elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,260
- 9,704
- Thread starter
- #81
Mimi naona maisha ya ndoa ya wazazi wako yamekuadhiri kisaikolojia, unahitaji ushauri tu na kutiwa moyo.
Ni kweli kuna watu wanajuta kuoa/kuolewa na wenzi walionao kutokana na mifarakano ya hapa na pale na isiyoisha, ila watu hawaishi kuoa/kuolewa eti kwa vile kuna mifarakano kwenye ndoa fulani hata kama ni wazazi wako, wewe unapaswa kujifunza kutokana na makosa hayo na kudhamiria kutoyarudia makosa hayo kamwe katika ndoa yako, kumbuka wewe ni wewe, wao ni wao na sisi ni sisi.
Ukizaa bila kuishi na mwanamke utamuathiri sana mtoto kwani atapata malezi na makuzi ya ajabu sana na atakosa upendo wa wazazi wake wakiwa pamoja, na mwisho utakuja kujuta utapogundua mwanamke uliyezaa naye amaolewa na mtoto wako anateswa na baba wa kambo kiasi cha kunyimwa chakula. Usifanye hivyo ndugu yangu, wewe ni mtu mzima
(i hope so), jenga familia yako wewe mwenyewe, na usiige mtu hata kidogo maana ndoa hutengenezwa na wanandoa wenyewe kwa msaada wa Mungu.
Zaidi sana nakushauri mpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, utawaombea wazazi wako na wewe utaomba Mungu akupe mke mwema na wewe uwe mume mwema, barikiwa
Asante sana mkuu kwa ushauri wako umentia moyo