Ninawiwa kusema huyu MC Gara B anapendwa mno na hawa wanawake!

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
3,979
5,295
Leo hakuna cha salamu, nimeshaona kwa wanawake zaidi ya wanne wa jamaa zangu wakiwalazimisha waume zao kuwa liwalo na liwe kwenye events zao Mc ni lazima awe GaraB.

Sio mbaya, jamaa yupo vizuri na anafanya kazi nzuri. Napongeza kwa hilo. Shida ni hawa wake zetu hususani huyu wangu, karibu kila event ya GaraB anang'ang'ania kwenda.

Linaweza kuwa jambo zuri, ila kama mwanaume nasononeka mno kwa wife kuonesha kuvutiwa na events za jamaa japo ni jambo zuri!

Ila nimeongeza umakini na uangalifu kwa mke wangu kipindi hiki cha ujauzito wake, kuhusu mambo yake ya kuvutiwa na huyu MC.

Yaani kazini karibia wadada wote wanaonesha kumkubali mno GaraB mpaka wengine wanakiri kuwa tayari hata awafanye mipango ya kando tu.

Daaah! Hasara na pole kubwa kwa waume zao.
 
Back
Top Bottom