Ninawashangaa sana wana CCM wanaoshangilia ujio wa wahamiaji ndani ya chama chao!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Nina washangaa sana hawa watu na kwa kweli sielewi wanashangilia nini!

Mtu anahamia ndani ya chama chao ili apate ulaji (Achukue nafasi ya mwana CCM ambaye pengine angekumbukwa kwenye hiyo nafasi) kisha yeye anakaa anashangilia kama zuzu!

Hivi doctor Mashinji, Machali, Kafulila na wengine wengi sampuli ya kina Waitara, Gekul etc, walienda CCM kukiimarisha chama? Ni asset?

Hawa nawahakikishieni kuwa jogoo hatowika kabla hamjaanza kuwavurumishia mawe na maneno makali! Muda utaongea.
 
Kama hukuwashangaa wanaCHADEMA waliokuwa wakishangilia ujio wa hao wahamiaji hupaswi kuwashangaa wanaCCM!

Mamvi alikuja huko kama taasis na safu yake akina Makene wakawekwa pembeni na bado mlimpigia mbinja na kumdekia leo ndo mmezinduka!

Watu wanashangilia mpinzani wao kujifia kibudu,vyeo baadae!
 
Hii picha ina maelelzo mengi!
IMG-20150727-WA0013-729322.jpg
 
Nina washangaa sana hawa watu na kwa kweli sielewi wanashangilia nini!

Mtu anahamia ndani ya chama chao ili apate ulaji (Achukue nafasi ya mwana CCM ambaye pengine angekumbukwa kwenye hiyo nafasi) kisha yeye anakaa anashangilia kama zuzu!

Hivi doctor Mashinji, Machali, Kafulila na wengine wengi sampuli ya kina Waitara, Gekul etc, walienda CCM kukiimarisha chama? Ni asset?

Hawa nawahakikishieni kuwa jogoo hatowika kabla hamjaanza kuwavurumishia mawe na maneno makali! Muda utaongea.
Kumekuwa na wimbi la post za ajabu kama hizi tokea kushuhudiwa wimbi la wahamiaji wenye influence toka upinzani hususan chadema.
Wanataka kujaribu kuchonganisha wanaccm na viongozi wao au na wageni.
Kimsingi hakuna mgeni anakuja kuchukua nafasi ya mtu kama mgeni huyo tayari ni mwanachama wa CCM...! Katika history ni Mbatia pekee ndio alichukua nafasi za wenyeji pale alipoteuliwa kuwa mbunge akiwa ni kiongozi wa NCCR MAGEUZI. Athari yake mpaka leo yeye ni mbunge kwani alipewa paltform, exposure,na rasilimali fedha alivyotumia kugombea ubunge na kumuwezesha kushinda.
Mgeni mwingine yeyote, Madhali amepewa fursa akiwa mwanachama mpya, haina shida. Zaidi ni motisha kwa wageni.
Aidha waliopewa ubunge na udiwani kama walikuwa na vyeo hivyo kabla ni halali yao kwani wewe au yule anayedai amepokwa fursa jiulize ulishindwaje kuwa Mbunge au Diwani badala yake akawashinda wanaccm?
Leo kaja yeye na wafuasii wake japo wachache, kaleta na cheo alichokuwa nacho halafu mbinafsi mmoja anataka kuhoji?
Ulitaka abaki hukohuko tukipiganie kwa gharama?.
Kwangu mimi nitaona tabu sana kama Vincent Mashinji atapewa cheo cha Dr. Bashiru na awe SG was CCM..!!!
Lakini kama atapewa ukurugenzi, udc au urc au ukatibu mkuu wa wizara au Ubalozi bado sioni shida kwa sababu nafasi hizo hazikuwa na watu walokuwa kwenye foleni wanangojea zamu.
Yeyote anayedai wageni wanachukua fursa ni mbinafsi, mchonganishi mtetea tumbo tu. Hebu fikiria leo kuna wanachama 15milioni je kuna nafasi ngapi!?
Wako wadau wanaojitolea sana lkn hawafikirii au kutegemea hata ubalozi wa shina au umesenja ofisi za serikali... Wao wana mapenzi ya kweli tu. Kama kuna mtu anakipigania chama ili apate uongozi huyo hafai, apishe.
Ndio maana tulimzonga NAPE alipoinua mkono na kudai mkono wake imeiingiza ccm madarakani.
Hakupaswa kusema hivyo badala yake alipaswa kutambua kwamba yeye ndio alipewa fursa na chama, na haikumaanisha kwamba chama hakikuwa na mtu bora zaidi wa kukaa pale, au hajui kuwa wakati yeye akifanya kazi kwa kulipwa kuna mamilioni ya wanaccm walipigana mitaani na vijijini bila kulipwa na wakati mwingine kwa gharama zao...!?
Ukiwa mwanachama wa chama chochote kukipigania chama ni WAJIBU na kupewa fursa ni PRIVILEGE tu.
Suala la msingi ni kuwepo kwa mchakato huru wa kidemokrasia ktk kupata wateule wa CHAMA kwenye uchaguzi mkuu, lkn sio chaguzi ndogo zinazofanywa baada ya kuwatongoza walioshinda....
 
