Ninayokumbuka nikiwa shule ya msingi miaka ya 1980 huko Dodoma Kijiji cha Mpwayungu

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,319
2,000
Somo tajwa hapo juu lahusika. Twende kazi

1. Kwenda na kuni, maji, miti kwa ajili ya kufungia miti ya mizabibu

2. Kwenda shule na kinyesi cha ng'ombe kwa ajili ya kutandaza chini ili kupiga mtama

3. Kulima mashamba ya walimu na kupukuchua mahindi yao

4. Kwenda na majivu shuleni kwa ajili ya kupendezesha mawe na madhari ya shule

5. Michezo ya UMITASHUMTA

6. Kuweka kambi shule zaidi ya moja inapokaribia kufanya mtihani wa darasa la 7

7. Kukaguliwa meno, kucha, nyayo na kwenye pindo za kaptula na shati tukiwa paredi

8. Kukimbia mchaka mchaka chinja

9. Kupiga pushapu

10. Kulima mashamba ya shule

11. Kuiba zabibu za shule

12. Niliwahi mgomea Mwalimu wangu asinichape fimbo, akanitimua mbiyo

13. Kuchelewa shule na kujificha kichakani au HADO

14. Kunywa uji usio kuwa na sukari

15. Kuweka madaftari mfuko wa nyuma

16. Kujaladia madaftari

17. Daftari la mwandiko mistari midogo na mikubwa

18. Niliwahi kuwa kiranja mkuu nikawa sichapwi mboko

19. Somo la uraia, historia, jogi, sayansi kimu. Vita vya maji maji

20. Hesabu za mafumbo

21. Mr na Mrs Daud, Neema na Baraka

22. Kufagia chini barabarani kwa kutumia ufagio wa majani

23. Nilikuwa natumia cha-cha-cha na raba aina ya DHU yaani Dingi Hana Uwezo

24. Nilikuwa napendelea kuvaa "cost" yaani chupi yenye rangi nyingiiii na ki-uzi katikati. Ambayo iliwahi kuchanika na kupanda kifuani wakati nacheza mpira

25. Nilikuwa napenda kukaa nyuma, monita wa darasa akawa ananoandika sana mpiga kelele

26. "Naam Mwalimu...Jana na leo"

Mungu acha aitwe Mungu.

Wewe je mwenzangu unakumbuka nn shule ya msingi?

Karibuni
 

kipwate

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
525
500
Na kumbuka vingi tu mkuu....
1: Jumatatu ilikuwa siku ngumu sana shule ilikuwa ya jeshi na muda mwingi jumatatu walimu walikuwa wanatoka zamu wana uchovu wamesha vurugaa hizo hasira zao wana malizia kwao ole wako ukose number na ucheleww mstarini utaisoma number
2:na miss kampani ya washikaji maana walimu walikuwa wanazingua sana watu kuchanganyika kijinsia hususani nje ya darasa unakuta muda wa mapumziko masela tuko kivyetu na wadada kivyao.
3:mchakamchaka wa ijumaa,kuja na mbolea,mbegu za michongoma kwa ajili ya kupendezesha shule wavivu walikuwa wakikosa wana chukua mkaaa wana ponda kidgo wanaomba baadh ya mbegu za michongoma kwa watu wakitikisa hivi unaona kweli jamaa kaja na mbegu za mchongoma
4:mkipiga kelele ghafla ukimya ukitawala mtasikia watu wanasema shetani kapita
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom