Ninawaza kuanzisha kitu kinachoitwa Tantech Association, naomba ushirikiano wenu

Sep 1, 2024
45
93
Hello,

Mimi ni mwanafunzi wa Shule ya sekondari Tambaza kidato cha tano katika mchepuo wa PMCs. Naitwa Baraka Range.

Napenda kuwashirikisha wadau wote wa tasnia ya teknolojia katika wazo langu la kuanzisha kitu kinaitwa Tantech Association ambayo itawasaidia vijana kuweza kuunganisha na wadau mbalimbali ambao ni wazoefu katika idara ya teknolojia.

Pia vijana wabunifu watapata nafasi za kuonyesha vumbuzi zao mbalimbali kwa wadau wao ili kuweza kupata misaada mbalimbali. Naombeni ushirikiano wenu ili kuweza kufanikisha jambo hili.
 
Sasa wewe upo form 5, unataka kuacha shule?
 
Kuwashirikisha kwenye nini ?
Wazo ?
Prototype ?
au Working Modal ?

Kuna Mdau mmoja ambaye sasa hivi ni gwiji (tena alichukua ideas za wadau wengine) alishasema Ideas are one thing..., but execution is the Key....

Kama una wazo na una wadau anza polepole na wadau wako jenga community na mwisho wa siku unaweza kuuza hata product yako (in such things most people pay for the community / users)
 
Sasa wewe upo form 5, unataka kuacha shule?
it's not about kuacha shule it's about on how youth one can be helped from downward to upward through getting experience from different computer experts from Tanzania.

Thinks that twice bro.,Vijana ambayo tunahitaji kuendelezea teknolojia ya nchi yetu tunaumia hivyi..Hii haitasaidia tu vijana ambao wana vumbuzi bali itasaidia watu wote wanaohitaji kujifunza teknolojia

Nchi yetu ina watu mbalimbali katika teknolojia kwanini wasigawe ujuzi wao kwa watu wengine? ndo maana nikawaza association hii ambayo itawaunganisha vijana mbalimbali na computer experts mbalimbali wa nchini Tanzania...
 
Shukrani sana unanipa moyo na ujasiri wa kuendelea,, 🙏🏽 Na naamiini hii kitu ikianzishwa itakuja saidia vijana wengine nchini Tanzania pia itasaidia watu waweze kupata elimu mbalimbali juu ya teknolojiaa maana Tantech itachapisha material mbalimbali ya kiteknolojia kutoka kwa wazoefu wa teknolojia nchini.
 
vyote wazo,prototype pia working modal ambayo itasaidia vijana kuongeza ujuzi katika juu ya maswala ya kiteknolojiaa
Haujanielewa..... Wewe una nini ? Kina Bill Gates na Rafiki yake hawakuja na kuwatangazia watu wana idea gani au wadau walioanzisha VLC Player (wanachuo kama experiment zao hawakuja kutangazia watu tunataka kufanya kitu gani from thin air); Walijikusanya wao kama marafiki wakafanya jambo wakiwa hapo Chuo na mwisho wa siku wakatangazia umati...

Kwahio ndio maana nimekuuliza wewe una nini....

Wazo ?: Just an idea / concept na hauna lolote lingine ndio unakuja kwetu tukupe idea au jinsi ya kukamilisha wazo lako....
Prototype: Tayari una hio portal na inaweza kufanya kazi ila bado haujapata wadau ndio unataka waingie ili uweze kuprove concept
Working Model: Tayari na wadau unao na inafanya kazi kabisa unataka tu kuongezea wadau na kuboresha...
 
Back
Top Bottom