Ninaweza kuanza kutumia matokeo yangu ya Masters?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,823
2,000
Kwa mfano mwaka juzi ( 2013 ) nilianza kufanya master's degree yangu ya miaka miwili ambapo nimeweza kusoma karibu masomo yote stahili japo yawezekana nikawa nina vimeo ( sups ) kama za masomo mawili hivi pamoja na kuandaa research proposal yangu na kuandika dissertation yangu na mwaka huu ( 2015 ) nilitakiwa kumaliza mwezi october na kuhitimu rasmi mwezi november lakini ghafla mambo ya hapa na pale yameingiliana hivyo imenibidi nisitishe masomo ili nijipange upya kipesa na nimalizie masomo yangu mwakani ( 2016 ). Maswali yangu kwenu ni haya yafuatayo :


  1. Je nitajiita ni msomi wa shahada wa pili au bado nitabaki na status ile ile kuwa nina first degree?
  2. Je nikiomba kazi nitumie cv ya masters japo bado sijamaliza au nitumie ile ile tu ya bachelor's degree?
  3. Je mtu akisema kuwa nina elimu gani niseme nina bachelor's degree au master's degree?
  4. Je nitakapomaliza hiyo mwakani badala ya mwaka huu kutakuwa na positive and negative impact gani kwangu kitaaluma?
  5. Je psychologically haitaniathiri nitakapoona wenzangu nilioanza nao kusoma wao wanahitimu mwaka huu na mimi nimesitisha hadi mwakani? Na kama itakuwepo ni jinsi gani nitajiweka sawa kisaikolojia ili nisiathirike?

Maswali yangu makubwa kwenu ni hayo matano ( 5 ) tu na nitashukuru kama nitapata majibu ya kisomi kama siyo ya kitaaluma zaidi kutoka kwenu nikiamini kuwa humu kuna wabobezi wa kila aina wa masuala mbalimbali na pia kuna wahadhiri wa vyuo mbalimbali wenye uzoefu wa kutosha.

Wasalaam na jioni njema wapendwa.
 

kinyangesi

JF-Expert Member
Jul 15, 2012
247
225
Kama umemalza course work maana yake una masters, unaweza hata kuajiriwa vyuoni. Kwenye CV uweke bt useme in dissertation stage.
Itkuathiri vizur wenzio wakimalza nawe ukibaki, kama una uwezo jitahd umalze kwa muda!
 

I and myself

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
318
500
Sizani kama utakuwa tayari una masters apo mana hata ukiweka hayo matokeo mwisho wa siku wata taka cheti cha masters.. kitu ambacho hauna mpaka sasa.. pili kama una vimeo ndo kabisa... navyo fahamu mimi ili uwe una masters tayari lazima uwe ume clear kila kitu kuanzia course work na research.. ila advantage uliyo nayo utakuwa una uelewa mpana kuliko mtu wa bachelor japo uta kuwa upo level moja nae mana huna cheti cha masters
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom