Ningekuwa Balozi Dr. Slaa ningeuliza tena: Is Lowassa a liability or an asset to CCM?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Alihama CCM na sasa amerejea 'nyumbani'. Alipojiunga na CHADEMA,aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Balozi Dr. Wilbrod Slaa alijitokeza na kutoa hotuba ndefu kuhusu kujiweka pembeni na siasa za vyama.

Pamoja na mambo mengine,Balozi Slaa aliweka wazi kutomuunga kwake mkono Lowassa ndani ya CHADEMA/UKAWA kwa kumchambua vilivyo kwenye mkutano wake wa Serena Hotel na hata mahojiano yake kwenye runinga ya StarTV ya jijini Kwanza.

Balozi Slaa aliwataka viongozi na wanachama wa CHADEMA/UKAWA kujiuliza kama Lowassa ni liability au asset.Kwake Balozi Slaa,Lowassa alikuwa liability kwa CHADEMA/UKAWA. Kwake yeye,Lowassa hakufaa na hivyo alijitenga naye.

Sasa Lowassa amerejea CCM anakokuita nyumbani. Kwanini swali la iwapo Lowassa ni liability au asset kwa CCM hivisasa lisiulizwe na kujibiwa na makada wa CCM na hata Balozi Slaa? Wale 'waliomkimbia Lowassa CHADEMA/UKAWA watamkimbia tena huko CCM?

Wakati utajibu hadi kusaza...
 
Hakuna mahala popote dr. Slaa alitangaza kujiunga ccm na hakuna siku yoyote dr. Slaa alitamka kugombea uongozi wowote ccm. Hivyo itambulike dr.Slaa ni mtumishi wa umma kama walivyo watumishi wengine wasio na vyama. Dr. slaa alikataa kumnadi fisadi lowasa akiwa katibu mkuu chadema kwaiyo lowasa kurudi ccm nyumbani kwa mafisadi hakumfanyi kuwa msafi ni fisadi tu. dr. Slaa hausiani na chama chochote kwasasa ilo swali ungewauliza viongozi wa chadema na ccm kwamba je lowasa sasa ni fisadi au mtu wa mabadiliko? baada kusuguliwa bafuni na kina mbowe kwasasa polepole nae anamsugua
 
Sio lazima aulize, tokea aachane na siasa hajawahi kuzungumzia tena masuala ya siasa. Muacheni mzee amalizie uzee wake.

Halafu mnadhani kuwa Balozi lazima uwe mwanaccm ndio maana mnamuandama.
.... Wanaelewa tatizo kukimbiwa na lowasa wamevurugwa kabisa lawama wanamuangushia dr. Slaa wakati mchawi wao ni mbowe na genge lake kumkabizi chama fisadi na mafuriko yake. Yaani kuazima mgombea kutoka ccm na cuf hahahaaaaaa wamesahau kwamba chakuazima akistili makalio
 
Hakuna mahala popote dr. Slaa alitangaza kujiunga ccm na hakuna siku yoyote dr. Slaa alitamka kugombea uongozi wowote ccm. Hivyo itambulike dr.Slaa ni mtumishi wa umma kama walivyo watumishi wengine wasio na vyama. Dr. slaa alikataa kumnadi fisadi lowasa akiwa katibu mkuu chadema kwaiyo lowasa kurudi ccm nyumbani kwa mafisadi hakumfanyi kuwa msafi ni fisadi tu. dr. Slaa hausiani na chama chochote kwasasa ilo swali ungewauliza viongozi wa chadema na ccm kwamba je lowasa sasa ni fisadi au mtu wa mabadiliko? baada kusuguliwa bafuni na kina mbowe kwasasa polepole nae anamsugua
Wapi kwenye mada yangu nimesema Dr. Slaa ni CCM?
 
Lowasa alikua aidha Liability au Asset, pale tu alipohamia chadema akitokea ccm ili agombee urais. Huu ndiyo ulikua wasiwasi wa Dr.Slaa. Sasa amekaa chadema miaka 3, maisha yamemshinda na kuamua kurudi nyumbani;

Sasa hapa Dr. Slaa mbona hahusiki kulijibu swali ambalo kimsingi aliwauliza viongozi na wanachama wenzake kabla ya kufikia hitimisho la kujitenga na siasa! Hivyo basi swali hili bado linawahusu wanachadema wote watujibu kwa sababu ndiyo walioulizwa na huyo balozi wetu Dr. Slaa.
 
Alihama CCM na sasa amerejea 'nyumbani'. Alipojiunga na CHADEMA,aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Balozi Dr. Wilbrod Slaa alijitokeza na kutoa hotuba ndefu kuhusu kujiweka pembeni na siasa za vyama.

Pamoja na mambo mengine,Balozi Slaa aliweka wazi kutomuunga kwake mkono Lowassa ndani ya CHADEMA/UKAWA kwa kumchambua vilivyo kwenye mkutano wake wa Serena Hotel na hata mahojiano yake kwenye runinga ya StarTV ya jijini Kwanza.

Balozi Slaa aliwataka viongozi na wanachama wa CHADEMA/UKAWA kujiuliza kama Lowassa ni liability au asset.Kwake Balozi Slaa,Lowassa alikuwa liability kwa CHADEMA/UKAWA. Kwake yeye,Lowassa hakufaa na hivyo alijitenga naye.

Sasa Lowassa amerejea CCM anakokuita nyumbani. Kwanini swali la iwapo Lowassa ni liability au asset kwa CCM hivisasa lisiulizwe na kujibiwa na makada wa CCM na hata Balozi Slaa? Wale 'waliomkimbia Lowassa CHADEMA/UKAWA watamkimbia tena huko CCM?

Wakati utajibu hadi kusaza...
Angeuliza kama nani wasomi wengine cjui huwa unafikiri nn. Tumieni akili zenu vizuri. Tanzania naona wasomi wengi ni sawa na alienda shule na wanazidiwa na hata wasioenda shule
 
Back
Top Bottom