Ningekuwa CC ya CHADEMA ningemsamehe Kitila Mkumbo

Watu aina ya Dr. Kitilaa hawafai kusamehewa hata kidogo. Wasiliti na wahaini siku zote upigwa risasi tena hadharani bila huruma, kwani bila kufanya hivyo nchi au taasisi hazitaacha kupinduana na kuleta machafuko miongoni mwa raia na vyombo vyake vya usalama.
 
Siyo kila anayekuja na mawazo tofauti au mtizamo tofauti ni mwanaCCM. Acheni utoto huo. Ni kwa lipi baya nililomsema Ben Saanane? Sijawahi kutofautiana na Ben Saanane, ila nimemtolea mfano tu, focus ya mjadala hapa ni Kitila, kama una la kuchangia kuhusu Kitila fanya hivyo.

Akili ya Bavicha ipo hivi kwa sababu ya bange na viroba!

1620987_688701521226278_62794813_n.jpg
 
Kitila Mkumbo ni msomi aliyebobea na hata ushauri wake ni wa kisomi. Kweli kakosea ila kusamehewa pia kungefaa sana maana hata kumvua nyadhifa zake ni adhabu ya kwanza tosha. Ila yote yamepita ikitokea tena tupunguze hasira kabla ya kufanya maamuzi.
 
mawazo mazuri hata vitabu vya mungu vinahimiza kusameheana.Lakini mueleze kawatuma mumuombee radhi? au afute kauli zake
 
Salit mpenzi wako au mchumba na hata mke au mume lakn c taasisi. Pabaya hapo, khusu ben sa8 kwa uelewa wangu yeye alwasaliti wakna zito na ndo mana zto anamtuhum ben ati yeye anamuingilia kwenye mawacliano private. Na polc mpka juz wanamsumbua ben. Mkumbo ---- mtu na phd unaendeshwa na ---- zto kana kwamba hatumii akil.
 
Umeshasema ungekuwa cc ya Chadema, sasa kwa kuwa wewe siyo cc, kaa kimya, usibeze kazi iliyofanywa na cc, sababu hujui waliwaza nini mpaka wakafikia maamuzi yale, usicheze ngoma usiyoielewa, cc ndiyo inayomjua vilivyo Dr Kitila Mkumbo na makosa aliyokuwa akiyafanya, wewe siyo cc kama ulivyokili mwenyewe, na ni vigumu kujua nini kinaendelea ndani ya cc, ukisema kafanya kosa moja tu, unakosea, sababu wewe upo nje ya mfumo, pia kusema kuna watu walifanya uamuzi kwa kufuata mihemko, huko ni kuikosea heshima cc, sababu yale siyo maamuzi ya mtu binafsi, after low, wewe siyo Chadema, na kama upo Chadema wewe ni mamluki, wenzio tunatengeza future, wewe unakomaa na furish past, acha utoto.
 
Mi natamani wote warudi tuanze upya, msamaha ungekibeba sana chadema kuliko hii timua timua
 
Mwl. wangu Kitila nimekusamehe lakini SITASAHAU uliyoyafanya kwa chama.
 
Watanzania wengi bado wapo katika hali ya tahayari kufuatia kufuatia maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA (CC) kuwafukuza wanachama wake watatu ambao walikuwa na majina makubwa ndani ya chama hicho. Ni wazi kuwa CHADEMA haikumuangalia mtu usoni, ikarusha lungu lake bila kujali linamwangukia nani.

Nikiwa kama mwanachama wa CHADEMA, kwanza naunga mkono maamuzi ya CHADEMA kwa ujumla wake kwa kuwa yanajaribu kukitofautisha na vyama vingine vinavyolinda zaidi uenzetu badala ya kusimamia sheria na taratibu za uongozaji wa chama na pia katiba ya vyama vyao. Katika hili, CHADEMA imetuaminisha kwamba hata ikishika dola, itakuwa tayari kumuwajibisha yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na miiko ya uongozi, atakayeisaliti nchi, kuitia aibu na hata kutusababishia hasara au kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa vyenye kuisababishia umaskini nchi yetu na watu wake. Katika hili nakipongeza CHADEMA chama changu.

