Ninawashangaa CHADEMA kwa kutotaka CUF idhoofike au ife?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Kwa mtu yoyote anayefahamu siasa za Tanzania atafahamu kudhoofika au kufa kwa CUF ni kukomaa kwa CHADEMA.

Kama kweli CHADEMA wanaamini CUF ya Prof. Lipumba inadhoofika au inakufa kulingana na takwimu zilizotolewa na Tundu Lissu basi wangeacha iendelee kudhoofika au kufa chini ya Prof. Lipumba ili CHADEMA iimarike zaidi na kuwa chama kikubwa na kikuu nchini.

Demokrasia ya kweli haipimwi kwa wingi wa vyama vya siasa bali kwa nguvu ya kisiasa ya vyama vya siasa. Huwezi kupata nguvu ya kisiasa kama una utitiri wa vyama vyenye nguvu inakaribiana sawa kisiasa.

Tanzania inahitaji vyama viwili vikubwa vyenye nguvu ya kisiasa ili kupiga hatua ya kidemokrasia. Kinyume cha hivyo ni kupoteza muda na fedha za wananchi zinatolewa kwa njia ya ruzuku.

Uwepo wa chama kimoja kikubwa cha upinzani ungeilazimisha serikali kusikiliza madai au ushauri kwa makini na kikubwa zaidi ungerahisisha misimamo, mawasiliano na madai ya wadau wa maendeleo kama Watanzania, World Bank, IMF, EU, USA na China katika kusimamia madai ya upinzani.

Uwepo wa chama kimoja kikubwa cha upinzani utaondoa hata mitafaruku na migogoro ndani ya chama ambayo inaiathiri pia CHADEMA kwa njia moja au nyingine. Kwa mfano, kwa sasa mgogoro wa CUF umeiathiri pia CHADEMA kwa sababu ni moja ya chama kinachounda UKAWA.

Badala ya CHADEMA kushughulikia masuala mengine, kwa sasa inawabidi waelekeze nguvu zao kwenye matatizo yaliyoko ndani ya CUF pamoja na kwamba Katiba ya CUF haiwatambui.

Tusishangae baada ya kumaliza mgogoro wa CUF, tutasikia tena matatizo mengine yanaibuka ndani ya NCCR-Mageuzi ambapo itabidi CHADEMA waanze tena kuhangaika na matatizo ya NCCR-Mageuzi.

Baadaye kuna NLD ambayo pia inaweza kuingia kwenye mgogoro wa utawala.

Uwepo wa vyama vingi vya upinzani vyenye nguvu sana unasababisha muongezeko wa migogoro na matatizo ndani ya chama ambayo yanasababisha hata vyama vingine kupatwa na matatizo.

Kwa mfano, CUF imara inaweza ikapata mgombea maarufu kutoka CCM wakati huo huo CHADEMA ina mgombea pia maarufu ndani ya chama au kutokea CCM. Matatizo ya kupata wagombea wawili ni tatizo ambalo linaondolewa na uwepo wa chama kimoja kikubwa cha upinzani.

Wataalam wa magonjwa ya milipuko wana njia mbili za kupambana na tatizo hilo ambazo ni Isolation and quarantine. Isolation separates sick people with a contagious disease from people who are not sick while Quarantine separates and restricts the movement of people who were exposed to a contagious disease to see if they become sick.

Kwa mantiki ya kisiasa, isolation ni CHADEMA kuwa na chama kimoja kikubwa na kikuu cha upinzani wakati quarantine ni kutokuwa kwenye umoja wa UKAWA.

Hii ina maana kuwa kama CHADEMA ingekuwa isolated au kwenye quarantine isingepata matatizo yanayoipata CUF. Kwa maana nyingine, hata kama ingepata matatizo ingekuwa ni rahisi kupambana nayo na kushinda.

Kwa nini CHADEMA hawataki CUF ife ili wasiwe exposed kwenye mitafaruku ya kisiasa.
 
chadema hawataki CUF ife??Hayo ni mawazo ya Jumla, lwa ufupi chadema wanataka kuiteka CUF ili isiwe na nguvu bali ifanye kazi kwa matamko ya chadema!Hakuna namna chadema wanaweza kuwa na nia njema ya moja kwa moja kwa CUF maana nao ni threat!CUF imara hasa huku bara ni hatari sana kwa chadema
 
Rafiki yako akiuliwa unafurahi?
Shetani/ccm utamjua kwa matendo yake tu, ila mjue plan yenu imefikia njie subirini ile plan yenu ya kuiba kura tu.
 
1. Katiba yetu inasema nini juu ya idadi ya vyama vya siasa?

2. Muungano wowote huanzia kwenye moja au nyingi kuwa moja....kwanini UKAWA na nini kinaunda ukawa?

3. Je zipi sababu za msingi zinazopelekea kuwa na vyama vingi kimuundo....

4. Kwanini ccm isiungane na wengine woote ili hatime mwisho tuwe na vyama viwili tu yaani CDM na CCM....Kwanini haiwi hivyo?

nitarudi ukijibu hayo maswali kwa hatua moja baada ya jingine na kwa idadi.
 
chadema hawataki CUF ife??Hayo ni mawazo ya Jumla, lwa ufupi chadema wanataka kuiteka CUF ili isiwe na nguvu bali ifanye kazi kwa matamko ya chadema!Hakuna namna chadema wanaweza kuwa na nia njema ya moja kwa moja kwa CUF maana nao ni threat!CUF imara hasa huku bara ni hatari sana kwa chadema
Mbona Tundu Lissu alisema uwepo wa Prof. Lipumba ndani ya CUF unaifanya idhoofike kila siku. Alienda mbali zaidi na kutoa takwimu za uchaguzi zinazoonyesha jinsi ambavyo CUF inadhoofika kila mwaka.

Kwa nini wasimuache aendelee kuidhoofisha ili isiwe na nguvu.
 
1. Kwahiyo hoja yako CUF ife?

2. wewe unaumwa nini ikiishi?

3. Kunasehem yoyote katiba inazuia vyama ama wanachama wasishirikiane au wasisaidiane? weka hapa hicho kifungu.
 
Maswali yako yamejibiwa kwenye mada.
 
Kwa mtu yoyote anayefahamu siasa za Tanzania atafahamu kudhoofika au kufa kwa CUF ni kukomaa kwa CHADEMA.

Kama kweli CHADEMA wanaamini CUF ya Prof. Lipumba inadhoofika au inakufa kulingana na takwimu zilizotolewa na Tundu Lissu basi wangeacha iendelee kudhoofika au kufa chini ya Prof. Lipumba ili CHADEMA iimarike zaidi na kuwa chama kikubwa na kikuu nchini.

Demokrasia ya kweli haipimwi kwa wingi wa vyama vya siasa bali kwa nguvu ya kisiasa ya vyama vya siasa. Huwezi kupata nguvu ya kisiasa kama una utitiri wa vyama vyenye nguvu inakaribiana sawa kisiasa.

Tanzania inahitaji vyama viwili vikubwa vyenye nguvu ya kisiasa ili kupiga hatua ya kidemokrasia. Kinyume cha hivyo ni kupoteza muda na fedha za wananchi zinatolewa kwa njia ya ruzuku.

Uwepo wa chama kimoja kikubwa cha upinzani ungeilazimisha serikali kusikiliza madai au ushauri kwa makini na kikubwa zaidi ungerahisisha misimamo, mawasiliano na madai ya wadau wa maendeleo kama Watanzania, World Bank, IMF, EU, USA na China katika kusimamia madai ya upinzani.

Uwepo wa chama kimoja kikubwa cha upinzani utaondoa hata mitafaruku na migogoro ndani ya chama ambayo inaiathiri pia CHADEMA kwa njia moja au nyingine. Kwa mfano, kwa sasa mgogoro wa CUF umeiathiri pia CHADEMA kwa sababu ni moja ya chama kinachounda UKAWA.

Badala ya CHADEMA kushughulikia masuala mengine, kwa sasa inawabidi waelekeze nguvu zao kwenye matatizo yaliyoko ndani ya CUF pamoja na kwamba Katiba ya CUF haiwatambui.

Tusishangae baada ya kumaliza mgogoro wa CUF, tutasikia tena matatizo mengine yanaibuka ndani ya NCCR-Mageuzi ambapo itabidi CHADEMA waanze tena kuhangaika na matatizo ya NCCR-Mageuzi.

Baadaye kuna NLD ambayo pia inaweza kuingia kwenye mgogoro wa utawala.

Uwepo wa vyama vingi vya upinzani vyenye nguvu sana unasababisha muongezeko wa migogoro na matatizo ndani ya chama ambayo yanasababisha hata vyama vingine kupatwa na matatizo.

Kwa mfano, CUF imara inaweza ikapata mgombea maarufu kutoka CCM wakati huo huo CHADEMA ina mgombea pia maarufu ndani ya chama au kutokea CCM. Matatizo ya kupata wagombea wawili ni tatizo ambalo linaondolewa na uwepo wa chama kimoja kikubwa cha upinzani.

Wataalam wa magonjwa ya milipuko wana njia mbili za kupambana na tatizo hilo ambazo ni Isolation and quarantine. Isolation separates sick people with a contagious disease from people who are not sick while Quarantine separates and restricts the movement of people who were exposed to a contagious disease to see if they become sick.

Kwa mantiki ya kisiasa, isolation ni CHADEMA kuwa na chama kimoja kikubwa na kikuu cha upinzani wakati quarantine ni kutokuwa kwenye umoja wa UKAWA.

Hii ina maana kuwa kama CHADEMA ingekuwa isolated au kwenye quarantine isingepata matatizo yanayoipata CUF. Kwa maana nyingine, hata kama ingepata matatizo ingekuwa ni rahisi kupambana nayo na kushinda.

Kwa nini CHADEMA hawataki CUF ife ili wasiwe exposed kwenye mitafaruku ya kisiasa.

Hii tamaa ya kwenda ikulu hii!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom