Ningekuwa CUF Ningerudisha "Kadi" na "Kukana" Uwanachama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningekuwa CUF Ningerudisha "Kadi" na "Kukana" Uwanachama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by niweze, Dec 28, 2010.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kutokana Yote Tunayafahamu Mpaka Sasa, Sharif Alipanga Kurudi CCM kwa Kupitia Njia ya Uchaguzi. Kawaida Wapinzani Dhaifu Wanarudi CCM kwa Njia ya Kutangaza Habari Maalumu Ila Sharif Ametumia Tactic Mpya ya Kukiua Chama Chake. Wananchi Tunajua Jinsi Gani Sharif Alikuwa Tayari Kupigana Alipoambiwa Kashindwa 2005 Leo Hii Tunaona Tofauti. Huu Uchaguzi wa Visiwani Unaonekana Kabisa CCM Walishindwa Sana na CUF Ila Kilichoshangaza Sharif Alikubali Haraka Sana Kupata Ofisi ya Makamu wa Raisi. Hii ni Tamaa Yake ya Madaraka na Visiwani Watajuta. Lipumba Mwenyewe Kapatwa Butwaa Aliposikia Kwenye Habari Sharif Kakubali Matokeo. Kwa Kifupi Bara, CUF Imekufa na Tunaona Wabunge Wao Hawana la Kufanya Ila Kuingia Kwenye Vikao vya CCM na Kukubali Kila Hoja ya CCM. CUF Imeingizwa Kwenye Vitabu vya Malipo vya CCM Hata CCM Wenyewe Hawakuamini Ingekuwa Raisi Hivi, the Strategy Work. Hizi Ndio Siasa za Visiwani, Hakuna Jipya Huko Issue Yao Kubwa ni Kujitenga. Wananchi Bara Mpaka Leo Hatujui Malengo ya CUF na Upinzani Wao Hauleweki Inchini. Kwa Wale Mnaotaka Kupeleka Mijadala Kwenye Udini, Hii Sio Nafasi Yenu Jitete na Hoja Yako Mwananchi... Kitu cha Kuuliza Wananchi Bara, Kuna Haja ya Tujali Sana Hatua za CUF Visiwani? Wanatupa Faida Yeyote
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe unayejiita Niweze yaelekea huelewi kitu. unajua seif alichokuwa akikidai zanzibar? au unarukia tu gari kwa mbele. Utagongwa.
  Lakini pia na lingine, je wajua kura za wabunge majimbo yote zilikuwa tayari zimeshatangazwa kabla ya saa 6 mchana? kwa nini urais ulitangazwa saa 5 usiku wakati ilikuwa ni hesabu ya kujumlisha tu hata mtoto wa darasa la 3 angefanya? Je wajua kuwa usiku kabla ya uchaguzi generali mwamnyange alikuwa zanzibar kuongea na amani karume, ulijua alienda kufanya nini na aliongea nii na amani? Je wajua mkapa na mwinyi walienda mchana zanzibar? walienda kufanya nini? unakumbuka siku ya kufunga kampani pale jangwani mkapa alisema nini?
  ukijiuliza haya yote then hutaleta thread ya kijinga kama hii hapa jf. seif na CUF si wajinga kiasi hicho. they know, what they are doing.
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ngwendu Wewe Kweli Jina Lako Linafanana na Maswali Unauliza. Kama Hutaki Wananchi Tujue Unamaanisha Nini Hayo Maswali na Unatuuliza Sisi. Sasa Wanajamii Tukuelewe Vipi? Tuelimishe na Kama Umesoma Hii Comment Ungejua Sharif Haeleweki na CUF Yenyewe Inawachanganya CUF-Bara. Tunaomba Maoni na Majibu Sio Maswali. Hakuna Sababu Yeyote ya Maana Ilimfanya Sharif Akubali Matokeo ni "Sale Out Thats It" Wanasiasa Wanaowadandanya Watanzania Kuwa Wanawajali Kumbe Nini Uroho wa Madaraka na Wizi wa Fedha.
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280

  Huyu amenisaidia kujuwa kwa nini shuleni kuna division za ufaulu, nimerudia kuisoma comment hii kwa zaidi ya mara 10 lakini bado sijaelewa, labda mnisaidie wadau maana Thread iko very clear inaeleweka, lakini huyu ngwendu kazi hipo. lakini hivi JF inatumia vigenzo gani kutoa hizi rank? eti mtu ni JF senior expart member alafu cha kushangaza anazidiwa mada na coment nzuri na junior member, mimi nashauri JF iangalia upya jinsi ya kutoa hizi rank.
  maana sasa hivi moderm zimeshuka bei sasa mtu akiwa na laptop yake tu basi huyo nae ni Great thinker, mimi binafsi ilinichukuwa miaka4 mpaka kujiunga na JF nilikuwa ni guest tu nafunguwa JF nasoma michango ya watu basi naenda kwenye web nyingine, lakini leo hii humu kuna watu utazani wanawashwa kwenye makalio yao, yaani hata kama hana cha kuchangia ili mradi tu na yeye aonekane eti yupo, huo ni ushamba.
  mimi binafsi ninakaribia mwezi sijaanzisha thread yoyote, lakini nachangia thread za wengine, ni busara kukaa kimya kuliko kuongea upumbavu.
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MATOLA umeongea Nazani wakuu wa JF wanapaswa kufikiria Jinsi ya Ku rank watu humu jamvini! Inatia shaka Senior Expert anaoa maoni kama ya mtoto wa darasa la kwanza! Inachefua sana. Ikiwezekana kuwe na means ya ku deduct marks kwa kila anayeleta hoja za kitoto ili iwe ngumu kwa watu kufikia Level Ya Expert or senior expert member!
   
 6. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi jana nilishiriki maandamano.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Najua mnaona sifa sana kuwa senior sijui JF senoir/premium, mimi kwangu hilo si tatizo kuitwa/kuandikwa great thinker, nyinyi simnataka sifa za kijinga.
  narudi kwenye maada, hapa tunachokijua wote ni kwamba atakaesifia chadema huyo ndo great thinker, (know this is poor thinking).
  Hebu jiulizeni CUF wameshinda mara ngapi zanzibar? kwanini hawajawahi kutangazwa washindi (sote ni mashahidi kuwa CUF walishinda). ukifikiria sana hapo utaona kuna jambo?
  Hivi unafikiri hata kama wangekataa CCM wangekubali? Yawezekana wangeshitakiwa hata akina mkapa kwa mauaji ya raia wake kwa kutumia vyombo vya dola, je wako tayari kuona haya? Jumuiya za kimataofa zinaweza fanya yale yaliyowapata akina Pierre Bemba, charles Tylor etc. kama mnakumbukumbu fupi, siku ya kumalizia kampeni pale jangwani mkapa alisema huo muafaka ni kwamba wao wawe wapili? au mmesahau nyie mnaojiita great thinker? wangekataa alafu damu ikamwagika tena ya raia wa zanzibar mngefurahi? Yapo mengi tu suala ni kwamba nyinyi ni wavivu wakufikiria. Suala hapa la mhimu ni katiba mpya au yenye mabadiliko tu. Otherwise hamna kitu. CUF wameandamana jana lakini wameambulia mabomo. Tunajua watu fulani wamefuri sana. lakini sisi hilo halitusumbi, so long we know what will be our fate.
   
Loading...