Siasa ni sayansi bwashee.

Vijana wangu ndio hao wanaorejea Lumumba kwa kasi baada ya kukamilisha majukumu ya kimkakati hapo Ufipa!
Inawezekana uwezo wako wa kufikiri kutokana na uchakavu umefikia kwenye point of retardation. Bora upumzike kwani unachofanya ni upotoshaji na wakati mwingine kuwatia hatiani hata wale unaodhani unawatetea. Unakumbuka umediriki kuleta hoja kinzani hapa kuwa Dr. Mashinji amekuja CCM ili afutiwe kesi ya jinai inayomkabili yeye na viongozi wengine waandamizi wa Chadema, ukionyesha kuwa kumbe Mahakama zetu haziko huru na zinaweza kupokea maagizo toka Lumumba. Jaribu kuwa na kiasi,usijione wewe ni CCM zaidi kuliko hiyo CCM yenyewe. Nafikiri wanaokulipa wataliona hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumekuwa na wimbi la post za ajabu kama hizi tokea kushuhudiwa wimbi la wahamiaji wenye influence toka upinzani hususan chadema.
Wanataka kujaribu kuchonganisha wanaccm na viongozi wao au na wageni.
Kimsingi hakuna mgeni anakuja kuchukua nafasi ya mtu kama mgeni huyo tayari ni mwanachama wa CCM...! Katika history ni Mbatia pekee ndio alichukua nafasi za wenyeji pale alipoteuliwa kuwa mbunge akiwa ni kiongozi wa NCCR MAGEUZI. Athari yake mpaka leo yeye ni mbunge kwani alipewa paltform, exposure,na rasilimali fedha alivyotumia kugombea ubunge na kumuwezesha kushinda.
Mgeni mwingine yeyote, Madhali amepewa fursa akiwa mwanachama mpya, haina shida. Zaidi ni motisha kwa wageni.
Aidha waliopewa ubunge na udiwani kama walikuwa na vyeo hivyo kabla ni halali yao kwani wewe au yule anayedai amepokwa fursa jiulize ulishindwaje kuwa Mbunge au Diwani badala yake akawashinda wanaccm?
Leo kaja yeye na wafuasii wake japo wachache, kaleta na cheo alichokuwa nacho halafu mbinafsi mmoja anataka kuhoji?
Ulitaka abaki hukohuko tukipiganie kwa gharama?.
Kwangu mimi nitaona tabu sana kama Vincent Mashinji atapewa cheo cha Dr. Bashiru na awe SG was CCM..!!!
Lakini kama atapewa ukurugenzi, udc au urc au ukatibu mkuu wa wizara au Ubalozi bado sioni shida kwa sababu nafasi hizo hazikuwa na watu walokuwa kwenye foleni wanangojea zamu.
Yeyote anayedai wageni wanachukua fursa ni mbinafsi, mchonganishi mtetea tumbo tu. Hebu fikiria leo kuna wanachama 15milioni je kuna nafasi ngapi!?
Wako wadau wanaojitolea sana lkn hawafikirii au kutegemea hata ubalozi wa shina au umesenja ofisi za serikali... Wao wana mapenzi ya kweli tu. Kama kuna mtu anakipigania chama ili apate uongozi huyo hafai, apishe.
Ndio maana tulimzonga NAPE alipoinua mkono na kudai mkono wake imeiingiza ccm madarakani.
Hakupaswa kusema hivyo badala yake alipaswa kutambua kwamba yeye ndio alipewa fursa na chama, na haikumaanisha kwamba chama hakikuwa na mtu bora zaidi wa kukaa pale, au hajui kuwa wakati yeye akifanya kazi kwa kulipwa kuna mamilioni ya wanaccm walipigana mitaani na vijijini bila kulipwa na wakati mwingine kwa gharama zao...!?
Ukiwa mwanachama wa chama chochote kukipigania chama ni WAJIBU na kupewa fursa ni PRIVILEGE tu.
Suala la msingi ni kuwepo kwa mchakato huru wa kidemokrasia ktk kupata wateule wa CHAMA kwenye uchaguzi mkuu, lkn sio chaguzi ndogo zinazofanywa baada ya kuwatongoza walioshinda....
Una kiwango kidogo sana Cha maarifa
 
Ccm wanajua wananchi wanaikubali sana cdm, hivyo wanaamini wakiwanunua viongozi wa cdm, basi wananchi wataipenda na kuikubali ccm. Bila kujua mchezaji akihamia timu hahami na mashabiki wake.
Mchezaji skihamia timu hahami na mashabiki wake!!

Umesahau usajili wa Lowasa cdm je hakuhama na mashabiki wake? Mpira wa miguu usiulinganishe na siasa. Siasa mtu akiwa mbovu watu wanamtafuta aliko kiongizi wanaeamini atawavusha na kuwafikisha wanakokutaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom