Ninazidi kuamini Uchaguzi Mkuu 2015 ulikuwa huru na haki!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana uliohusisha Wabunge, Madiwani na Rais, wagombea mbalimbali ambao hawakuridhishwa na Matokeo ya Uchaguzi waliamua kufungua kesi kupinga ushindi kwa wabunge waliotangazwa kuibuka kidedea.

Mashauri zaidi ya 13 ya uchaguzi wa wabunge yaliyopelekwa mahakamani yameanza kutoa sura ya zoezi la uchaguzi Mkuu.

Katika kesi zote za ubunge zilizotolewa hukumu nchini, hakuna hata moja ambayo matokeo yametenguliwa. Hii inaonyesha uchaguzi ulikuwa huru na haki kwa kiwango kikubwa ambacho hakuna nafasi ambayo inaweza kubadilisha maamuzi ya wananchi kwa kutumia Mahakama.

Matokeo haya yanadhihirisha pia mahakama zetu zimeanza kuwa huru na hakuna rushwa katika kufanya maamuzi.

Hili ni funzo kwa wale wagombea ambao bado wanadhani wanaweza kubadilisha matokeo mahakamani na kinyume chake wakajikuta wanalipia gharama kubwa kifedha katika kuendesha kesi na fidia.

1) Gwiji wa siasa za Tanzania, Stephen Wasira amegaragazwa Mahakamani na mgombea wa CHADEMA, Ester Bulaya.

2) ‘Mzee wa nyeti za kuku’, James Lembeli amegaragazwa mahakamani na Mgombea wa CCM, Jumanne Kishimba

3) Ezekiah Wenje ameangukia pua mahakamani kupinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula.

4) Willy Mungai wa CHADEMA amegaragazwa mahakamani na mgombea ubunge wa Jimbo la Mafinga wa CCM, Cosato Chumi.

5) Samora Kanje wa CCM amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Rombo kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Selasini

6) Emmanuel Masonga wa CHADEMA amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Njombe Kusini kwa tiketi ya CCM, Edward Mwalongo.

7) Dk. Luca Siame wa CCM amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Momba kwa tiketi ya CHADEMA, David Silinde.

9) Augustino Mrema wa TLP aliamua kuweka kwapani mafaili yake na kuondoka mahakamani baada ya kugundua hawezi kushinda kesi aliyofungua kupinga ushindi wa James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.

10) Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ilitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Iringa Mjini, yaliyompa ushindi Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi huo, Frederick Mwakalebela wa CCM.

11) David Kafulila wa NCCR-Mageuzi amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Kigoma Kusini, Husna Mwilima wa CCM.

Kesi nyingine bado zinaendelea kusikilizwa mahakamani lakini dalili zinazidi kuonyesha ni kilio kwa wale walifungua kesi za kupinga matokeo.

Kinachoshangaza Edward Lowassa bado anadai aliibiwa kura zake za Urais wa Tanzania na mpaka sasa hajamtambua Dk. John Magufuli kama Rais wa Tanzania! Nadhani hata viongozi wengine ndani ya CHADEMA wanamshangaa!
 
Endelea kuamini tu hivyohivyo
 
Hivi teuzi za ukuu wa Wilaya ni lini jamani? Hizo post bora zitoke tuu mapema angalao watu akili ziwarudi na waanze kufikiria kwa kina na kushughulisha bongo zao.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Na zike milion 15 za kufungulia kesi vp zitarudishwa au ndo imekula kwao
 
uchaguzi huru na haki hua hauamiliwi na mahakama, unaamuliwa kwenye sanduku la kura
 
Baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana uliohusisha Wabunge, Madiwani na Rais, wagombea mbalimbali ambao hawakuridhishwa na Matokeo ya Uchaguzi waliamua kufungua kesi kupinga ushindi kwa wabunge waliotangazwa kuibuka kidedea.

Mashauri zaidi ya 13 ya uchaguzi wa wabunge yaliyopelekwa mahakamani yameanza kutoa sura ya zoezi la uchaguzi Mkuu.

Katika kesi zote za ubunge zilizotolewa hukumu nchini, hakuna hata moja ambayo matokeo yametenguliwa. Hii inaonyesha uchaguzi ulikuwa huru na haki kwa kiwango kikubwa ambacho hakuna nafasi ambayo inaweza kubadilisha maamuzi ya wananchi kwa kutumia Mahakama.

Matokeo haya yanadhihirisha pia mahakama zetu zimeanza kuwa huru na hakuna rushwa katika kufanya maamuzi.

Hili ni funzo kwa wale wagombea ambao bado wanadhani wanaweza kubadilisha matokeo mahakamani na kinyume chake wakajikuta wanalipia gharama kubwa kifedha katika kuendesha kesi na fidia.

1) Gwiji wa siasa za Tanzania, Stephen Wasira amegaragazwa Mahakamani na mgombea wa CHADEMA, Ester Bulaya.

2) ‘Mzee wa nyeti za kuku’, James Lembeli amegaragazwa mahakamani na Mgombea wa CCM, Jumanne Kishimba

3) Ezekiah Wenje ameangukia pua mahakamani kupinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula.

4) Willy Mungai wa CHADEMA amegaragazwa mahakamani na mgombea ubunge wa Jimbo la Mafinga wa CCM, Cosato Chumi.

5) Samora Kanje wa CCM amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Rombo kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Selasini

6) Emmanuel Masonga wa CHADEMA amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Njombe Kusini kwa tiketi ya CCM, Edward Mwalongo.

7) Dk. Luca Siame wa CCM amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Momba kwa tiketi ya CHADEMA, David Silinde.

9) Augustino Mrema wa TLP aliamua kuweka kwapani mafaili yake na kuondoka mahakamani baada ya kugundua hawezi kushinda kesi aliyofungua kupinga ushindi wa James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.

10) Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ilitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Iringa Mjini, yaliyompa ushindi Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi huo, Frederick Mwakalebela wa CCM.

11) David Kafulila wa NCCR-Mageuzi amegaragazwa mahakamani na mgombea wa Jimbo la Kigoma Kusini, Husna Mwilima wa CCM.

Kesi nyingine bado zinaendelea kusikilizwa mahakamani lakini dalili zinazidi kuonyesha ni kilio kwa wale walifungua kesi za kupinga matokeo.

Kinachoshangaza Edward Lowassa bado anadai aliibiwa kura zake za Urais wa Tanzania na mpaka sasa hajamtambua Dk. John Magufuli kama Rais wa Tanzania! Nadhani hata viongozi wengine ndani ya CHADEMA wanamshangaa!
Ningewaamini zaidi kama tume ya uchaguzi itaundwa na vyama vyote pia hisiwe inawajibika kwa rais wa Tanzania hapo ndio utaona kama CCM uwa kila jimbo wanashinda kweli ama laah
 
Wale nyumbu wa mbowe ngoja waje utasikia mahakama ni za CCM
Sina tatizo kama mchangiaji atakuja na hoja yenye nguvu za hoja.

Mjinga anayetaka kujifunza atafunzwa.

Mpumbavu pia atajibiwa kama ulivyo upumbavu wake.
 
Back
Top Bottom