Ningalikuwa Makamba kamwe nisingaling'oka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ningalikuwa Makamba kamwe nisingaling'oka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shomoro, Nov 12, 2010.

 1. Shomoro

  Shomoro Senior Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 22, 2010
  Messages: 111
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wengi twamfahamu Katibu mkuu wa SISIEM anayesadikiwa kuwa na "mdomo mchafu" kuliko wote ambao wamepata kushika wadhifa huo. Wadau wengi baadhi wakiwa wanachama hai wa mapinduzi wanamshutumu kuwa ni chanzo cha chama hiko kikongwe kupoteza mwelekeo. Duru zinasema kuwa mtikisiko mkubwa ambao SISIEM imeupata katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni uthibitisho wa uongozi mbovu wa mkuu huyo. Ingawa mimi si shabiki wa SISIEM naona Makamba ana haki ya kujivinjari kwenye kiti chake kwa sababu sifuatazo.
  1. Licha ya tetesi kuwa kura zilizomrudisha bwana Kikwete madarakani ziliibwa (ama kuchakachuliwa kwa mujibu wa msamiati wa kisasa) bado Makamba amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mbinu zake za ushindi ingawa zilijaa kuwapaka matope wapinzani.
  2. Amefanikiwa kuzoa wabunge wengi ambao ni karibu 2/3 ya wabunge wote na hivyo kuli-control bunge.
  3. Ameweza kudhoofisha sana upinzani wa CUF na hivyo kubakia na msalaba mmoja tu ambao ni CHADEMA.
  4.Lakini kikubwa kuliko vyote ni kumwangusha chuma cha pua mkuu Samuel Sitta ambaye SISIEM walimwona kama muhogo mchungu na hatimaye kumsimika Mama Makinda. Ikumbukwe kuwa mama Makinda ni Spika wa kwanza mwanamke katika historia ya taifa letu.
  Kama nilivyowahi kumsikia mheshimiwa Makamba akinena nanukuhu "Mbaazi ukikosa maua husingizia jua" mimi nahisi bado jua halijamwakia vya kutosha na hivyo anastahili muda zaidi.
   
Loading...