Chikawe Jr
Member
- Jun 6, 2017
- 23
- 85
Kuna kanuni inasema ""anayekuringishia vyako alivyokuibia mwambie basi sivitaki tena"" ndio njia pekee ya kujikwamua na maumivu ya muda mrefu yanayotokana na kuibiwa au kudhulumiwa.
Kwa miaka 20, Tanzania imeingia katika Rushwa na UFISADI mkubwa na kusababisha kundi la watu wachache kuwa na NGUVU YA PESA na kutawala mzunguko wa fedha nchini. Hii imethibitika baada ya kikundi kidogo cha watu wenye maslahi ya kudumu ya kinyonyaji kuamua kuzifungia Pesa zao zilizokuwa katika mzunguko na kuzificha ndani(Home made shelves)
Athari kubwa iliyojitokeza baada ya kundi hili lenye nguvu kuficha UKWASI WAO ni pamoja na;-
1) Kupungua kwa fedha katika mzunguko.
2) Kupungua kwa uwezo wa kununua
3) Biashara za kati kufa
4) Kupotea kwa ajira za watu
5) Manung'uniko ya hali ngumu ya kiuchumi kwa watanzania hasa wa hali ya chini
Kwa uelewa wangu mdogo, pesa ni alama ya thamani katika kubadilishana huduma au bidhaa. Hakuna sababu iliyokuu ambayo inaweza kumfanya mtu akaficha pesa isipokuwa kuikomoa serikali na wananchi wake.
Wapo watu wanaosema pesa hizi zimebadilishwa 'interm of dollars' na kufichwa, lakini mimi nasema la hasha, pesa hizi zimefichwa katika hali yake ya Tshs. Kwa nini nasema hivyo, kuna sababu kuu 2 kama ifuatavyo;-
1) Kama ingekuwa zimefichwa interm of dollar, Tanzania tusingekuwa na changamoto ya mzunguko wa fedha hasa ndani kwa sababu Tshs ingekuwepo lakini Dollar ndio ingepotea sokoni.Ikumbukwe hakuna nchi yeyote duniani wanatumia currency yetu isipokuwa sisi wenyewe.
2) Changamoto ya kupungua kwa bidhaa zinazoingia nchini (Import trade) sio mitaji isipokuwa wanunuzi hawana uwezo wa kununua bidhaa sokoni kutokana na kupungua kwa fedha katika mzunguko wa maisha ya kila siku. (Currency flow in Business).
Katika hili tunaweza kujikwamua kwa njia nyingi lakini iliyo kuu ni Kubadilisha NOTI ya Elfu 10.
Kwanini kubadilisha NOTI ya elfu kumi kunaweza kutusaidia ni kwa sababu hakuna namna yoyote iliyobora itakayokuwezesha kumfanya mtu au kikundi cha watu walioficha fedha mafichoni isipokuwa tu watakapoona baada ya muda hazitatumika tena hivyo watalazimika kuziingiza katika mzunguko.
Na hili linaweza kusimamiwa kwa njia mbili
1) Kufanya uhakiki wa mitaji ya mabenki yote nchini
2) Kutoa tangazo la kusudio la kubadili NOTI ya elfu 10 na kuweka muda unaofaa kabla ya kuchukua hatua hiyo.
2) Kuweka viwango maalumu kwa mtu kubadilisha fedha zake katika mabenki ya kawaida na kama atazidi kiwango hicho basi atatakiwa kubadilisha fedha hizo Benki kuu kwa utaratibu maalumu.( Ninaposema utaratibu maalumu ni pamoja na kuhojiwa)
Kwa kufanya hivi tutatoa fursa kwa walioficha fedha kuchagua aidha fedha zao ziishie kuwa makaratasi ambayo hayatumiki tena au wayalete katika mzunguko na kuongeza uwekezaji.
Jambo hili lina tija kubwa kama litafanywa kitaalamu lakini nachelea kusema inawezekana wanaokushauri USIBADILI NOTI NAO WAMEFICHA MAJUMBANI MWAO.
Kama tunaweka mambo sawa basi hata ili linaweza kutusaidia
Nahitaji kuona hoja za wachumi hapa. Nini maoni yako?
Chikawe jr.
Sent using Jamii Forums mobile app