nyumba hadi nyumba
raia wote wa msumbiji wangeondolewa na kurudishwa makao.

nakumbuka kipindi kile cha wanyarwanda walivyoleta chokochoko walikiona cha mtema kuni
 
Kwa watu ambao hawajawahi kuishi Msumbiji wanaweza kuhisi kuwa Watanzania wanaofukuzwa huko ni wale ambao wamekosa uhalali tu, Si Kweli nimeshuhudia mara kadhaa watu wakichaniwa hati zao za muda na askari wa Msumbiji, Kilichokuwa kinaheshimiwa ni pasport kubwa tu!

Kwa taarifa niliyonayo mpaka sasa ni kuwa hata hizo pasport kubwa wananyang'anywa, Pamoja na msaada mkubwa ambao serikali ya Tanzania imeufanya kwa nchi ya Msumbiji lakini ni wazi kuwa askari wa Msumbiji wamekuwa na chuki kubwa na Watanzania kuliko Taifa lolote jingine, kwa wale ambao wamevuka mpaka wa msumbiji watakubaliana na mimi kuwa askari wa Mozambique hata kama utatimiza vigezo vyote bado watahitaji fedha kwa namna fulani ya kulazimisha.

Mheshimiwa Magufuli, hawa watu tumewavumilia kiasi cha kutosha,hakuna haja ya kugombana nao, tuwaoneshe tu kuwa na sisi tunaumia kwa yale wanayotutendea, Mrudishe balozi wetu nyumbani.

Kama Rais wa nchi unajisikiaje unaposikia raia wako wanabakwa na Askari wa nchi ambayo inajinasibu kuwa ni RAFIKI?
Wakati wa Opation ya kuwarudisha Wanyarwanda,rundi na raia wengine wa nchi jirani kwao chini ya kivuli cha [HASHTAG]#tokomeza[/HASHTAG] Ujangili mbona hakuna nchi ilirudisha balozi wake kwao, au wale raia wao hawakuwa na haki binadam?
 
Wakuu, kwani ni msumbiji ipi? Ni hii msumbiji ambayo wazazi wetu na mababu zetu walienda kumwaga damu ili kupambana na mkoloni aondoke huko msumbiji?

Ni msumbiji hii ambayo Samola Macheli alienda kambi ya Jeshi Kongwa huko Dodoma na kuweka kambi akisubiri msaada wa Hayati Mwalimu Nyerere ili apate uhuru nchini kwake?

Watanzania tumeshindwa kujiheshimu na sasa hata majirani hawatuheshimu.
 
Ukiwa kiongozi halafu hujui uwafanyie nini wananchi ni tatizo kubwa. Kuwalinda raia wako siyo kwamba unawapa hisani bali ni wajibu wako wa kwanza. Haiwezekani watu wako walalamike kuonewa wewe umekaa kimya. Hii inamaanisha upo pale kwa makosa. Ni kama kughushi uongozi.
 
Moza hawajafukuzwa watanzania tu. Wapo raia toka nchi mbalimbali. Tetesi ni kwamba lile jeshi ya uasi lipo kwenye recruitment processes ili waupige down uongozi uliopo. Na raia wa nchi nyingi wanakubali kuwa recruited maisha magumu. Kwahiyo moza walipofanya utafiti wakaona kideal na mmoja mmoja ingeleta picha mbaya kwahiyo raia wote upande wa mkwepeshi kupanda kule waasi walipojificha kwenye misitu minene wanaondolewa tena na jeshi. TETESI
 
Swala la kibali ya kuishi au kufanya kazi ni muhimu na lazima hata kama ni jirani yako au rafiki sheria ni sheria. Tuna waandishi wa habari na wanahabari mi nashangaa hata kushughulikia suala hili kujua ukweli wameshindwa ila wamebaki na siasa za ndani. Wanahabari wameshindwa kumhoji balozi wa msumbiji tanzania, wameshindwa kuvuka border kwa vibali vya uanahabari ili kwenda kufuatilia na kuhoji sehemu za matokeo na kwenda wizara ya ndani na nje ya msumbiji, hii nayo imewashinda? Tusibakie kuzungumza maneno ya "hearsay"
 
Subiri Mkuu. Usiogope utasikia soon. Kwa hiyo usiwe na papara ndugu. Yaani Jambo litokee na mara moja action. hatuendi hivyo kuna uchunguzi, kujiridhisha then action.
 
Ukisoma Bible kitabu cha Mwazo utakuta story ya Israel kuhamia nchi ya Misri kutoka nchi ya Kanani. Story inaeleza kuwa Mara baada ya wana wa mzee Yakobo(Israel) kumuuza ndugu yao Yusuf kwa watu wa misri, na Yusuf kupewa cheo cha uwaziri mkuu na farao, ilitokea njaa huko kanani ambapo ililazimika mzee Yakobo na wanawe 11 kuhamia Misri NA FARAO ALIYE MJUA VEMA YUSUF ALIWAKARIBISHA NA WALIISHI MAISHA YA RAHA MSTAREHE lakini Mara baada ya kufa yule farao na Yusuf alitokea farao mwingine asiye mjua Yusuf ambapo aliwatesa sana wana wa Israeli kwa kuwageuza kuwa watumwa hadi walivyo kuja okolewa na Mungu kupitia kwa MUSA. Ndilo linalotokea huko msumbiji kwa ndugu zetu watanzania. Nani asiyejua jinsi watanzania walivyo shiriki kupigania Uhuru wa msumbiji? Kuna askari wangapi wa kitanzania walikufa wakipigania Uhuru wa nchi hiyo? Ninahisi labda ametokea farao asiye mjua Yusuf ndiyo maana hayo yanatokea na kuwapata ndugu zetu
 
Back
Top Bottom