Ninawapiga fumbo, je mtaweza kulifumbua fumbo langu? Haya tuendelee

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
NINAWAPIIGIA FUMBO JE MUTAWEZA KULIFUMBUWA FUMBO LANGU? HAYA TUENDELEE.............

Mjomba kweli ulisema ukiondoka tutakukumbuka
wala sio utani tunakukumbuka sana mjomba
mana huyu uliyemuachia familia kawa hatari

kweli kweli imefikia hatua ukileta mchezo kidogo
anakufukuza kabisa kwenye ukoo na ikibidi
anakufunga,hatukuzoea hivyo mjomba

nakumbuka ilikuwa tukikosea kwenye familia
unatuhamishia kwa shangazi au ujombani
angalau tujirekebishe mjomba ..duhhh
nakukumbuka sana.

Mjomba enzizako MTU alikuwa akileta kelele
hatakama nimemuonea namuuliza unanijua Mimi
ni nani kwenye familia hii ntakufunga milele sasa
hivi ni tofauti sana mjomba yani kuwa kwenye

familia tu imekuwa mzigo mana huyu
uliyemkabizi familia akisikia tu unatumia cheo
kuwaumiza wengine umekwisha lazima
akutumbue...

Mjomba safari za kwenda sehemu mbalimbali za
kifahari kula bata kwako zilikuwa zakufikia yani

huyu sasa uliyemkabidhi sasa hivi akisikia
umesafiri bila ruhusa yake mana lazima uwe na
sababu za Msingi ukisafiri kinyemela umekwisha
lazima akuminye...

Mjomba unakumbuka rafiki zetu na ndugu zetu
walikuwa hawalipii kuingiza vyombo vywao kwetu
ila sasa hivi huyu uliyempa hata kijiko lazima

ulipie .yani ni hivi mjomba familia imekuwa
chungu mana kila kitu kinaenda kwa bajeti kama
Leo ni kande wote tutakula,nakukumbuka sana

mjomba mana wakati wako ilikuwa kula
nyumbani ni mpaka ukipenda lakini sasa hivi ni
lazima mana ukijifanya mbishi utakufa njaaaa,

Mjomba nyama choma imebaki story,unakumbuk
a mjomba nilikuwa silagi nyanya chungu ila sasa
hivi nakula vizuri,mjomba ofa sikuizi si wapi

watu,mjomba ile range nimeipaki nyumbani mana
inadaiwa unajua nikiitembelea hawa wasasa hivi
wakiikamata hawatataka kujua Mimi ni nani

watataka nilipe ......dah Nina mengi mjomba ila
kiukweli ulisema tutakukumbuka tena
mapemaaaaaaaaa kabla jua halijazama.ila poa

sio mbaya mana toka umemkabidhi kaka familia
kiasi flani tumeanza kueshimiana mjomba najua
huwezi rudi ila siku ukijisikia tusalimie hata
kwanjia ya simu....

Swali langu Mjomba huyo ni mjomba Gani?Na aliye achiwa Urithi na Mjomba ni Mjomba gani tena mwengine? Nijibuni jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom