GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,548
- 108,859
Kwa mfano mwaka juzi ( 2013 ) nilianza kufanya master's degree yangu ya miaka miwili ambapo nimeweza kusoma karibu masomo yote stahili japo yawezekana nikawa nina vimeo ( sups ) kama za masomo mawili hivi pamoja na kuandaa research proposal yangu na kuandika dissertation yangu na mwaka huu ( 2015 ) nilitakiwa kumaliza mwezi october na kuhitimu rasmi mwezi november lakini ghafla mambo ya hapa na pale yameingiliana hivyo imenibidi nisitishe masomo ili nijipange upya kipesa na nimalizie masomo yangu mwakani ( 2016 ). Maswali yangu kwenu ni haya yafuatayo :
Maswali yangu makubwa kwenu ni hayo matano ( 5 ) tu na nitashukuru kama nitapata majibu ya kisomi kama siyo ya kitaaluma zaidi kutoka kwenu nikiamini kuwa humu kuna wabobezi wa kila aina wa masuala mbalimbali na pia kuna wahadhiri wa vyuo mbalimbali wenye uzoefu wa kutosha.
Wasalaam na jioni njema wapendwa.
- Je nitajiita ni msomi wa shahada wa pili au bado nitabaki na status ile ile kuwa nina first degree?
- Je nikiomba kazi nitumie cv ya masters japo bado sijamaliza au nitumie ile ile tu ya bachelor's degree?
- Je mtu akisema kuwa nina elimu gani niseme nina bachelor's degree au master's degree?
- Je nitakapomaliza hiyo mwakani badala ya mwaka huu kutakuwa na positive and negative impact gani kwangu kitaaluma?
- Je psychologically haitaniathiri nitakapoona wenzangu nilioanza nao kusoma wao wanahitimu mwaka huu na mimi nimesitisha hadi mwakani? Na kama itakuwepo ni jinsi gani nitajiweka sawa kisaikolojia ili nisiathirike?
Maswali yangu makubwa kwenu ni hayo matano ( 5 ) tu na nitashukuru kama nitapata majibu ya kisomi kama siyo ya kitaaluma zaidi kutoka kwenu nikiamini kuwa humu kuna wabobezi wa kila aina wa masuala mbalimbali na pia kuna wahadhiri wa vyuo mbalimbali wenye uzoefu wa kutosha.
Wasalaam na jioni njema wapendwa.