Pamoja na pongezi hizi, bado naona kwamba maamuzi haya yalikuwa ni ya haraka, na pengine yalitokana na mihemuko ya baadhi ya wanachama. Nasema hivi kwa sababu, katika ushiriki wa MM, M1 na M3 katika uandaaji wa waraka wa siri 2013, mmojawao ambaye ni Kitila Mkumbo alikubali makosa mara moja baada ya waraka huu kugunduliwa, alikuwa tayari kuachia ngazi kama sehemu ya uwajibikaji kwa kosa alilofanya, na hata pale alipotakiwa kwenda mbele ya kamati kujitetea, alifanya hivyo tofauti na wenzake walivyofanya ambao waliamua kutoroka na hata kukimbilia mahakamani. Ni dhahiri kwamba yeye kwa nafasi yake aliyajutia makosa yake na akaonyesha nia ya kutubu na kuendelea kukitumikia chama chake. Tayari Dr. Mkumbo ameshaaminiwa na chama kwa mambo mengi na makubwa, na kwa hakika ameshawekeza vya kutosha kwa ajili ya chama, ilitosha kumsamehe na kumpa onyo.

Nikitazama nyuma, katika utumishi wake ndani ya chama; tofauti na wenzake yeye hajawahi kuwa na kashfa yoyote wala kushiriki kwa namna yoyote kukihujumu chama. Kwa mfano ukimtazama mtu kama Mwigamba, tayari alishawahi kutofautiana na chama kiasi cha kufikia kuondolewa katika nafasi yake ya uhasibu kule makao makuu. Wakati Zitto ameshajihusisha mara kadhaa katika vitendo vyenye kutiliwa shaka ikiwemo kuendesha kikundi cha PM7 ambacho kilifanya kazi ya kuwachafua viongozi kwa nia ya kumjenga Zitto. Lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia kujihusisha na lolote.
Ninawaza ya kwamba kama chama hiki kilikuwa tayari kumsamehe Ben Saanane, ambaye alikuwa ndiye master planner wa mkakati mzima wa kumpindua Mbowe na Slaa kwa faida ya Zitto, hasa baada ya kukosa nafasi BAVICHA, ni kwa vipi kimeshindwa kumsamehe Kitila ambaye alishiriki kuedit tu waraka huu wa kuwaangusha akina Mbowe?

Bado ninaona kwamba Kitila ana mapenzi mema na chama hata kama kwa sasa amekata tamaa na kutamani mbadala wa CCM na CHADEMA. Nafikiri yaanzishwe mazungumzo kati ya chama na Kitila ili kuona ni namna gani anaweza kurudi chamani na ikiwezekana atimize ndoto zake za kuwa mbunge wa Singida kupitia CHADEMA na apewe onyo ili akitumikie chama kwa uaminifu kwa mjibu wa katiba ya chama.

Nina matamanio makubwa ya kuona Kitila anarudi CHADEMA. Kama NCCR mageuzi walimsamehe Kafulila, ni kwa vipi CHADEMA washindwe kumsamehe Kitila na ukizingatia kuwa ni kosa lake la kwanza? Ni lazima tutambue kwamba kama binadamu tuna mapungufu yetu, and we are prone to mistakes. Haitashangaza sana iwapo itatokea kwamba hawa hawa wanaosimama kwenye CC ya CHADEMA na kutoa hukumu kali dhidi ya watu ambao wapo tayari kutubu na kujirekebisha wakafanya madudu makubwa kushinda haya.

Sijamsemea Zitto na Mwigamba kwa kuwa tayari walishakuwa na kashfa za utovu wa nidhamu ndani ya chama kiasi cha kustahili adhabu, lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia katika hayo.

Nawaombeni viongozi wa CHADEMA mpunguze hasira, na kutoa nafasi ya mazungumzo na mwanazuoni huyu, na ninamwomba sana Dr. Kitila apunguze hasira, ajirudi na kukubali mazungumzo na viongozi wa CHADEMA. Waswahili husema kosa moja haliachi mke, nami nasema kosa moja la Kitila lisitufanye tukose mchango wake mhimu kwa chama.

Mungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki CHADEMA!

umeongea la maana inawezekana kwenye hilo kind I ye alikua kifata mkumbo kama lilivyo jina lake
 
Last edited by a moderator:
Ninawaza ya kwamba kama chama hiki kilikuwa tayari kumsamehe Ben Saanane, ambaye alikuwa ndiye master planner wa mkakati mzima wa kumpindua Mbowe na Slaa kwa faida ya Zitto, hasa baada ya kukosa nafasi BAVICHA, ni kwa vipi kimeshindwa kumsamehe Kitila ambaye alishiriki kuedit tu waraka huu wa kuwaangusha akina Mbowe?

Nadhani una hoja nzuri, ila kwa mkutano wa waandishi wa habari ambao Kitila Mkumbo alishiriki mara baada ya kutimuliwa, ni dhahiri alistahili kuchukuliwa hatua. Hata kuomba kwake msamaha na kutaka kujiudhulu nyazifa zake, kuna uwezekano ulikuwa ni ujanja ili bado aendelee kubaki kwenye chama na kuendelea kukibomoa kwa kivuli cha uanachama.
Ila kuhusu la Ben Saanane, uko sahihi kabisa maana operationi PM7 ilikuwa hatari zaidi kuliko hiyo ya akina Kitila, na yawezekana ndiyo iliyozaa pia hizo harakati za akina Kitila. Hata hivyo, makosa mawili yanayofanana hayafanyi moja liwe sawa. Chama kama kilikosea kumwacha huru Ben Saanane, hakitakiwi kufanya kosa hilohilo kwa kumwacha huru Kitila Mkumbo.
 
Watanzania wengi bado wapo katika hali ya tahayari kufuatia kufuatia maamuzi ya kamati kuu ya CHADEMA (CC) kuwafukuza wanachama wake watatu ambao walikuwa na majina makubwa ndani ya chama hicho. Ni wazi kuwa CHADEMA haikumuangalia mtu usoni, ikarusha lungu lake bila kujali linamwangukia nani.

Nikiwa kama mwanachama wa CHADEMA, kwanza naunga mkono maamuzi ya CHADEMA kwa ujumla wake kwa kuwa yanajaribu kukitofautisha na vyama vingine vinavyolinda zaidi uenzetu badala ya kusimamia sheria na taratibu za uongozaji wa chama na pia katiba ya vyama vyao. Katika hili, CHADEMA imetuaminisha kwamba hata ikishika dola, itakuwa tayari kumuwajibisha yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na miiko ya uongozi, atakayeisaliti nchi, kuitia aibu na hata kutusababishia hasara au kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa vyenye kuisababishia umaskini nchi yetu na watu wake. Katika hili nakipongeza CHADEMA chama changu.

Pamoja na pongezi hizi, bado naona kwamba maamuzi haya yalikuwa ni ya haraka, na pengine yalitokana na mihemuko ya baadhi ya wanachama. Nasema hivi kwa sababu, katika ushiriki wa MM, M1 na M3 katika uandaaji wa waraka wa siri 2013, mmojawao ambaye ni Kitila Mkumbo alikubali makosa mara moja baada ya waraka huu kugunduliwa, alikuwa tayari kuachia ngazi kama sehemu ya uwajibikaji kwa kosa alilofanya, na hata pale alipotakiwa kwenda mbele ya kamati kujitetea, alifanya hivyo tofauti na wenzake walivyofanya ambao waliamua kutoroka na hata kukimbilia mahakamani. Ni dhahiri kwamba yeye kwa nafasi yake aliyajutia makosa yake na akaonyesha nia ya kutubu na kuendelea kukitumikia chama chake. Tayari Dr. Mkumbo ameshaaminiwa na chama kwa mambo mengi na makubwa, na kwa hakika ameshawekeza vya kutosha kwa ajili ya chama, ilitosha kumsamehe na kumpa onyo.

Nikitazama nyuma, katika utumishi wake ndani ya chama; tofauti na wenzake yeye hajawahi kuwa na kashfa yoyote wala kushiriki kwa namna yoyote kukihujumu chama. Kwa mfano ukimtazama mtu kama Mwigamba, tayari alishawahi kutofautiana na chama kiasi cha kufikia kuondolewa katika nafasi yake ya uhasibu kule makao makuu. Wakati Zitto ameshajihusisha mara kadhaa katika vitendo vyenye kutiliwa shaka ikiwemo kuendesha kikundi cha PM7 ambacho kilifanya kazi ya kuwachafua viongozi kwa nia ya kumjenga Zitto. Lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia kujihusisha na lolote.
Ninawaza ya kwamba kama chama hiki kilikuwa tayari kumsamehe Ben Saanane, ambaye alikuwa ndiye master planner wa mkakati mzima wa kumpindua Mbowe na Slaa kwa faida ya Zitto, hasa baada ya kukosa nafasi BAVICHA, ni kwa vipi kimeshindwa kumsamehe Kitila ambaye alishiriki kuedit tu waraka huu wa kuwaangusha akina Mbowe?

Bado ninaona kwamba Kitila ana mapenzi mema na chama hata kama kwa sasa amekata tamaa na kutamani mbadala wa CCM na CHADEMA. Nafikiri yaanzishwe mazungumzo kati ya chama na Kitila ili kuona ni namna gani anaweza kurudi chamani na ikiwezekana atimize ndoto zake za kuwa mbunge wa Singida kupitia CHADEMA na apewe onyo ili akitumikie chama kwa uaminifu kwa mjibu wa katiba ya chama.

Nina matamanio makubwa ya kuona Kitila anarudi CHADEMA. Kama NCCR mageuzi walimsamehe Kafulila, ni kwa vipi CHADEMA washindwe kumsamehe Kitila na ukizingatia kuwa ni kosa lake la kwanza? Ni lazima tutambue kwamba kama binadamu tuna mapungufu yetu, and we are prone to mistakes. Haitashangaza sana iwapo itatokea kwamba hawa hawa wanaosimama kwenye CC ya CHADEMA na kutoa hukumu kali dhidi ya watu ambao wapo tayari kutubu na kujirekebisha wakafanya madudu makubwa kushinda haya.

Sijamsemea Zitto na Mwigamba kwa kuwa tayari walishakuwa na kashfa za utovu wa nidhamu ndani ya chama kiasi cha kustahili adhabu, lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia katika hayo.

Nawaombeni viongozi wa CHADEMA mpunguze hasira, na kutoa nafasi ya mazungumzo na mwanazuoni huyu, na ninamwomba sana Dr. Kitila apunguze hasira, ajirudi na kukubali mazungumzo na viongozi wa CHADEMA. Waswahili husema kosa moja haliachi mke, nami nasema kosa moja la Kitila lisitufanye tukose mchango wake mhimu kwa chama.

Mungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki CHADEMA!

tulishafunga mjadala huu kiherehere cha nini tunawaza bunge la katiba mpya mijitu mingine ametumwa au imejituma
 
Last edited by a moderator:
Hawawezi kumsamehe. Chuki iliopo ni kubwa mno. Sharti alilopewa Kitila ni kumkana Zitto. Yeye akakataa kata kata. Wana ukaribu mno na Zitto kwa kiwango ambacho kila mtu haelewi. Yaani ni kama kumwambia Lema amkana Mbowe!
 
Kitila Mkumbo ni msomi aliyebobea na hata ushauri wake ni wa kisomi. Kweli kakosea ila kusamehewa pia kungefaa sana maana hata kumvua nyadhifa zake ni adhabu ya kwanza tosha. Ila yote yamepita ikitokea tena tupunguze hasira kabla ya kufanya maamuzi.

Wawa samehe wote Zitto, Kitila na Mwigamba. Wakisha samehewa wasipewe cheo chochote ndani ya chama kwa muda fulani wakiwa kwenye matazamio na uangalizi maalumu, siku wajumbe wa chadema wakijiridhisha kwamba wamebadilika mtazamo na kurudi kundini kwa dhati basi wanaweza wapa vyeo pia. Ni mawazo yangu tu jamani mimi mwanachama wa chadema pia.
 
Pamoja na pongezi hizi, bado naona kwamba maamuzi haya yalikuwa ni ya haraka, na pengine yalitokana na mihemuko ya baadhi ya wanachama. Nasema hivi kwa sababu, katika ushiriki wa MM, M1 na M3 katika uandaaji wa waraka wa siri 2013, mmojawao ambaye ni Kitila Mkumbo alikubali makosa mara moja baada ya waraka huu kugunduliwa, alikuwa tayari kuachia ngazi kama sehemu ya uwajibikaji kwa kosa alilofanya, na hata pale alipotakiwa kwenda mbele ya kamati kujitetea, alifanya hivyo tofauti na wenzake walivyofanya ambao waliamua kutoroka na hata kukimbilia mahakamani. Ni dhahiri kwamba yeye kwa nafasi yake aliyajutia makosa yake na akaonyesha nia ya kutubu na kuendelea kukitumikia chama chake. Tayari Dr. Mkumbo ameshaaminiwa na chama kwa mambo mengi na makubwa, na kwa hakika ameshawekeza vya kutosha kwa ajili ya chama, ilitosha kumsamehe na kumpa onyo.

Ninawaza ya kwamba kama chama hiki kilikuwa tayari kumsamehe Ben Saanane, ambaye alikuwa ndiye master planner wa mkakati mzima wa kumpindua Mbowe na Slaa kwa faida ya Zitto, hasa baada ya kukosa nafasi BAVICHA, ni kwa vipi kimeshindwa kumsamehe Kitila ambaye alishiriki kuedit tu waraka huu wa kuwaangusha akina Mbowe?

Bado ninaona kwamba Kitila ana mapenzi mema na chama hata kama kwa sasa amekata tamaa na kutamani mbadala wa CCM na CHADEMA. Nafikiri yaanzishwe mazungumzo kati ya chama na Kitila ili kuona ni namna gani anaweza kurudi chamani na ikiwezekana atimize ndoto zake za kuwa mbunge wa Singida kupitia CHADEMA na apewe onyo ili akitumikie chama kwa uaminifu kwa mjibu wa katiba ya chama.

Nina matamanio makubwa ya kuona Kitila anarudi CHADEMA. Kama NCCR mageuzi walimsamehe Kafulila, ni kwa vipi CHADEMA washindwe kumsamehe Kitila na ukizingatia kuwa ni kosa lake la kwanza? Ni lazima tutambue kwamba kama binadamu tuna mapungufu yetu, and we are prone to mistakes. Haitashangaza sana iwapo itatokea kwamba hawa hawa wanaosimama kwenye CC ya CHADEMA na kutoa hukumu kali dhidi ya watu ambao wapo tayari kutubu na kujirekebisha wakafanya madudu makubwa kushinda haya.

Sijamsemea Zitto na Mwigamba kwa kuwa tayari walishakuwa na kashfa za utovu wa nidhamu ndani ya chama kiasi cha kustahili adhabu, lakini Mkumbo hatukuwahi kumsikia katika hayo.

Nawaombeni viongozi wa CHADEMA mpunguze hasira, na kutoa nafasi ya mazungumzo na mwanazuoni huyu, na ninamwomba sana Dr. Kitila apunguze hasira, ajirudi na kukubali mazungumzo na viongozi wa CHADEMA. Waswahili husema kosa moja haliachi mke, nami nasema kosa moja la Kitila lisitufanye tukose mchango wake mhimu kwa chama.

Mungu ibariki Tanzania!
Mungu ibariki CHADEMA!
Mkuu Kyafulilo, japo mimi sio Chadema, ila kiukweli nimeguswa na andiko lako kiukweli kweli!.
Naamini kama Chadema ina watu kama wewe, then amini usiamini nyinyi ndio mtakuja kuikomboa Chadema na kuifanya ikabidhiwe nchi!.

Umeandika very bonafide and genuine concern kumhusu Dr. Kitila. My opinion ni Dr. Kitila is one of the best brains Chadema has ever had!. Naomba nisieleze machungu yang kwa maamuzi ya mihemiko na double standards za CC ya Chadema!. nimefarijika kujua kumbe Chadema in a some few real people, wise, humble wanamini in humility and forgiveness vs confrontations, hatred, kukomoana na kukomeshana!.

Kiukweli kama mtazamaji wa nje ya box, ule waraka ulikuwa ni kutengeneza a "winning coalition" ningependa wakosaji wote wahukumiwe kwa haki huku wakitendewa haki!.

Baada ya kuwatimua kina Shonza kinyeme cha sheria, taratibu na kanuni, niliwasisitiza [h=3]Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea haki Watanzania...[/h]
Ubarikiwe sana!.

Pasco
 
Ndio maana wewe sio CC ya CHADEMA, CC ya CHADEMA ina consist watu wenye upeo wa kuona mbali pamoja na kubaini watu waliojivika ngozi ya kondoo, Dr Kitila alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wamejivika ngozi ya kondoo.

Sasa hivi anasema wazi kuwa anahitaji mbadala wa CCM na CHADEMA, Unahitaji ushahidi gani kuamini kuwa lengo la Kitila na mawakala wake lilikuwa ni kuua CHADEMA???. Unataka kumbakisha mtu kwenye chama ambaye lengo lake ni kuua chama???
 
Back
Top Bottom